Ni ujinga kununua simu ya zaidi ya milioni kama haina cha ziada katika shughuli zako unless you are rich , simu nyingi ≤ milioni 1 zinajotosheleza.

Ni ujinga kununua simu ya zaidi ya milioni kama haina cha ziada katika shughuli zako unless you are rich , simu nyingi ≤ milioni 1 zinajotosheleza.

Ebu tupe elimu basi ni simu,je hata za laki 3?,na twambie kwa kututajia ni features gani waweza nufaika nazo kwenye simu?mbali na kupeuzi mitandaoni,kupiga,ku sms,na vingine ni vipi?
 
Kumpangia mtu maisha kama vile anatumia pesa zako ni utoto na ushamba, mtu hata akiamua kununua simu ya milioni 2 na analala kwenye godoro na mkeka ni maisha yake wewe hayakuhusu, usione mawazo yako wewe ni bora kuliko ya wengine kila mmoja na maisha yake
 
Hiyo ni kweli lakini fanya ufanyavyo hakikisha hautumii Infinix, Tecno, Redmi, oppo na simu zingine zenye majina ya ajabu ajabu.
Hayo nimetalia maanani, kwa watu wanaotaka simu zenye majina makubwa bado wanaweza kupata mashine kali kwa ≤ milioni
 
Kumpangia mtu maisha kama vile anatumia pesa zako ni utoto na ushamba, mtu hata akiamua kununua simu ya milioni 2 na analala kwenye godoro na mkeka ni maisha yake wewe hayakuhusu, usione mawazo yako wewe ni bora kuliko ya wengine kila mmoja na maisha yake
Hajawapangia maisha ila ameongelea kua huo ni uzwazwa
 
me nishafanya utafiti bado kupublish tu. matumizi ya sim za gharama ni moja ya vitu vinafanya vijana wa hali ya chini wasipige hatua.

upande wangu nina smart tangu 2020 hadi leo ipo, no topup, no chochote kile na huduma zote napata.
nunua simu ya bei kubwa kama una matumizi nayo muhim.
 
Na hii ipo zaidi kwa bongo, simu mpya nyingi zinatoka kwa kuongezewa features ambazo wabongo hawazitumii kabisa au nchi haina miundo mbinu yake. mashahidi ni nyie hata humu jamii forums jukwaa la tech lina wadau wachache,

Matumizi ya simu ni kupiga simu, kuchati, kusikiliza muziki, kurushiana connection, kujiweka filter, n.k. THATS IT !! Nje ya hapo maybe ile mikwara mbuzi ya kutumia kitambi kusafisha screen.

On average unaweza kupata simu itayokidhi matumizi yako kwa bajeti ya laki 3 - 5 lakini tunaelewa kuna watu wanataka simu zenye majina makubwa, zisiwe outdated sana, camera nzuri, n.k. katika hali hio bajeti ya laki 6 hadi milioni 1 unaweza kupata mashine ya viwango.

Unanunua simu ya bei mbaya kioo kikipasuka uambiwe milioni 1 jasho linaanza kukutoka, umefosi.

Navyoona hizi simu za milioni 1 na laki kadhaa, milioni 2, milioni 3, n.k. maybe ni kwa celebrities wanaojiongeza kwenye kujibrand, wakuu wa taasisi nyeti wanao mingle international levels, matajiri, n.k.

WATANZANIA WENGI HAWAPIGI HATUA KWASABABU YA TAMAA YA KUISHI MAISHA YANAYOWAZIDI WANAPOPATA VIJISENTI BADALA YA KUWEKEZA & KUSAVE.
Kama mhusika hajadhulumu wala kuiba, utampangiaje namna ya kutumia fedha yake mwanangu? Heri anayenunua simu kuliko ngono akaishia ukimwi
 
Back
Top Bottom