Ni vigumu CHADEMA kuleta mabadiliko nchi kwa sababu ya udini

CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.
Kwanza kusema Wana sera nzuri wakati hata wewe hujui sera Yao hata Moja ni utovu wa nidhamu.

ACT ndio Wana sera nzuri hao Chadema wao Wana matusi Mazuri na wanasheria Waziri,sera zao nzuri ni zipi?
 
Yoda niliwahi kukuambia upotofu wako ukanijia juu sasa utakuwa ushaelewa sasa. Kuwaza tu mambo haya ni upotofu mkubwa.
Watanzania tuache unafiki na uoga wa kuzungumzia mambo ya hizi dini mbili zinavyoingiliana na maisha yetu kwa sababu ni uhalisia na zina athari chanya na hasi namna zinavyo shape maisha yetu hasa katika siasa.

Hivi wewe unafikiria imekuwa ni bahati mbaya tu kwamba kwenye Urais wa CCM akitoka Mkristo Mkatoliki anakuja Muislamu wa BAKWATA kwa miaka yote??
 
CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.
Mkuu Bado uko kwenye pingu za dini kwenye hiki kizazi cha kuhoji?! Kama una zaidi ya miaka 35 nitakuelewa ukiwaza kwa mtazamo wa kidini. Ukweli ni kuwa wengi wa walioko chini ya miaka 35 ni nadra kufanya maamuzi kwa hisia za kidini, maana hawaamini kwenye hizo dini, bali AI Technology. Na kwa kukusaidia tu, haitapoteza muda kubalance wafuasi kwa kigezo cha dini, maana dini si kigezo cha kuwa mfuasi wa cdm. Hizo ni siasa za kiccm. Na hakuna muisilamu yoyote kazuiwa kujiunga na cdm.
 
Makamu Mwenyekiti Zanzibar?

Amandla...
Kama yasingekuwa matakwa ya kisheria ya vyama vya siasa CHADEMA wasingekaa kuhangaika na Zanzibar, Haina maslahi yoyote kwao
 
Hata Marekani leo hii dini bado X factor kubwa sana kwenye chaguzi zao za kidemokrasia. Kwa Tanzania dini bado ina nguvu sana kwenye siasa.
Pia mimi sijasema wabalance ila nimeongelea ninachokiona katika jamii
 
Kama yasingekuwa matakwa ya kisheria ya vyama vya siasa CHADEMA wasingekaa kuhangaika na Zanzibar, Haina maslahi yoyote kwao
Kama vile ambavyo CUF ya Maalim ilivyokuwa haina mpango na Bara. Chama chochote makini kina wekeza zaidi pale ambapo wana matumaini ya kukubalika. Ndio maana Chadema haijawahi kuwa na mgombea wa maana wa u Rais Zanzibar.

Amandla...
 
CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.
Na hapo ndio ubora wa CCM unapojionesha wazi. Wao wapo kotekote!
 
CCM haipendwi na raia wa dini zote kwa ujumla kwa wingi, imebakisha watu wachache sana wa dini zote mbili hasa wazee, vijana wasaka vyeo na fursa na ambao familia zao zinanufaika kupitia mfumo wa CCM. Huwezi kusema huo ni ubora.
 
Ccm wanajua nguvu ya dini Tanzania hii ndio maana wapo serious na muungano chadema wanajifanya hamnazo kupuuza hili na kutaka kusimamia sheria bila kujali matabaka ndio maana watakaa miaka buku wasipate madaraka ya nchi hii mtoa mada upo sahihi sana
 
Sijasema kwamba wana chuki na CHADEMA, kutokukikubuli kitu au chama sio sawa na kuwa na chuki nacho, inawezekana ni kutoona faida yake au maslahi yake.
Hawaoni faida kwa sababu CHADEMA haina sera nzuri, au kwa sababu wameaminishwa kupitia propaganda za miaka mingi kuwa CHADEMA haitawajali?
 
Waislamu wachache wanaikubali CHADEMA humu ndani, wengi wanaipinga. Hata Zanzibar na Mikoa ya Lindi, Mtawara, Tanga na mengine yenye Waislamu wengi CHADEMA imekuwa inapata shida kufanya vizuri muda wote.
Nachingwea Lindi CHADEMA inakubakika Sana.
Nadhani imeshawahi kuwa na wawakilishi kwenye ngazi za udiwani na serikali za mitaa na vijiji. Mikoa ya bara ina wafuasi waislam Ila mikoa ya pwani na visiwani ndiyo haina wafuasi wengi waislam. Ukiondoa Dar na Pwani yenyewe.
 
Hawaoni faida kwa sababu CHADEMA haina sera nzuri, au kwa sababu wameaminishwa kupitia propaganda za miaka mingi kuwa CHADEMA haitawajali?
Sera zina nafasi ndogo sana katika demokrasia katika mahali ambapo raia wengi wana elimu ndogo, isiyo bora au wakiwa hawana taarifa nyingi sahihi. Hata Marekani ni vigumu kwa Waislamu na watu we dini nyingine kushinda uchaguzi kwenye red states kwa sababu hizi.
 
CCM haipendwi na raia wa dini zote kwa ujumla kwa wingi, imebakisha watu wachache sana wa dini zote mbili hasa wazee, vijana wasaka vyeo na fursa na ambao familia zao zinanufaika kupitia mfumo wa CCM. Huwezi kusema huo ni ubora.
Ahahahahaha!
 
Back
Top Bottom