"Ni Tanzania tu utasikia biashara inakufa kwa sababu ina wateja wengi" Yerico Nyerere

Miye kilaza flani, sina elimu yeyote, ila nahisi hujasoma na kuelewa nilichokiandika. Narudia tena, miradi sampuli ya mwendokasi ni kwa ajili ya huduma na si kutengeneza faida…!
Okay bro.
 
"Black people are not complete human beings because THEY DON'T HAVE A GOOD BRAIN to govern the society as White people. They are still under the process of becoming the complete human beings."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Usije ukawa una digrii yako ya Tumaini University ukadhani unajua, umetembea humu duniani ukajifunza wengine wanafayaje na kwasababu gani?
Duh. Okay bro.
Mimi nimesoma wakati Tanzania Kuna UDSM na Sokoine tu.
Asalaam aleykhum.
 
Naomba serikali isishiriki katika kutoa huduma moja kwa moja badala yake iwapatie sekta binafsi ndio iendeshe, serikali i deal na kumsimamia huyo sekta binafsi.
 
Tumewakosea sana nyani na tumbili,hata wao kwenye jamii yao hawana uongozi wa hovyo kama tulionao sisi binadamu.
Aibu yetu hii tupambane nayo bila kushirikisha viumbe wengine ambao bora wao manyani ndio wangekuwa baadhi ya viongozi wetu ili tuwe na sababu ya kusema.
 

Kuna mahala Serikali inakosea
Serikali inafikiri madegree ndiyo yanafanya kazi/ Biashara na ndio sababu wanajaza wezi kwenye mashirika.
Huwezi kuweka mtu mwenye degree au madegree umpe kazi ya kukata ticket, sijui kupanga mafaili, sijui apost petty cash, sijui aangalie watu wanao ingia kwenye mwendo kasi, au sijui awe mtendaji wa kijiji au sijui afundishe kiswahili darasa la tatu nk nk halafu umlipe shs laki tano halafu utegemee ufanisi au asiwe mwizi huku anaona kabisa watu wa Elimu yake wana pata mara tatu na zaidi ya mshahara wake; Kimsingi hizo ni nafasi za watu wa Cheti na diploma

Private sector wanalijua hilo na ndio sababu kila ngazi ina kiwango chake cha elimu na hata ungeomba ukiwa na pHD huwezi kupata kazi ya mtu wa Diploma kwani wanaona kabisa hutaweza kuwa na ufanisi ukilipwa mshahara wa mtu wa diploma; sana sana ataishia kujisifia kuwa unamadegree bila ufanisi na kuiba au dili mbaya kwani kipato hakiendani na elimu yake......
 
wanayoyafanya kenya yalitakiwa kufanyika kwetu, sisi tumekuwa brain washed kabisa, inawezekana kweli ule mwenge ni zindiko la viongozi linalosaidia kuwapumbaza wananchi wasiielewe kinachoendelea na hata wakielewa wasifanye chochote (zombinization), hii nchi ina uongozi kutoka kuzimu kabisa, very dumb, very selfish, hamna anayefikiria future ya nchi, wote wanafikiria kubaki relevant kisiasa tu ili wazidi kupuga pesa na ku secure future za watoto wao basi, ila hakuna mwenye dedication kwa kizaz kijacho cha hili taifa.
nawaheshimu wale viongozi wa zamani the likes of kina chief mkwawa, ambao walikua watetezi wa kweli wa mali zetu, himaya zetu na future ya watu wao, walikufa wakitupigania... ila hz tumbili zilizopata madaraka kimdebwedo bure, bure, bure kabisa.
ingekua kubadilisha uongozi ni simple kama kubadilisha line, tungeshawatupa kwenye dustbin mapema sana hawa watu.
 
Sikubaliani na wewe kwenye matumizi ya maneno makali, lakini kuhusu mwenge, ninakuunga mkono kwa asilimia mia moja. Mwenge ni uchawi wa Serikali wenye lengo la kuwapumbaza wananchi ili watawalike kirahisi. Kuna nyuzi kadhaa humu jukwaani zinazoelezea ukweli wa mbio za mwenge. Ni ushikina kamili!
 
Mkuu sasa tangu lini Ufisadi,Rushwa,Ubadhilifu wa mali ya umma,utakatishaji wa fedha,wizi,nk viliisha lini katika nchi yetu?
Ripoti ya CAG ikishasomwa inawekwa kabatini! Hakuna kinachoendelea!
Ukisikia ya nchi hii unaweza wakati wote kujifungia chumbani unalia weeee mpaka basi!
Ukija mifuko ya jamii (PSSSF/NSSF) ni kilio,ukija NHIF ni kilio,ukija kwenye taasis ni kilio,kila mahali ni kilio!
Wengi wanatoa jasho lakini wanaokula kutokana na jasho lao ni Wachache!
Manyani ni sisi wananchi ambao tunatawaliwa!
Raia namba moja amekata tamaa anasema Wale kwa urefu wa kamba zao!
Mungu atusaidie!
 
Jibu ni jepesi tu kwamba Watanzania ni wezi na mafisadi sana hasa wale wanaojiita wasomi na wenye madaraka kuanzia serikalini hadi kwenye sekta binafsi.
 
Mali ya umma,wanaosimamia kuziongoza hawana huruma nazo

Ova
 
Itakua staff wa Dart wewe tena wale wanao tuibia chenchi zetu pale dirishani kimara mwisho
 
Kwa nini eti umewatukana hao wanyama mwitu kiasi hicho?

