Ni Tanzania pekee ambapo ujinga unatetewa na kundi kubwa la watu

Kwa mtazamo wangu jiwe kama mwanadamu mwingine yoyote Yule ana mazuri yake na mapungufu yake,Hilo lipo wazi kabisa.

Kwa maoni yangu alifanya mengi mazuri Kwa inchi hii ambayo hata mwananchi wa kawaida aliweza kuyaona,aliwatetea wanachi wake na kujitahidi kupunguza changamoto zao Kwa kiasi Fulani.

Inchi ilipofikia kipindi kile ilimhitaji mtu kama yeye kuyaweka mambo Sawa,maana Uhuru ulizidi Sana,ilifikia kipindi eti watu wanaenda kufanya mikutano ulaya Kwa ishu zinazo husu mambo ya hapa Tanzania,ukiuliza eti Tanzania haina sehemu za kufanyia vikao? Ebu angalia inchi ilipokuwa imefikia,nadhani wote mnakumbuka Ile ishu ya kupakwa rangi ndege za ATCL, ilikuwa ikatumike zaidi ya SHS mil 200 eti kupaka rangi ndege,mwisho wa siku watanzania walipaka Kwa mil 5 ingawa jembe akawaongezea ikafika 10,sasa ebu angalia Hali jinsi ilivyokuwa mbaya.

Kuna watu walikuwa wanalipwa mshahara mpaka milioni 40,wengine hela za maendeleo zilikuwa zinawekwa benki wapate riba huku miradi ikicheleweshwa Kwa manufaa Yao,kwahiyo hayo ni machache Tu, ilihitajika kuwa na kiongozi wa Kariba Ile ili walau kuyaweka mambo Sawa, sisemi aliweza kufanikiwa Kwa asilimia zote lkn alifanya alichoweza.

Itakuwa si Busara kumlaumu jiwe Kwa kila kitu,na kuona mabaya yake Tu,hapana tuwe wa kweli wa nafsi zetu Kwa kumpongeza Kwa mazur aliyofanya pia. Itoshe kusema kuwa alifanya kile alichoweza kufanya,na tukiacha unafiki pembeni wengi wetu tunaukubali mchango wake.

Natambua kuwa vile vile pia kama kiongozi yoyote hakosi mapungufu ya kiutawala,hata mwalimu Nyerere binafsi alikiri kuna mambo alikosea kama kiongozi wa Taifa,na jiwe naye hawezi kuepukana nayo.

Kuendelea kumsema marehemu haitabadilisha chochote,ni busara ya kibinadamu kujadili wakati uliopo kwani huu TUNAWEZA kuubadilisha,Ila wakati uliopita ushapita hakuna cha kufanya,wakulungwa walisema yaliyopita sindwele Bali tugange yajayo.
Hakuna mtu anayebishana na wewe, alikua ni kiongozi wa kawaida kabisa na aliyoyafanya mengi ni mabaya kuliko hayo machache unayoyasema.

Hakupandisha mishahara ya wafanyakazi na madaraja stahiki kwa miaka sita; kwa kuwa yeye alikua ameshiba hela za walipa kodi alijinasibu kabisa hawezi kupandisha maslahi ya wafanya kazi, bali atajenga madaraja na miundombinu;

Alivunja ndoa nyingi kwa kuamisha watumishi Dodoama bila ya kujali mustkabali wa wenza wao;

Katika kipindi chake kulikua na kesi nyingi ziki walenga wanasiasa na wengi aliwaweka ndani na kuwadhalilisha utu wao;

Aliwafukuza kazi watu bila kujali haki zao za msingi za kisheria za kusikilizwa;

Anatuhumiwa kwa kuuza nyumba za serikali nchi nzima, na nyingine kuwahonga ndugu zake na wanawake wake;

Anatuhumiwa kwa kujenga barabara na madaraja chini ya kiwango wakati akiwa waziri wa ujenzi na hata akiwa raisi miradi mingi haikufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma kama vile ununuzi wa ndege kama mashati;

Anatuhumiwa kupoteza Trillion 1.5 pesa ambazo hazijulikani zilipo;

Mkuu mambo ya huyo mtu ni mengi, itoshe kusema Mungu amrehemu.
 
Wasalaam wana JF

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita nchi yetu ilishuhudia utawala usiofuata sheria na kutojali haki na heshima za binadamu. Watanzania wengi walikua wamekatwa mikia na kugugumia. Haki za kisiasa na kiraia ziliporwa na watu waliumizwa kimwili na kiuchumi na wengine kupoteza maisha.

Mustakabali mzima wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ulikua chini ya maamuzi ya mtu mmoja. Yeye ndiye aliyekua muamuzi wa wapi maendeleo yaende au la, nani ale au afe njaa, nani ateuliwe au atumbuliwe. Mkusanyiko wa ujinga mwingi kama huu ulitotokana na udhaifu wa katiba yetu lakini pia na mapungufu ya afya ya akili ya kiongozi wetu.

