Muwe mnatuliza mioyo na akili zenu. Hapo Askofu hana kitu chochote cha kitibu. Aliye lofa kuitwa lofa siyo tusi, bali ameelezwa ukweli jinsi alivyo.
Hiyo aliyeandika hiyo barua kwenda Vatican, kwa kweli siyo lofa tu, bali ni mnafiki na msaliti wa imani, maana neno la Mungu linamraka kuwa mkweli, mpenda haki, mteteaji wa wanaonewa; sasa yeye kumshtaki Fr Kitima ambaye daima amesimama imara katika kuyaishi maagizo hayo ya Mungu, basi yeye si mkristo tena. Lakini pia kutojua utaratibu wa kanisa wa kuwakilisha malalamiko yoyote, huyo ni lofa na mjinga wa hairakia ya utawala wa Kanisa.
Mleta mada, katika ulofa huo, na wewe umo kwa sababu huelewi chochote ya imani ya kweli ya kikatoliki inayomtaka kila muumini kuwa mkweli wa nafsi, hiwezi kumwambia Askofu aombe msamaha kwa sababu amekuwa mkweli. WEWE NAWE, HAKIKA LOFA MWENZAKE WA HUYO ALIYEAMBIWA NI LOFA.