Ni vema Askofu Ruwai'chi akatubu kwa kumuita lofa mtu aliyemshitaki Padri Kitima kwa Papa

Ni vema Askofu Ruwai'chi akatubu kwa kumuita lofa mtu aliyemshitaki Padri Kitima kwa Papa

Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)
Huyu Askofu Ruwaichi ni mfuja mali za kanisa mkubwa sisi Mwanza tulihakikisha anaondoka alikuwa anafuja mali za Hospitali ya Bugando. Hivyo ana tabia ya kujikweza sana wakati anafuja mali za waumini ambao leo anawadharau na kuwaita malofa.
 
Huyu Askofu Ruwaichi ni mfuja mali za kanisa mkubwa sisi Mwanza tulihakikisha anaondoka alikuwa anafuja mali za Hospitali ya Bugando. Hivyo ana tqbia ya kujikweza sana wakati anafuja mali za wauminj ambao leo anawadharau.
Duh aisee hatari sana
 
Ya kawaida kwako kwa sababu wewe ni mhuni kama huyo Askofu Ruwaichi
Wahuni ni Samia na nyinyi genge lake! Wasema ukweli ni wapenzi wa Mungu ila nyinyi mafisadi na vibaraka wenu ndio wahuni.
 
November 3- Wale ni vijana kutoka nch8 jirani

November 12 - Wale vijana walifuata mkumbo.

December 2- Wale vijana walilipwa kuandamana.

Hizo ni kauli za mtu mmoja jitafakari.

Hao TISS ni watu kutoka Nampula Mozambique au ni Watanzania??

Umeshindwa kusoma katikati ya mistari kujua kila mtu ni usalama wa taifa ??

Anakukwaza wewe na nani?

Kwa mfano aliposema kauli hii "Polisi walileta watu wakiwa na majeraha wakawakata wataalam wetu wa afya kuwahudumia na kuwaacha wafe au wakatupwe ili wafie mochwari "

Wewe hiyo kauli hapo ilikukera?

Angepigwa risasi mdogo wako ungesikia alikua na chance ya kupona ila akazuiliwa matibabu ili afe ndio ungefurahi na sio kukereka?

Rais Samia haniongozi mimi hata kwa sekunde moja , na sio rais wangu hilo huwezi kunilazimisha.

Kwahiyo ubalozi wakimuita ni rais ndio lazima na mimi awe rais kwangu ?

Kwahiyo kwakua wewe hujaumwa na au hujaenda kufanya vipimo hospitali angali ni mzima ina maana hospitali hazina umuhimu?

Kwahiyo wewe kwakua hujaugua unafikiri ndio hospitali hazipo???

Hospitali zina wagonjwa kila leo licha ya kuwa wewe labda hujakanyaga hospitali miezi 6 iliyopita ila bado zipo na zinahudumia watu.

Kutekwa kupo na hatuwezi kusema kutekwa hakupo sababu mimi na wewe hatujatekwa hiyo ni MYOPIC THINKING.

Kuteka kupo kisheria?..

Tuanzie hapo kwanza, sheria gani inasema mtu mwenye kosa atekwe.?

Kwenye sheria kuna ARREST [kukamata] je ABDUCTION [kuteka] ipo kisheria?

Kama haipo kisheria basi tuzungumzie ARREST ambayo iko kisheria na inasema mtu akikamtwa ashifikishwe mahakamani katika saa 24, kupewa wakili na hata kuambiwa kosa analoshtakiwa na kujulisha watu wa karibu , na kupewa dhamana.

Heche alikamatwa mahakamani , imechukua siku 3 [saa 72 ] kujulikana tu alipo hizo haki zote za mkamatwaji alinyimwa sasa nani anavunja sheria.

Fortunatus Buyobe alikamatwa tarehe 6 , December , ila imekuja kujulikana anaposhikiliwa ni kituo cha polisi Chang'ombe na hii kujulikana haikua taarifa ya polisi bali watu wema walioamua kuvujisha siri hii , naye haki zake zote hizo kama mtu aliyekamatwa hazikufuata je nani kavunja sheria?

