Ni vema Askofu Ruwai'chi akatubu kwa kumuita lofa mtu aliyemshitaki Padri Kitima kwa Papa

Ukisikia kelele kwa jiwe la gizani,mpiga kelele kaguswa nalo.Pole Kimbesal a.k.a lofa mwimba amani na mwoga wa kuiimba haki na mdau wa Amani ya mafisadi wa taifa hili.
Mkuu , Mimi siyo rofa
 
Makosa ya Kitima.

1.Kusema serikali ikiri watu watu walipigwa risasi za moto.

2.Majeruhi waliletwa katika hospital za kanisa chini ya amri ya polisi wakiamu wasitibiwe bali waachwe wafe au watupwe mochwari angali hai.

3. Waliomshambulia wanafahamika na ndio maana polisi wako kimya [May -December] kwa jeshi linalojinasibu lina intelijensia kali haliwezi kushindwa kuwakamata hao washambuliaji .

4.Serikali inafahamu fika sababu za watu kuandamana na sio kwamba haijui , isijifiche katika kivuli cha vijana wa nchi jirani au vijana waliolipwa ilhali vijana hawana ajira na wanatekwa wanapodai haki zao.

5.Watu wanataka haki , haki ya kuchagua watu wawapendao imepokwa na ndio maana hata mapendekezo yao kupeleka serikali iangalie namna ya kufanya uchaguzi usiwe na machafuko waliikamilisha April mwishoni na May akashambuliwa, ni mtu asiye timamu tu ndio ataamini October 29 kulikua na uchaguzi maana jina la tume ni huru ila muundo wa tume sio huru hata kwa asilimia 1%

6.Serikali iwape ndugu, jamaa na marafiki maiti za ndugu zao , wakikaa kimya haitosaidia bali itazidi kupanda chuki kama unafahamu fika ndugu yako ameuliwa na hata mwili hupewi unazika unafikiri huyo mtu atajenga picha gani kwa waliomfanyia ndugu , jamaa , rafiki yao?

Nimepitia video ile ya aliyoongea Kitima hayo ndio makosa yake makuu hadi kushtakiwa .

Nimemkumbuka sana mwalimu wangu mmoja wa shule ya msingi alipokuwa anatufundisha kusoma "KATIKATI " ya mistari au kusoma kwa ufahamu .

Leo nimeamini sio wote wanaweza kusoma kwa ufahamu na kuelewa baadhi ya vitu vinavyohitaji bongo safi zinazochemka.

Kama kaulimbiu yenu ya Kazi na Utu mliimanisha na vitu alivyoongea Kitima mmeona sio sawa basi itabidi kuanzia ile kamati kuu wawe declared "MENTAL INCAPACITATED STATE"

View: https://www.youtube.com/live/oUTsR9GjXR8?si=ijDeThphHWB8Jx-p

Subiri barua kwa Papa irudi kama mtu hajawa kama Dr slaa
 
Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)
wewe ndo utubu kwa kuwa na kichwa kizito kushindwa kumwelewa askofu
 
Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)

What the meaning of Lofa?
Isikute Lofa ni Advective
 
Tumuache papa aamua
Nakuuliza swali tarehe 29 Kitima alikua barabarani na mitaani kupiga watu risasi?

Hawa wahuni waliokuwa wanapiga watu risasi mmewashtaki wapi??
20251104_030225.jpg
 
Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)
Thread zaidi ya 3 . Unaishambulia catholic huogopi
 
Makosa ya Kitima.

1.Kusema serikali ikiri watu watu walipigwa risasi za moto.

2.Majeruhi waliletwa katika hospital za kanisa chini ya amri ya polisi wakiamu wasitibiwe bali waachwe wafe au watupwe mochwari angali hai.

3. Waliomshambulia wanafahamika na ndio maana polisi wako kimya [May -December] kwa jeshi linalojinasibu lina intelijensia kali haliwezi kushindwa kuwakamata hao washambuliaji .

4.Serikali inafahamu fika sababu za watu kuandamana na sio kwamba haijui , isijifiche katika kivuli cha vijana wa nchi jirani au vijana waliolipwa ilhali vijana hawana ajira na wanatekwa wanapodai haki zao.

5.Watu wanataka haki , haki ya kuchagua watu wawapendao imepokwa na ndio maana hata mapendekezo yao kupeleka serikali iangalie namna ya kufanya uchaguzi usiwe na machafuko waliikamilisha April mwishoni na May akashambuliwa, ni mtu asiye timamu tu ndio ataamini October 29 kulikua na uchaguzi maana jina la tume ni huru ila muundo wa tume sio huru hata kwa asilimia 1%

6.Serikali iwape ndugu, jamaa na marafiki maiti za ndugu zao , wakikaa kimya haitosaidia bali itazidi kupanda chuki kama unafahamu fika ndugu yako ameuliwa na hata mwili hupewi unazika unafikiri huyo mtu atajenga picha gani kwa waliomfanyia ndugu , jamaa , rafiki yao?