Kama wenzangu walivyosema, mwenye enzi Mungu alituamulia ugomvi huu, je kuna haja ya kuendelea kutetea ujinga huo mwingi uliopita? Tumuombe Mungu atuvushe na atupe mapito na mwisho mwema. Asanteni

Ashukuriwe Mungu kwa kutuondolea yule binadamu movu
 
Dah, ilikuwa hatari
 
Ila ujue Tz inatakiwa mtu mwenye maono hata kama ni ku- dictate ili watu waamke. Watu wamezoea madili tu, akitokea mtu wa kukemea hayo madili watu wanachukia. Mwanzoni ilionekana Tanzanite inatoka nchi jirani, ila mwenye maono akakataa, na kufanya yake. Hebu sasa kila mtu awajibike na kuwa mzalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga na waliokosa Elimu bora ni wengi sana huwezi kuwalaumu kuhusu hilo Mkuu hata hivyo naona wapo vizuri sana...
 
Wasalaam wana JF

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita nchi yetu ilishuhudia utawala usiofuata sheria na kutojali haki na heshima za binadamu. Watanzania wengi walikua wamekatwa mikia na kugugumia. Haki za kisiasa na kiraia ziliporwa na watu waliumizwa kimwili na kiuchumi na wengine kupoteza maisha.

Mustakabali mzima wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ulikua chini ya maamuzi ya mtu mmoja. Yeye ndiye aliyekua muamuzi wa wapi maendeleo yaende au la, nani ale au afe njaa, nani ateuliwe au atumbuliwe. Mkusanyiko wa ujinga mwingi kama huu ulitotokana na udhaifu wa katiba yetu lakini pia na mapungufu ya afya ya akili ya kiongozi wetu.

Kama wenzangu walivyosema, mwenye enzi Mungu alituamulia ugomvi huu, je kuna haja ya kuendelea kutetea ujinga huo mwingi uliopita? Tumuombe Mungu atuvushe na atupe mapito na mwisho mwema. Asanteni

...Mbona hukutoa Suluhisho? Tufanye Nini ili Tujikomboe??
 
Mjinga na MPUMBAVU ni wewe unayepigwa kodi kila unapogeuka huku wenzio wakilamba ASALI! Hakuna utawala wa hovyo kama huu uliopo sasa! Magufuli pamoja na madhaifu yake hauwezi kumfananisha na takataka nyingine yoyote!
Nenda kazikwe pamoja nae. Mjomba kifo chake hakina tofauti na paka
 
Heading na Content ni vitu viwili tofauti...

Nikajua kwenye content humu ndo ungeelezea Tanzania ndo nchi pekee mtu hupata umaarufu na maisha humnyookea kwa kufanya ujingaujinga tu mitandaoni na anapata na wadhamini wanampa na gari na ubalozi wa makampuni huku watu timamu wenye vigezo wakibaki wanapuyanga na wakati hao ndo wanahitajika kwa mustakabali wa taifa. Anyways! Kila mtu na uwezo wake wa kufikiri na utambuzi wa mambo.

Nawasilisha mkuu!
 
Mama mwenyewe ameomba siasa ziwe za kistaarabu.
Atokee mtu awe anamdhihaki continously unafikiri ataachwa atambe tu?! Awe anamchamba mwanzo mwisho mitandaoni na field.
 
Heading na Content ni vitu viwili tofauti...

Nikajua kwenye content humu ndo ungeelezea Tanzania ndo nchi pekee mtu hupata umaarufu na maisha humnyookea kwa kufanya ujingaujinga tu mitandaoni na anapata na wadhamini wanampa na gari na ubalozi wa makampuni huku watu timamu wenye vigezo wakibaki wanapuyanga na wakati hao ndo wanahitajika kwa mustakabali wa taifa. Anyways! Kila mtu na uwezo wake wa kufikiri na utambuzi wa mambo.

Nawasilisha mkuu!
Anzisha uzi wako
 
Wasalaam wana JF

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita nchi yetu ilishuhudia utawala usiofuata sheria na kutojali haki na heshima za binadamu. Watanzania wengi walikua wamekatwa mikia na kugugumia. Haki za kisiasa na kiraia ziliporwa na watu waliumizwa kimwili na kiuchumi na wengine kupoteza maisha.

Mustakabali mzima wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ulikua chini ya maamuzi ya mtu mmoja. Yeye ndiye aliyekua muamuzi wa wapi maendeleo yaende au la, nani ale au afe njaa, nani ateuliwe au atumbuliwe. Mkusanyiko wa ujinga mwingi kama huu ulitotokana na udhaifu wa katiba yetu lakini pia na mapungufu ya afya ya akili ya kiongozi wetu.

Kama wenzangu walivyosema, mwenye enzi Mungu alituamulia ugomvi huu, je kuna haja ya kuendelea kutetea ujinga huo mwingi uliopita? Tumuombe Mungu atuvushe na atupe mapito na mwisho mwema. Asanteni

umepatia
 
Kitendo cha kujua hujui kitu ni busara na una akili. Ila anaejua anajua kumbe hajui hana busara. Je umeshindwa kuelewa maendeleo yaliyoletwa kwa mda mfupi na mwamba JPM?
 
Back
Top Bottom