Ni suala la muda tu kabla CCM hawajatuletea 'Magufuli' mwingine

Ni suala la muda tu kabla CCM hawajatuletea 'Magufuli' mwingine

1. Ben Sanane
2. Azory Gwanda
3. Wananchi zaidi ya 300 wa MKIRU
4. Kushambuliwa Tundu Lissu
5. Kumteka Mo Dewji
We ni bendera fuata upepo, Azory gwanda ,Aquilina, na Dr ulimboka kungolewa kucha na meno ni Awamu ya nne.

Vp mbona jk hujampa Jina baya?
 
CCM walilazimika kumpa madaraka Magufuli kutokana na mazingira ya wakati ule ila walidhani wangeweza kumdhibiti. Magufuli akawashangaza na kuwafumba midomo hata wale ambao walidhani wangekuwa na sauti juu yake. Mmoja wa watu pekee ambaye NADHANI bado alibaki na kauwezo fulani ka kumkemea alikuwa ni Benjamin Mkapa.

Lakini kwa wengine Magufuli alikuwa too much. Si vigogo si nani, wote waliishi kwa hofu wasijue mzee anaweza akaamka na maamuzi gani juu ya maisha yao.

Sasa hivi CCM wako comfortable, Mama ameweza kuwadhibiti watu wa Magufuli. Polepole kamalizwa kisiasa kwa kupewa ubalozi na wengine kama kina Mwigulu ndiyo wanachafuliwa CV zao za kuwamaliza kabisa kisiasa.

Ila ninachoona CCM ni chama kinachotapatapa. Toka 1995 ni chama ambacho ni nusu mfu. Chochote wanachoweza kujishikizia ili waendelee tu kubaki madarakani, wanafanya hivyo. Siyo tena habari za itikadi au principles. Kwa maneno ya Kolimba, ni chama kilichopoteza dira na muelekeo.

Kesho wanaweza kumtengeneza 'Magufuli' mwingine ambaye watajiaminisha wataweza kumdhibiti tofauti ya yule wa nyuma au mazingira yatawalazimisha kumuunga mkono, na watatulazimisha tumkubali. Na kama kawaida yetu, tutakuwa tunarudia makosa ya nyuma bila kujifunza chochote kwa yaliyopita.
Haifai kabisa kutokea kiongozi dizaini ya yule bwana
 
We ni bendera fuata upepo, Azory gwanda ,Aquilina, na Dr ulimboka kungolewa kucha na meno ni Awamu ya nne.

Vp mbona jk hujampa Jina baya?
We kweli rababendi, Aqwilina ni wakati wa Jk? na Azory gwanda wakati wa Jk!? Ngosha aliharibu kweli akili zenu,mmekuwa mazuzu
 
..hapana.

..matendo ya Magufuli hayakuwa yanaendana na mtu ambaye yuko karibu na anashauriwa na Ben Mkapa.

..Magufuli angekuwa anashauriwa na Mkapa asingeharibu taswira ya nchi kimataifa na kidiplomasia kiasi kile.
Ebu tueleweshe jinsi taswira ya nchi ilivyoharibiwa kwa mifano halisi pamoja na hasara na faida zake tofauti na sasa!
 
Na kama kawaida yetu, tutakuwa tunarudia makosa ya nyuma bila kujifunza chochote kwa yaliyopita.
Kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa - Mwl. JK Nyerere.
When faced with hard choices to choose in between the two devils, better choose the devil you know, than a devil you don't know, hivyo Watanzania tutaendelea kilichagua zimwi litujualo... simply kwa sababu we have no choices to choose from, au tuna mbadala wowote wa kuchagua from?.
P
 
Ajabu dua hizo hamzielekezi kwenye kuomba kuondokana na mizizi ya matatizo yetu kama kuondoa ccm au kupata katiba mpya.
Na wewe inaruhusiwa kuomba hiyo dua, CCM ni janga la kitaifa wote tushiriki kuitokomeza
 
1. Ben Sanane
2. Azory Gwanda
3. Wananchi zaidi ya 300 wa MKIRU
4. Kushambuliwa Tundu Lissu
5. Kumteka Mo Dewji
We ni bendera data upepo, Azory gwanda ,Aquilina, na Dr ulimboka kungolewa kucha na me ni Awamu ya nne.