Wafanyie heshima basi kwa sababu sioni kibaya anachofanya nyani na hao wanyama wengine, ikilinganishwa na matendo ya kushangaza na kuhuzunisha afanyayo kiumbe mwanadamu.
Hakika usemacho, nyani ni bora kwa matendo yake kuliko watu wa hapa..tuwape heshima zao wanyama .
Nchi yenye rasilimali nyingi ,watu wake hupata udumavu wa maono .
 
Kaka umesomea wapi?
Umenitisha kwa kusema mwendokasi haitakiwi kupata faida na ku reinvest hiyo profit ili wapanue huduma mpaka Gingo la mboto, na Bunju na Chalinze ikiwezekana wakafungue hii huduma Tabora, TANGA na Moshi.

Sijaelewa concept yake. Mimi ninachofahamu hiyo ilikuwa ni economic modal ndani ya ideology ya kisocialism (soma kitabu cha social stratification and differentiation cha cecil Rhodes (1923) utapata ufahamu mkubwa, ameanza kwa kutoa original copies za classic theories e.g Reninism, Maxist na modern theories kabla ya kupambanua consequences ya hizo idelogies to the economy na social wellfare).Sema tu humu wanajamii forum tumeacha kupambanua haya mambo muhimu kwa kina na kiundanani zaidi kwa kutumia concept za elimu za juu kufafanua kwa lugha rahisi, sio kama miaka 10 iliyopita, tumebaki kushabikia machawa)

Ebu turudi kwanye mada sasa. Baada ya sisi kuingiza free market economy automatically tumetoka kwenye socialism modal na kuingia kwenye capitalist economic modals ambaz0 market ina-determine the price in a free uncontrolled environment. Hizo subsidies zilikuwa za enzi hizo za ujamaa na ndio maana mashirika mengi ya umma yaliishia kwenye kifo cha mende. Ebu angalia shirika zuri la umma mfano NHC-mbona wao hawajawahi kupata hasara , wanajiendesha kwa faida kwa bei fair kwa customers wao na wanapanua bussiness zao kila kukicha. hicho ndicho tunachoongelea hapa.

Ukisoma vizuri andiko limejikita kwenye unparallel advantages haya mashirika ya umma, mwendokasi na bima za afya , air Tanzania, mabenki yenye hisa kubwa za serikali; kwani wafanyakazi wote wa serikali wanatakiwa kufungua account huko NMB; kwa hiyo suala la wateja si issue kwao ni kuchukua mahela tu, kuchukua mafaida tu, compared to private business. Kwa hizo advantages hasa kubwa zaidi kutengewa wateja mpaka wanashindwa kuwamudu, uwezo wa kudetermine price na aina ya services regardless what customers wants, ndio maama tunasema haiwezekani kamwe chini ya jua wapate hasara.

Ebu angalia scernario hii iliyonitokea mimi recently (kisa mkasa). Jana nilibook flight ya tarehe 23/06/2024 one way flight air Tanzania from to DSM to Mza, then Dodoma, ,kwani ndiyo almost airline pekee iliyobaki ,serikali imemonopolize na kuua airline zote ili ishike hatamu. Ghalama ilikuja 850,000/= almost a million, na nafasi zilikuwa zimejaa. Kesho unaambiwa wanajiendesha kwa hasara.Pathetic. Maana yake to na fro itakuwa almost 1.4 to 1.5 Millions, sasa hapa tutapata maendeleo kweli. Kumbuka kwa wenzetu effective management ya airline na flight ni moja ya nguzo muhimu ya maendeleo (economic trigger)

Hawa walikuwa wanatakiwa wapate faida ,waboreshe na kupanua bussiness, washushe price na kuifanya services zao ziwe accessible kwa wananchi wa Kawaida. Tatizo tunaingiza siasa kwenye biashara na kuingiza upigaji mkubwa sana na wa kutisha.na hakuna anayejali kwani wakuu wetu kila mtu amejitengea sehemu ya kupiga na wanajuana, Ndio maana ni ngumu sana kunyoosheana vidole,
 
Nchi hii ingekua ni msichana hakuna ambaye angetamani kumuoa maana inapigwa kila mahali na pande zote.
 
Hakika umenena vizuri, Manyani ni sisi na sio hao wanyama
 
Kamanda husiangalie hoja kwa jicho moja au kwa upande mmoja.

Mashirika ya umma in a modern economy lazima yatengeneze faida na kuexpand bussiness..Kinachotakiwa kwa sababu ya unparallel favour na advantages wanazopewa during the course of running their bussiness, wanatakiwa price yao iwe affordable na fair kwa majority of citizen na ndiyo maana ya kupewa favour kubwa hizo.

Ila suala la kutengeneza faida halikwepeki. Nafikiri ni mwezi ulipita ulimuona mkuu wa nchi akikabidhiwa gawio la serikali toka mashirika ya umma na kipindi cha mwendazake the same, halafu concept yako inasema serikali ndiyo itoe divident huoni hapo kuna kitu kinamiss.Tunaongelea modern economy ambayo model yake kwetu haijulikani kama ni ni socialism au capitalism ila inaendeshwa kicapitalism ingawa hawajatamka. Ila kwa azimio la Zanzibari automatically waliua ideologies zote za kisocialism toka kwenye azimio la Arusha, the late Mwl Nyerere alifafanua vizuri kabisa hii controversy au naweza kuhiita inconsistency ideologies.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…