Katika kipindi cha Mwaka mmoja na miezi michache nchi yetu inashuhudia utawala unaolinda Viongozi mafisadi, wafanyabiashara wakubwa na watumishi chawa na kutojali haki na heshima za raia wa hali ya chini kama kiini na chachu ya maendeleo kupitia makusanyo ya kodi na tozo za kinyonyaji.
Watanzania wote wasio viongozi,wafanyabiashara wakubwa watumishi wenye nyadhifa za juu serikalini wamekatwa mkia na kuwa hawana tofauti na wakimbizi nchini.
Mustakabali wote wa mipango, maendeleo na matumizi ya nchi yako kwa kikundi cha watu wachache "Oligarchs" ambao ni wanasiasa wa CCM na wafanyabiashara wakubwa tokana na fedha wanazokwapua toka kwa raia kupitia kodi na tozo za kinyonyaji pamoja na kuuza rasilimali za taifa.
Tunatumaini ipo siku yatakwisha haya ila hatuna hakika tutakuwa katika hali gani hio siku ambayo haya yatafikia tamati. Tumerudi nyuma kihatua kwa 99% toka ambako tulikuwa tunaelekea kimaendeleo na utunzaji wa rasilimali za taifa.
Zile zama za shamba la bibi zimerejea kwa kasi kubwa na sasa yote yanafanyika bila vazi la uwoga wala aibu mbele ya raia. Maisha yanapanda kwa kasi ya ajabu, tozo lukuki, kila kitu bei juu. Miradi haiendelezwi, ni udokozi unafanyika bila soni watu wanalambishana asali huku wananchi hawaelewi hatma yao ya kesho.
Mamlaka zimejipanga kunyonya raia kwa kisingizio kuwa ni kuleta maendeleo ambayo ni kiini macho. Maendeleo hayo hayo ambayo yanakopewa hela kwa matrillion ndio hayo hayo yanayokusanyiwa tozo. Msimamizi yupo ila hatuoni hatua za kiuongozi anazochukua.
Sina budi kusema tuliingia choo cha kike kwenda kinyume na ukuu wa Mungu kwa kujifanya tuna akili sana. Mama kazi yake halisi ni kuzaa, kulea na kusimamia nyumba sio majukumu mazito ambayo tumemtwisha. Kwa upande wa mafisadi na ma chawa kwao awamu hii ni bora kuliko iliopita ila raia wa hali ya chini ni msiba usio na wafariji.
Tusijizime data, hio kazi na uchawa unaoringa nao baada ya miaka 5-10 watoto wako hawatafaidika nao kwa lolote lile. System inazidi kuoza kwa comfort ya muda mfupi.