Umeuliza swali la kipuuzi sasa kwamba wanaotekwa wana kosa gani , hivi tangu lini mtu mwenye kosa anastahili kutekwa au kuuwawa , je kazi ya mahakama ni nini?
Unapotekwa unakuwa umefanya makosa, labda ya uchochezi. Wakati mwingine inakuwa ni sababu za kibiashara au ugomvi wa kimapenzi, kumbuka Chadema ilikuwa na tabia ya kuteka wanasiasa wa chama hicho hicho kimoja, unaweza kuisingizia serikali kwamba inahusika na utekaji kwenye mazingira ya aina hiyo?.

Tume ipo kazini muda huu itakuja na majibu kamili kuhusiana na chanzo haswa cha maandamano kilikuwa ni nini.

Huna uwezo wa kufanya shughuli ya TISS ingawa sikufahamu, tabia ni zile zile za kibongo kudhani anafahamu kila kitu kwa sababu anao uwezo wa kutoa maoni yake kupitia simu yake ya Iphone.

Mimi muumini wa kanisa katoliki, analoliongoza na kuingiza siasa za kivyama bila ya kujua wengine hatuamini kile anachokiamini.

Mdogo wangu asingeweza kutoka nje katika mazingira ya tarehe 29 October mkuu wa polisi aliposema mwisho kutembea ni saa 12 maana yake zaidi ya hapo ukikutwa huko barabarani unapigwa risasi, mazingira ya kivita yalikwisha kuingia nchini.

Samia ni rais wa JMT tena halali baada ya kushinda uchaguzi ambao nyinyi mliamua kuususia mkadhani kwamba mpo peke yenu mlisahau kwamba kulikuwa na vyama 16 vilivyoweka wagombea hakuna muda wa kubembeleza wale wapuuzi wa 'no reform' nchi inakwenda bila ya uwepo wao.

Kutekwa kupo dunia nzima mkuu, nenda katazame ICE wanavyowakamata raia ambao hawana uhalali wa kuishi Marekani halafu njoo ulinganishe na namna watu wanavyotekwa hapa Tanzania.

Wewe uwe mtii wa sheria ukijifanya kondoo kichwa ngumu utakutana na vichwa ngumu wengi tu watakushughulikia kwa mujibu wa sheria hizo hizo unazohoji juu ya uwepo wake.
 
Unapotekwa unakuwa umefanya makosa, labda ya uchochezi. Wakati mwingine inakuwa ni sababu za kibiashara au ugomvi wa kimapenzi,
Sheria gani inaruhusu kuteka [Abduction] sababu ya hayo makosa.
kumbuka Chadema ilikuwa na tabia ya kuteka wanasiasa wa chama hicho hicho kimoja, unaweza kuisingizia serikali kwamba inahusika na utekaji kwenye mazingira ya aina hiyo?.
Mwanasiasa yupi alitekwa na CHADEMA hebu mtaje hapa .

Polepole nae ni mwanasiasa alitekwa na CHADEMA?
Tume ipo kazini muda huu itakuja na majibu kamili kuhusiana na chanzo haswa cha maandamano kilikuwa ni nini.
Tume???

Tume ya kitu gani na inachunguza chanzo cha maandamano kutokea wapi?
Huna uwezo wa kufanya shughuli ya TISS ingawa sikufahamu, tabia ni zile zile za kibongo kudhani anafahamu kila kitu kwa sababu anao uwezo wa kutoa maoni yake kupitia simu yake ya Iphone.
Unajuaje sina uwezo , hao TISS ni viumbe kutoka sayari ya Mars??

Hizo tabia za "kibongo" ni zipi??
Mimi muumini wa kanisa katoliki, analoliongoza na kuingiza siasa za kivyama bila ya kujua wengine hatuamini kile anachokiamini.
Sijakuuliza wewe ni muumini wa wapi, na imani yako haina msaada hapa.

Mimi namuongelea Kitima kama mtanzania anayekemea utekaji na mauaji simuongelei katika uwanja wa ukasisi.

