Nyerere aliwafukuza kazi kina DGIS Emilio Mzena, Peter Siyovelwa, Peter Kisumo na maafisa usalama wengi tu miaka ya 70's kwasababu walifanya mauaji makubwa ya watanzania wasiokuwa na hatia. Mwaka 1975 akafanya
En Masse Recruitment na kuisuka upya idara ya usalama wa taifa, akiwafukuza Thugs and Sadists na kuajiri maelfu ya vijana wasomi kutoka chuo kikuu na sekondari.
Hili bado halikusaidia kwasababu usalama wa taifa chini ya Imran Kombe walikuwa kama A Loose Cannon, wanakamata, wanatesa, wanaua watu wakilazimisha ujamaa ambao umeshafeli. Imran Kombe alikuwa ana nguvu kama mungu mtu, vile. Moja ya chanzo cha kupitisha sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1996 ilikuwa ni malalamiko kwamba idara inaendeshwa kimajungu na kihuni-huni tu bila uwajibikaji wowote ule.
Jambo ambalo linashanganza ni kwamba sheria ya mabadiliko ya mwaka 2023 imeturudisha kulekule kwenye Pre-1996 ambako TISS haina Civilian Oversight, ati DGIS hawajibiki kwa MINISTER OF STATE na CHIEF SECRETARY, kwamba wao wanajifanyia tu wanachotaka kama ilivyo CIA. Wamepewa kinga (Immunity) na wanaruhusiwa kutengeneza (Paramilitary Forces) ambazo zitakuwa na makomandoo, wanajeshi na polisi.
Jeshi tayari tunalo, polisi tunao, hizi Paramilitary Forces za nini ?
Tena siku wameenda mbali kuwaruhusu kumiliki silaha wakiwa kweny kazi.
I
NA MAANA SASA:
-TISS watafanya operesheni na hakuna anayejua.
- Watapanga bajeti na CHIEF SECRETARY wala MINISTER OF STATE hafahamu.
- Watafanya Operesheni kubwa kwa idhini ya DGIS bila Civilian Oversight.
Huu ujinga hata World Class Intelligence Organisations kama CIA, MI6 na MSS uliwashinda. Shirika la kijasusi kuendeshwa bila Civilian Oversight is a recipe for disaster. Ubaya zaidi hata kwa bunge hawawajibiki, wanawajibika kwa Raisi. Siku nchi inatawaliwa na wahuni, unadhani kitatokea nini ?