Kuna funzo hapa.
Wanandoa tarajali kusainiana Mikataba ya Kusajili Mali zao (Pre-nuptial Contract) ni muhimu sana katika maisha ya Sasa.
Pre-nuptial Contract will help to avoid the problem of the Marriage Conemanship in case of divorce like this.
Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba kiuhalisia Wanaume wenyewe huwa wanakuwa chanzo cha matatizo yote haya ya wao kutapeliwa au kudhulumiwa mali zao kwenye masuala haya ya talaka.
Kwa kawaida mgawanyo wa mali kwenye talaka huwa unagusa mali zile tu ambazo ni 'Chumo la Ndoa,'(Matrimonial Property). Kama Mwanandoa wa kike naye alichangia kwenye suala la upatikanaji wa mali husika, sioni tatizo lolote lile na yeye akipewa Haki yake katika mchakato mzima wa mgawanyo wa mali wakati wa talaka.