Ni ujinga wa karne kukataa kiwanda cha kuchuja mafuta kujengwa Tanga-missed oppurtunities

Mkatapa wa DP WORLD unawafunga mikono. Hawaruhusiwi kuendeleza bandari yoyote. Si Tanga tu, hata Mtwara.
 
Oyah nitokezee huo uhuni basi 😂
Mbona upo mitandaoni ,alikuwa analalamika sana hujuma viongozi wa serikalini walikuwa wanamfanyia hadi akataka kukifunga wakenya wakamuomba aende kufungua kwao.
 
Huyo Dangote ni mwekezaji sawa na wawekezaji wengi. Hapo hapo Tanga refinery itajengwa.

Huwezi kujenga bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka hapo Tanga halafu kiwanda ukakijenga Mombasa. Ni kichekesho kuamini hilo linawezekana.

Wapiga kelele wengi wanaandika makala ndefu kuhusiana na kitu wasichokifahamu vyema,

Wajenzi wa refinery wapo wengi duniani ambao tunaweza kufanya nao biashara sio lazima awe Dangote peke yake.

Tanzania katika hii biashara kafanana na binti mzuri kigoli anayewapeleka puta wanaume wenye pesa zao, hana cha kupoteza kwake biashara ni nzuri sana na anakwenda kwa utulivu na akili nyingi.
 
Mkatapa wa DP WORLD unawafunga mikono. Hawaruhusiwi kuendeleza bandari yoyote. Si Tanga tu, hata Mtwara.
Hujui ulichokiandika. Hakuna ukweli wa kufungwa na mkataba wa DP World, hizo bandari za Bagamoyo na Tanga zinatafutiwa mwekezaji mwenye uwezo, Akipatikana atakuja kuziendesha.
 
Mmekataa nyinyi au mwenye hela zake ndiye kaamua awekeze anakohitaji mwenyewe?

NB:Bei ya mafuta haiwezi kushuka hata kijengwe Tanga sababu atajaziwa makodi na tozo kibao
Hiyo refinery itajengwa Tanga ni suala la muda tu. Dangote labda hana uelewa wa biashara hii.

Haiwezekani bomba lijengwe Tanzania halafu refinery ijengwe Kenya, inawezekana ni njia ya kuivuta mezani serikali ya Tanzania kwa maana ya mbinu za kibiashara.

Lakini refinery inaweza kujengwa na makampuni mengi tu haswa yale ya Ulaya hivyo serikali haina haraka wala pupa kwenye ujenzi wa hiyo refinery.
 
Nakuelewa vizuri mkuu, na najua nimesimplify the whole story ili kila mtu aweze kuwa pamoja na mada yenyewe.
Nipe kiswahili cha refinery-sidhani kama mtu wa kawaida aatkuelewa.
Crude oil refinery ni kama kiwanda cha TIPER , kilichojengwa na Mwalimu na kuuzwa na Mzee Mwinyi.
Hii ni teknologia kwa sasa haipo nchini zaidi ya miaka 40, na watu kuwaeleza kirahisi refinery kuwa sawa na kuchuja , basi ingalau mko pamoja.
 
Well said!
 
Jua liwake mvua inyeshe lazima refinery itajengwa Tanga, LAZIMA.

Hizi siasa za Dangote kutaka ijengwe Kenya wakati bomba lipo Tanzania pengine ni wasiwasi alionao mfanyabiashara huyo kwamba anaweza kukosa biashara mazima hivyo kaona aongee kwa nia ya kuwaweka pamoja Kenya na Tanzania.

Refinery itajengwa Tanga pengine kampuni itakayofanya hivyo inaweza kuwa ya Wazungu kutoka Ulaya.

Hii biashara serikali yetu inaiendea kwa akili kubwa pasipo kukurupuka.
 