Nimepitia video ile ya aliyoongea Kitima hayo ndio makosa yake makuu hadi kushtakiwa .

Nimemkumbuka sana mwalimu wangu mmoja wa shule ya msingi alipokuwa anatufundisha kusoma "KATIKATI " ya mistari au kusoma kwa ufahamu .

Leo nimeamini sio wote wanaweza kusoma kwa ufahamu na kuelewa baadhi ya vitu vinavyohitaji bongo safi zinazochemka.

Kama kaulimbiu yenu ya Kazi na Utu mliimanisha na vitu alivyoongea Kitima mmeona sio sawa basi itabidi kuanzia ile kamati kuu wawe declared "MENTAL INCAPACITATED STATE"

View: https://www.youtube.com/live/oUTsR9GjXR8?si=ijDeThphHWB8Jx-p

Ujinga aliousema Father Kitima ni kuita yale maandamano, hayakuwa maandamano ulikuwa uasi ulioandaliwa kwa miezi kadhaa.

Awe mwangalifu pia kwani usalama wa Taifa wanapokaa kimya haina maana hawajui michezo ambayo CHADEMA waliicheza kuelekea October 29. Chama ambacho yeye Father ni mdau mkubwa akiwa anatoka sehemu moja na Lissu.

Pia kwake kuamua kuongea na waandishi wa habari siku moja kabla Rais hajaongea tena suala lile lile ni dharau kwa mkuu wa nchi, ndio maana siku ile anaongea na wazee Rais alimshambulia Kitima japo hakumtaja jina, anayakwaza mamlaka yake na ameanza hiyo hulka tangu suala la DP World liliposhindwa baada ya watu kuelewa kuhusiana na upotoshaji alioufanya kwa kusambaza barua makanisani kupinga uwekezaji.

Angevua joho akaingia mtaani hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo Dr Slaa alifanya hivyo na hakuna ambaye alimshangaa.
 
Ujinga aliousema Father Kitima ni kuita yale maandamano, hayakuwa maandamano ulikuwa uasi ulioandaliwa kwa miezi kadhaa.
Hao waasi walitokea wapi na walitaka kuasi kitu gani?
Awe mwangalifu pia kwani usalama wa Taifa wanapokaa kimya haina maana hawajui michezo ambayo CHADEMA waliicheza kuelekea October 29. Chama ambacho yeye Father ni mdau mkubwa akiwa anatoka sehemu moja na Lissu.
Kila mtu ni usalama wa taifa awapo nchini kwake hao usalama wa taifa unaowaongelea wewe ni wapi?

Kitima akiona hatari akakemea maana yake katumia jukumu lake kama mwananchi kulinda usalama wa taifa.
Pia kwake kuamua kuongea na waandishi wa habari siku moja kabla Rais hajaongea tena suala lile lile ni dharau kwa mkuu wa nchi
Rais yupi unayemuongelea hapa?

Maana Tanzania kwa sasa hakuna rais nchi iko chini ya jeshi.
, ndio maana siku ile anaongea na wazee Rais alimshambulia Kitima japo hakumtaja jina, anayakwaza mamlaka yake na ameanza hiyo hulka tangu suala la DP World liliposhindwa baada ya watu kuelewa kuhusiana na upotoshaji alioufanya kwa kusambaza barua makanisani kupinga uwekezaji.
Kitima kushambuliwa kwa maneno ndio mwisho wa kuongea?

Mbona alishambuliwa tangu May kwa silaha kabisa na lengo lilikua kumuua je mlishamkamata aliyemshambulia?
Angevua joho akaingia mtaani hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo Dr Slaa alifanya hivyo na hakuna ambaye alimshangaa.
Mimi habari za joho hapa hazinihusu na simuongelei Kitima katika nyanja ya cheo chake kama kasisi bali ni kama mtu mwingine awaye yoyote ambae ni sober atasimama kusema MAUAJI, UFISADI , WIZI WA KURA, UTEKAJI hakubaliani navyo.
 
Hao walirudisha heshima mtaani, wale vibaka wakaanza kuingia chini ya uvungu wa vitanda vyao.
Heshima ipi unayozungumzia ?

Siku hizi kuua watu ni heshima???

Watu kupigwa risasi wakiwa majumbani wamepumzika ni heshima

Kwahiyo Sheikh Sharif Majini na Master Tindwa walikua vibaka?

Maana hao wawili ni miongoni mwa watu wengi waliouwawa wakiwa majumbani mwao.
 
Hao waasi walitokea wapi na walitaka kuasi kitu gani?

Kila mtu ni usalama wa taifa awapo nchini kwake hao usalama wa taifa unaowaongelea wewe ni wapi?

Kitima akiona hatari akakemea maana yake katumia jukumu lake kama mwananchi kulinda usalama wa taifa.

Rais yupi unayemuongelea hapa?

Maana Tanzania kwa sasa hakuna rais nchi iko chini ya jeshi.

Kitima kushambuliwa kwa maneno ndio mwisho wa kuongea?

Mbona alishambuliwa tangu May kwa silaha kabisa na lengo lilikua kumuua je mlishamkamata aliyemshambulia?