Kitima kama victim wa matukio hayo anayo haki ya kuyapazia sauti, alinusurika kuuwawa mwezi May na hadi leo waliomfanyia hayo matukio hawajafikishwa katika vyombo vyovyote vya kisheria.
Mdogo wangu asingeweza kutoka nje katika mazingira ya tarehe 29 October mkuu wa polisi aliposema mwisho kutembea ni saa 12 maana yake zaidi ya hapo ukikutwa huko barabarani unapigwa risasi, mazingira ya kivita yalikwisha kuingia nchini.
Neno mdogo wako limetumika kama mfano , tu unaweza kuwa na ndugu yoyote au rafiki aliyeshambuliwa katika maandamano kama hukupatwa na janga hilo haimanishi hakuna waliouwawa katika maandamano.

Wewe una uhakika waliopigwa risasi wote ni waliotoka majumbani kwao zaidi ya saa 12?

Sheikh Sharif Majini na Master Tindwa walipigwa risasi majumbani kwao hili hukusikia au umeamua kufanya cherry picking?
Samia ni rais wa JMT tena halali baada ya kushinda uchaguzi ambao nyinyi mliamua kuususia mkadhani kwamba mpo peke yenu mlisahau kwamba kulikuwa na vyama 16 vilivyoweka wagombea hakuna muda wa kubembeleza wale wapuuzi wa 'no reform' nchi inakwenda bila ya uwepo wao.
Kwangu simtambui kama rais sababu hakuchaguliwa, halafu ukisemea "nyinyi mlisusia" sijui unalenga kitu gani ?

Vyama 16 ?? Hivyo vyama au washirika wa CCM?
,
Kutekwa kupo dunia nzima mkuu, nenda katazame ICE wanavyowakamata raia ambao hawana uhalali wa kuishi Marekani halafu njoo ulinganishe na namna watu wanavyotekwa hapa Tanzania.
Sihitaji kutazama video za ICE , nimekuuliza hapa nijibu ni wapi sheria za kitanzania zinasema kuteka mtu aliye na makosa.

Kwahiyo dunia nzima wanateka watu wanaosema Angela Kizigha ni fisadi, dunia nzima wanateka wanaosema Abdul ni mwizi.

Kwahiyo dunia nzima mwenyekiti wa chama kinachogombea ana mamlaka ya kuteua tume inayoenda kusimamia uchaguzi anaoshiriki ilhali kuna uwepo wa mgongano wa kimaslahi?

Kwahiyo dunia nzima matokeo ya urais yamezuiliwa kuhojiwa mahakamani?

Kwahiyo kama wewe jirani yako ameamua kutokula ilhali chakula kipo na wewe ni lazima usile sababu yeye hajala?

Wewe uwe mtii wa sheria ukijifanya kondoo kichwa ngumu utakutana na vichwa ngumu wengi tu watakushughulikia kwa mujibu wa sheria hizo hizo unazohoji juu ya uwepo wake.
Sheria zipi unazozungumzia sizitii?

Na umetumia mawanda yapi kujua mimi sifuati sheria??

Nimekupa mifano miwili ya Heche na Buyo be waliokamtwa na polisi je polisi ndio waliovunja sheria au hao wahusika.

Wameshikiliwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa mahakamani wala kuambiwa nini wamekamatiwa.

Hawakupewa nafasi ya kupata wakili wala watu wao wa karibu kujulishwa wanashikiliwa wapi.

Hawakupewa dhamana kwa mujibu wa sheria.
 
Lugha ya wahuni ambayo maana yake nini? Ni matusi?!
Lofa ni slang ya Kiswahili maana Yake mtu asiye na msimamo. Au asiyechukulia mambo Kwa uzito...je hakuna neno rasmi ? Au atakuwa naye anapiga kijiti kabla ya kusalisha
 
Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)
Wewe lofa hujui maana ya neno lofa. Nani amekuambia neno lofa ni tusi?
 
Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)
Ulofa hauna dini ulofa ni sawa upumbavu unaokemewa vikali kwenye maandiko matakatifu
 
Katika Hali isiyo ya kawaida Askofu amemuita lofa mtu aliyeandika barua kwenda Italy kwa lengo la kumshitaki Kitima.
Askofu Ruachi ameonyesha kukosa uvumilivu wakimungu na kumtukana lofa mtu huyo, Hivyo basi ni vema akatubu hadharani watu waone ili asamehewe.
View attachment 3520782
#Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa TUTUBU (Eze, 18:20)
Hakufuata utaratibu , unajua utaratibu wa kumstaki mtumishi wa kanisa?
 
Back
Top Bottom