Ni ujinga kununua simu ya zaidi ya milioni kama haina cha ziada katika shughuli zako unless you are rich , simu nyingi ≤ milioni 1 zinajotosheleza.

Ni ujinga kununua simu ya zaidi ya milioni kama haina cha ziada katika shughuli zako unless you are rich , simu nyingi ≤ milioni 1 zinajotosheleza.

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Na hii ipo zaidi kwa bongo, simu mpya nyingi zinatoka kwa kuongezewa features ambazo wabongo hawazitumii kabisa au nchi haina miundo mbinu yake. mashahidi ni nyie hata humu jamii forums jukwaa la tech lina wadau wachache,

Matumizi ya simu ni kupiga simu, kuchati, kusikiliza muziki, kurushiana connection, kujiweka filter, n.k. THATS IT !! Nje ya hapo maybe ile mikwara mbuzi ya kutumia kitambi kusafisha screen.

On average unaweza kupata simu medium kwa bajeti ya laki 3 - 5 lakini tunaelewa kuna watu wanataka simu zenye majina ya kampuni kubwa, ziwe na 5G, system za kisasa, camera nzuri, n.k. katika hali kama hii ukiwa na bajeti ya laki 6 hadi milioni 1 unapata mashine ya viwango.

Unanunua simu ya bei mbaya kioo kikipasuka uambiwe milioni 1 jasho linaanza kukutoka, umefosi hapo.

Navyoona hizi simu za milioni 1 na laki kadhaa, milioni 2, milioni 3, n.k. maybe ni kwa celebrities wanaojiongeza kwenye kujibrand, wakuu wa taasisi nyeti wanao mingle international levels, matajiri, n.k.

WATANZANIA WENGI HAWAPIGI HATUA KWASABABU YA TAMAA YA KUISHI MAISHA YANAYOWAZIDI WANAPOPATA VIJISENTI BADALA YA KUWEKEZA & KUSAVE.
 
Upo sahihi sana

Na kuna wengine hawana hela wanafosi wawe na simu za gharama.. wanaenda nunua simu used sijui refurbrished za dubai kwa kina matelephone china plaza.

Simu zinachemka mpaka wanaziweka kwenye friji na freezer.

Simu inakuwa inashinda ndani ya friji kama matunda ama mboga
 
Na hii ipo zaidi kwa bongo, simu mpya nyingi zinatoka kwa kuongezewa features ambazo wabongo hawazitumii kabisa au nchi haina miundo mbinu yake. mashahidi ni nyie hata humu jamii forums jukwaa la tech lina wadau wachache.

mtu anatumia simu kupiga, kuchati, kusikiliza muziki na mitandao ya kijamii

kuna haja gani ya kununua simu za gharama kubwa kama haikusaidii kwenye shughuli zako na wewe sio tajiri ?
Computer yangu ya kwanza ilikuwa na RAM ya 1GB, ilikuwa clone Moja matata,.... Sasa unaweza kuelewa nikiwa na android ya 6GB RAM moyo wangu unavyo furahi... simu yangu haijawahi kuzidi 300k na sijawahi kuweka screen protector!
 
Uzi hauna afya

Ukifika page ya 3 huko wanaume wenye iphone wataanza kuchambwa

Ila siku hizi si kuna ile ku-'top up' mtu yeyote anapata simu kali tu
Yani hebu waza mi nimenunua simu kwa milioni zangu kadhaa naitumia kuchat ama pics tu wewe unateseka na kipi hasa au kinakuwasha kitu gani? Unanijua?
Nakula kwenu?
Unanidai?
Nimekuibia?

Jibu hapana sasa kelele za nini?
 
Back
Top Bottom