Kwa mtazamo wangu jiwe kama mwanadamu mwingine yoyote Yule ana mazuri yake na mapungufu yake,Hilo lipo wazi kabisa.
Kwa maoni yangu alifanya mengi mazuri Kwa inchi hii ambayo hata mwananchi wa kawaida aliweza kuyaona,aliwatetea wanachi wake na kujitahidi kupunguza changamoto zao Kwa kiasi Fulani.
Inchi ilipofikia kipindi kile ilimhitaji mtu kama yeye kuyaweka mambo Sawa,maana Uhuru ulizidi Sana,ilifikia kipindi eti watu wanaenda kufanya mikutano ulaya Kwa ishu zinazo husu mambo ya hapa Tanzania,ukiuliza eti Tanzania haina sehemu za kufanyia vikao? Ebu angalia inchi ilipokuwa imefikia,nadhani wote mnakumbuka Ile ishu ya kupakwa rangi ndege za ATCL, ilikuwa ikatumike zaidi ya SHS mil 200 eti kupaka rangi ndege,mwisho wa siku watanzania walipaka Kwa mil 5 ingawa jembe akawaongezea ikafika 10,sasa ebu angalia Hali jinsi ilivyokuwa mbaya.
Kuna watu walikuwa wanalipwa mshahara mpaka milioni 40,wengine hela za maendeleo zilikuwa zinawekwa benki wapate riba huku miradi ikicheleweshwa Kwa manufaa Yao,kwahiyo hayo ni machache Tu, ilihitajika kuwa na kiongozi wa Kariba Ile ili walau kuyaweka mambo Sawa, sisemi aliweza kufanikiwa Kwa asilimia zote lkn alifanya alichoweza.
Itakuwa si Busara kumlaumu jiwe Kwa kila kitu,na kuona mabaya yake Tu,hapana tuwe wa kweli wa nafsi zetu Kwa kumpongeza Kwa mazur aliyofanya pia. Itoshe kusema kuwa alifanya kile alichoweza kufanya,na tukiacha unafiki pembeni wengi wetu tunaukubali mchango wake.
Natambua kuwa vile vile pia kama kiongozi yoyote hakosi mapungufu ya kiutawala,hata mwalimu Nyerere binafsi alikiri kuna mambo alikosea kama kiongozi wa Taifa,na jiwe naye hawezi kuepukana nayo.
Kuendelea kumsema marehemu haitabadilisha chochote,ni busara ya kibinadamu kujadili wakati uliopo kwani huu TUNAWEZA kuubadilisha,Ila wakati uliopita ushapita hakuna cha kufanya,wakulungwa walisema yaliyopita sindwele Bali tugange yajayo.