Mimi habari za joho hapa hazinihusu na simuongelei Kitima katika nyanja ya cheo chake kama kasisi bali ni kama mtu mwingine awaye yoyote ambae ni sober atasimama kusema MAUAJI, UFISADI , WIZI WA KURA, UTEKAJI hakubaliani navyo.
Jiulize kwanini wale vijana waliokamatwa walipewa kesi ya uhaini ndio utajua maana ya uasi ni nini.

TISS ndio usalama wa taifa kila mtu hawezi kufanya shughuli wanayoifanya.

Kitima anatukwaza baadhi ya wakatoliki bila yeye kujua madhara ya hulka zake kwa taasisi kubwa ya kanisa katoliki.

Rais Samia anayekuongoza kwa haki baada ya kula kiapo halali, barua ya ubalozi wa USA imemtambua kwa kumuandika President Samia wewe chawa wa CHADEMA ni nani nchi hii mpaka uupinge uwepo wake?.

Mbona wewe na mimi tunaongea bila ya kutekwa?. Jiulize hao wanaotekwa wana kosa gani mpaka wakutane na adha hiyo.
 
Jiulize kwanini wale vijana waliokamatwa walipewa kesi ya uhaini ndio utajua maana ya uasi ni nini.
November 3- Wale ni vijana kutoka nch8 jirani

November 12 - Wale vijana walifuata mkumbo.

December 2- Wale vijana walilipwa kuandamana.

Hizo ni kauli za mtu mmoja jitafakari.
TISS ndio usalama wa taifa kila mtu hawezi kufanya shughuli wanayoifanya.
Hao TISS ni watu kutoka Nampula Mozambique au ni Watanzania??

Umeshindwa kusoma katikati ya mistari kujua kila mtu ni usalama wa taifa ??
Kitima anatukwaza baadhi ya wakatoliki bila yeye kujua madhara ya hulka zake kwa taasisi kubwa ya kanisa katoliki.
Anakukwaza wewe na nani?

Kwa mfano aliposema kauli hii "Polisi walileta watu wakiwa na majeraha wakawakata wataalam wetu wa afya kuwahudumia na kuwaacha wafe au wakatupwe ili wafie mochwari "

Wewe hiyo kauli hapo ilikukera?

Angepigwa risasi mdogo wako ungesikia alikua na chance ya kupona ila akazuiliwa matibabu ili afe ndio ungefurahi na sio kukereka?
Rais Samia anayekuongoza kwa haki baada ya kula kiapo halali, barua ya ubalozi wa USA imemuita Rais Samia yeye chawa wa CHADEMA ni nani nchi hii mpaka uupinge uwepo wake?.
Rais Samia haniongozi mimi hata kwa sekunde moja , na sio rais wangu hilo huwezi kunilazimisha.

Kwahiyo ubalozi wakimuita ni rais ndio lazima na mimi awe rais kwangu ?
Mbona wewe na mimi tunaongea bila ya kutekwa?
Kwahiyo kwakua wewe hujaumwa na au hujaenda kufanya vipimo hospitali angali ni mzima ina maana hospitali hazina umuhimu?

Kwahiyo wewe kwakua hujaugua unafikiri ndio hospitali hazipo???

Hospitali zina wagonjwa kila leo licha ya kuwa wewe labda hujakanyaga hospitali miezi 6 iliyopita ila bado zipo na zinahudumia watu.

Kutekwa kupo na hatuwezi kusema kutekwa hakupo sababu mimi na wewe hatujatekwa hiyo ni MYOPIC THINKING.
. Jiulize hao wanaotekwa wana kosa gani mpaka wakutane na adha hiyo.
Kuteka kupo kisheria?..

Tuanzie hapo kwanza, sheria gani inasema mtu mwenye kosa atekwe.?

Kwenye sheria kuna ARREST [kukamata] je ABDUCTION [kuteka] ipo kisheria?

Kama haipo kisheria basi tuzungumzie ARREST ambayo iko kisheria na inasema mtu akikamtwa ashifikishwe mahakamani katika saa 24, kupewa wakili na hata kuambiwa kosa analoshtakiwa na kujulisha watu wa karibu , na kupewa dhamana.

Heche alikamatwa mahakamani , imechukua siku 3 [saa 72 ] kujulikana tu alipo hizo haki zote za mkamatwaji alinyimwa sasa nani anavunja sheria.

Fortunatus Buyobe alikamatwa tarehe 6 , December , ila imekuja kujulikana anaposhikiliwa ni kituo cha polisi Chang'ombe na hii kujulikana haikua taarifa ya polisi bali watu wema walioamua kuvujisha siri hii , naye haki zake zote hizo kama mtu aliyekamatwa hazikufuata je nani kavunja sheria?

Umeuliza swali la kipuuzi sasa kwamba wanaotekwa wana kosa gani , hivi tangu lini mtu mwenye kosa anastahili kutekwa au kuuwawa , je kazi ya mahakama ni nini?
 
Back
Top Bottom