Ukiwa na akili ya kichawa hata usiku basi utasema ni mchana kweupe na huku unaingia shimoni.
Hatusikitiki kukosa tu fursa ya kiwanda cha kuchuja magfuta toka Uganda, tunasikitika kwa vile ambavyo tuwa watu wanavaa masuti makubwa makubwa na magari meusi yenye ving'ora vingi na mataa taa ya kuchngaya humo mabarabarani, lakini kichwani hamna kitu!

Fursa ya Dangote kama uniona kama wawekezaji wengine basi wewe ni mmoja wao niliowaelezea hapo huu, hamna akili sana.
Danote anawekeza kwa ushirikiano wa south south
Dangote hatakuwa na masharti kama ya Wprld Bank na IMF
Dangote tayari amesha wekeza nchi kiwanda cha simenti
Dango na watu wengine watatua au wanne wa aina hiyo itattuondoa katika utegemezi wa wazungu

Sasa tuje kwetu jinsi hao mlio na masuti makubwa makubwa mnavyofanya
Mwekezaji anaombwa rushwa za kurahisisha kuwekeza
Muwekezaji anaombwa asilimia(shares) za kampuni atakayoianzisha nchini
Muwekezaji anaombwa nafasi kubwa kubwa za kazi kwa watoto wa vogogo

Haya yote yanafanyika na sisi wananchi tunayajua, kwa vile wawekezaji wenyewe wanasema hali ilivyo.

Hivyo bradha usitetee udhaifu wako.
 
Umejielekeza kule nilikokudadavua,
Kwenu uwekezaji si kwa ajili yaTaifa, mwataka kula na wazungu!
 
Tuwe makini na huyu chura aka kizimkazi!! Kisa jamaa kagoma kutoa rushwa kwa familia za wanamtandao. Na pia ni hofu kwa wanamtandao kuhusu kushuka kwa bei za mafuta kwa sako la ndani. Kumbuka wako na nguvu kuliko chura.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Dangote ni mfanyabiashara mwenye kutazama maslahi yake, lakini aheshimu pia taratibu za mataifa anayokwenda kufanyia biashara.

Huwezi kujenga refinery Kenya wakati bomba linatoka Uganda na kupitia Tanzania!. Ukitaka ijengwe refinery Kenya maana yake lijengwe bomba jingine kutokea Uganda mpaka Mombasa, nani anatoa pesa hizo nyingi za ujenzi ambao tayari umeshafanyika Tanzania?. Mzee Museveni anaweza kusubiri miaka mingine mitano wakati keshasema anaelekea kuondoka madarakani?.

Anachokifanya Dangote kinaweza kufanywa na wawekezaji wengine wenye teknolojia na mtaji wa kujenga refinery, wapo wengi tu hivi sasa serikali inafanya nao maongezi ili lolote likitokea wapewe tenda ya ujenzi wa hiyo refinery.
 
Sio kweli, tunaijali Tanzania kuliko hao wazungu.

Kujenga refinery sio suala dogo inahitajika mtaji na elimu kubwa.
Mbona unajikanyaga kama vile una hallucinate!
Tunasoma michango yote humu, kwa watu walioenda shule tunaelewa.
Mtaji ulikuwepo-Dangote
Elimu-ipo na haiwezi potea kuna vijana wengi sana wa |Process Engineering hawana kazi.
Unachoongea sasa tofauti na ulichokiandika awali.

Uchawa usio na maana unaliangamiza Taifa.
 
Tatizo lako ni Dangote au siyo?
Akija mzungu kukupa rushwa unafurahi gego hadi gego!!!
 
Tatizo lenu humu jukwaani ni kutopenda kupingwa katika kile mnachoamin ikwamba ni sahihi, hamchelewi kuja na majina mengi na dhihaka isiyo na sababu.

Narudia tena kukwambia kwamba Refinery itajengwa hapo Tanga.

Huyo Dangote hajui mengi kuhusiana na namna biashara nzima ya usafirishaji wa mafuta inavyoendeshwa. Huwezi kujenga chujio la mafuta mahali ambapo hakuna bomba lenye kuyasafirisha kuyatoa yanapotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…