Vp mbona jk hujampa Jina baya?
We kweli rababendi, Aqwilina ni wakati wa Jk? na Azory gwanda wakati wa Jk!? Ngosha aliharibu kweli akili zenu,mmekuwa mazuzu
Usikurupuke kama Nyumbu. Tafuta records
 
CCM walilazimika kumpa madaraka Magufuli kutokana na mazingira ya wakati ule ila walidhani wangeweza kumdhibiti. Magufuli akawashangaza na kuwafumba midomo hata wale ambao walidhani wangekuwa na sauti juu yake. Mmoja wa watu pekee ambaye NADHANI bado alibaki na kauwezo fulani ka kumkemea alikuwa ni Benjamin Mkapa.

Lakini kwa wengine Magufuli alikuwa too much. Si vigogo si nani, wote waliishi kwa hofu wasijue mzee anaweza akaamka na maamuzi gani juu ya maisha yao.

Sasa hivi CCM wako comfortable, Mama ameweza kuwadhibiti watu wa Magufuli. Polepole kamalizwa kisiasa kwa kupewa ubalozi na wengine kama kina Mwigulu ndiyo wanachafuliwa CV zao za kuwamaliza kabisa kisiasa.

Ila ninachoona CCM ni chama kinachotapatapa. Toka 1995 ni chama ambacho ni nusu mfu. Chochote wanachoweza kujishikizia ili waendelee tu kubaki madarakani, wanafanya hivyo. Siyo tena habari za itikadi au principles. Kwa maneno ya Kolimba, ni chama kilichopoteza dira na muelekeo.

Kesho wanaweza kumtengeneza 'Magufuli' mwingine ambaye watajiaminisha wataweza kumdhibiti tofauti ya yule wa nyuma au mazingira yatawalazimisha kumuunga mkono, na watatulazimisha tumkubali. Na kama kawaida yetu, tutakuwa tunarudia makosa ya nyuma bila kujifunza chochote kwa yaliyopita.
Haiwezekani
 
Na wewe inaruhusiwa kuomba hiyo dua, CCM ni janga la kitaifa wote tushiriki kuitokomeza
Sasa mbona mliomba Magufuli afe na kuacha kuomba ccm ife? Matokeo yake bado mnaendelea kuangaika na matatizo yenu yaleyale ya siku zote.
 
Sasa mbona mliomba Magufuli afe na kuacha kuomba ccm ife? Matokeo yake bado mnaendelea kuangaika na matatizo yenu yaleyale ya siku zote.
Nyie vibaraka wa dikteta nasikia hamlipi tozo na mna maduka na masoko yenu maalum.
 
Vyama ni wanachama ambao ni watu. Huo upya wa vyama unatoka wapi wakati kina Odinga ni walewale kila uchaguzi! Utasikia leo odm, kesho narc, kesho kutwa azimio...

Hivi chadema ingeshinda 2015 kuna mtu mwenye akili angetamba kwamba ccm imeondoshwa madarakani?
Wewe mwenye akili. Unatumia njia GANI? KuiungANisha "CHADEMA" na "CCM"
 
Kama ni kweli basi magufuli alikuwa ni GENIUS
Alikuwa ni mshamba siyo genius. Genius person asingetumia njia ile aliyoitumia kumuua Tundu Lissu!! Angekuwa genius asingekufa kwa COVID-19.

Hatutaki kutawaliwa na washamba wa Kolomije tena
 
We ni bendera fuata upepo, Azory gwanda ,Aquilina, na Dr ulimboka kungolewa kucha na meno ni Awamu ya nne.

Vp mbona jk hujampa Jina baya?
Rabbon huna ubongo wa ku argue humu JF. Soma halafu pita mbali. Aquilina amekufa Januari 2018 wakati yule Kichaa wenu kamnunua Ally Mtulia hivyo basi ukaitishwa uchaguzi mdogo. Azory Gwanda naye aliuliwa Novemba 2018 akiripoti mauaji ya Kibiti.

Usipokuwa na facts Kaa mbali na jukwaa la wenye akili. Bakia Chitchat au Facebook
 
1. Ben Sanane
2. Azory Gwanda
3. Wananchi zaidi ya 300 wa MKIRU
4. Kushambuliwa Tundu Lissu
5. Kumteka Mo Dewji
Hao uliowataja ni takataka gani

Mbona kigoma tu hapo watu saba wa familia moja wameuawa kwa shoka katika utawala huuhuu? Wao siyo watu?

Vipi na hawa wako wapi?
Screenshot_20220817-164556_Chrome.jpg
20220727_205015.jpg
 
Back
Top Bottom