Ni Tanzania pekee ambapo ujinga unatetewa na kundi kubwa la watu

Hakuna mtu anayebishana na wewe, alikua ni kiongozi wa kawaida kabisa na aliyoyafanya mengi ni mabaya kuliko hayo machache unayoyasema.

Hakupandisha mishahara ya wafanyakazi na madaraja stahiki kwa miaka sita; kwa kuwa yeye alikua ameshiba hela za walipa kodi alijinasibu kabisa hawezi kupandisha maslahi ya wafanya kazi, bali atajenga madaraja na miundombinu;

Alivunja ndoa nyingi kwa kuamisha watumishi Dodoama bila ya kujali mustkabali wa wenza wao;

Katika kipindi chake kulikua na kesi nyingi ziki walenga wanasiasa na wengi aliwaweka ndani na kuwadhalilisha utu wao;

Aliwafukuza kazi watu bila kujali haki zao za msingi za kisheria za kusikilizwa;

Anatuhumiwa kwa kuuza nyumba za serikali nchi nzima, na nyingine kuwahonga ndugu zake na wanawake wake;

Anatuhumiwa kwa kujenga barabara na madaraja chini ya kiwango wakati akiwa waziri wa ujenzi na hata akiwa raisi miradi mingi haikufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma kama vile ununuzi wa ndege kama mashati;

Anatuhumiwa kupoteza Trillion 1.5 pesa ambazo hazijulikani zilipo;

Mkuu mambo ya huyo mtu ni mengi, itoshe kusema Mungu amrehemu.
 
Ashukuriwe Mungu kwa kutuondolea yule binadamu movu
 
Dah, ilikuwa hatari
 
Ila ujue Tz inatakiwa mtu mwenye maono hata kama ni ku- dictate ili watu waamke. Watu wamezoea madili tu, akitokea mtu wa kukemea hayo madili watu wanachukia. Mwanzoni ilionekana Tanzanite inatoka nchi jirani, ila mwenye maono akakataa, na kufanya yake. Hebu sasa kila mtu awajibike na kuwa mzalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga na waliokosa Elimu bora ni wengi sana huwezi kuwalaumu kuhusu hilo Mkuu hata hivyo naona wapo vizuri sana...
 
...Mbona hukutoa Suluhisho? Tufanye Nini ili Tujikomboe??
 
Mjinga na MPUMBAVU ni wewe unayepigwa kodi kila unapogeuka huku wenzio wakilamba ASALI! Hakuna utawala wa hovyo kama huu uliopo sasa! Magufuli pamoja na madhaifu yake hauwezi kumfananisha na takataka nyingine yoyote!
Nenda kazikwe pamoja nae. Mjomba kifo chake hakina tofauti na paka
 
Heading na Content ni vitu viwili tofauti...

Nikajua kwenye content humu ndo ungeelezea Tanzania ndo nchi pekee mtu hupata umaarufu na maisha humnyookea kwa kufanya ujingaujinga tu mitandaoni na anapata na wadhamini wanampa na gari na ubalozi wa makampuni huku watu timamu wenye vigezo wakibaki wanapuyanga na wakati hao ndo wanahitajika kwa mustakabali wa taifa. Anyways! Kila mtu na uwezo wake wa kufikiri na utambuzi wa mambo.

Nawasilisha mkuu!
 
Mama mwenyewe ameomba siasa ziwe za kistaarabu.
Atokee mtu awe anamdhihaki continously unafikiri ataachwa atambe tu?! Awe anamchamba mwanzo mwisho mitandaoni na field.
 
Anzisha uzi wako
 
umepatia
 
Kitendo cha kujua hujui kitu ni busara na una akili. Ila anaejua anajua kumbe hajui hana busara. Je umeshindwa kuelewa maendeleo yaliyoletwa kwa mda mfupi na mwamba JPM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…