Ni ujinga kununua simu ya zaidi ya milioni kama haina cha ziada katika shughuli zako unless you are rich , simu nyingi ≀ milioni 1 zinajotosheleza.

Ebu tupe elimu basi ni simu,je hata za laki 3?,na twambie kwa kututajia ni features gani waweza nufaika nazo kwenye simu?mbali na kupeuzi mitandaoni,kupiga,ku sms,na vingine ni vipi?
 
Kumpangia mtu maisha kama vile anatumia pesa zako ni utoto na ushamba, mtu hata akiamua kununua simu ya milioni 2 na analala kwenye godoro na mkeka ni maisha yake wewe hayakuhusu, usione mawazo yako wewe ni bora kuliko ya wengine kila mmoja na maisha yake
 
Hata kama haumudu, kuna mtu atamudu kwa ajili yako.

πŸ˜…
Ndio ndioπŸ˜…πŸ˜…nimekupata kwa uzuri kabisa simu ya gharama ni nzuri asikudanganye mtu, mi nilipoteza hii nilihaha vibaya muno, naulizwa unataka ipi ya 2025, halafu nijishaue kisa kuna mjf mmoja kasema ni ujinga bla bla bla blaaaaa😁😁😁
 
Hiyo ni kweli lakini fanya ufanyavyo hakikisha hautumii Infinix, Tecno, Redmi, oppo na simu zingine zenye majina ya ajabu ajabu.
Hayo nimetalia maanani, kwa watu wanaotaka simu zenye majina makubwa bado wanaweza kupata mashine kali kwa ≀ milioni
 
Mweeeeeh yaani milioni ninunue simuπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈ

Tecno tu ze wolidi. Haka kasimu kangu nilinunua laki, ila kuna muda hadi naiota, ndio iwe milioniπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈ
 
Wachana na uongo muone πŸ˜…
 
Hajawapangia maisha ila ameongelea kua huo ni uzwazwa
 
me nishafanya utafiti bado kupublish tu. matumizi ya sim za gharama ni moja ya vitu vinafanya vijana wa hali ya chini wasipige hatua.

upande wangu nina smart tangu 2020 hadi leo ipo, no topup, no chochote kile na huduma zote napata.
nunua simu ya bei kubwa kama una matumizi nayo muhim.
 
Kama mhusika hajadhulumu wala kuiba, utampangiaje namna ya kutumia fedha yake mwanangu? Heri anayenunua simu kuliko ngono akaishia ukimwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…