Nitakua mtu wa mwisho kuamini kua mauaji ya huyu ndugu yetu ni serikali yetu ya mama imeshiriki. Wahuni ni watu wabaya sana wanatumia mbinu zote kumchafua mama lakini mwisho wa yote watashindwa tu. Huu utekaji umeshamiri sasa hivi baada ya wahuni kutimuliwa kwenye baraza la mawaziri. Ila kwa vile wabongo wengi ni wapumbavu wataamini ni serkali ndio imefanya upuuzi huu.
Unachowaza na kufikiri ni kweli na ni sahihi...
Lakini unafikiri serikali (Rais Samia), Bunge na mahakama itakwepaje lawama iwapo hawachukui hatua stahiki kukomesha mauaji haya...?
Si ndiye Rais Samia huyu huyu alibeza malalamiko ya wananchi waathirika wa matukio haya kwa kusema "hizo ni drama tu.......??"
Kwa kauli hii ya Rais kwanini tusiseme kuwa kumbe serikali na vyombo vyake (polisi & TISS) ndiyo wahusika wa matukio haya kisha wanaenda kwa Rais na kumpa taarifa za uongo na kumfanya Rais aonekane kituko kwa raia...?
SIKILIZA BWANA: Rais anayo njia nzuri na salama kuitumia kuwang'amua hawa unaowaita wahuni iwe wapo ndani ya vyombo vya serikali kama polisi, TISS, jeshini, Baraza la mawaziri au wakiwa nje ya vyombo vya serikali....
Njia yenyewe ni Rais kutumia mamlaka yake ya U - RAIS, AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA, MKUU WA SERIKALI na zaidi MAMLAKA YA KIKATIBA kuunda kamati huru maalumu ya uchunguzi ya kijaji ili ichunguze mambo haya na kumpa ripoti....
Kamati haipaswi kuwa na polisi wala TISS maana hawa ndiyo wanatuhumiwa. Kwa kuwa wanatuhumiwa, hawataweza kujichunguza wenyewe badala yake wachunguzwe ili wasafishwe au watiwe hatiani kama wanahusika na Rais mwenye atajua cha kuwafanya kwa mujibu wa katiba....