Ni vigumu CHADEMA kuleta mabadiliko nchi kwa sababu ya udini

Ni vigumu CHADEMA kuleta mabadiliko nchi kwa sababu ya udini

CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.
Nilistuka kidogo kusoma kichwa cha mada; halafu na kutazama mwanzilishi wa mada ni nani.

Lakini niliposoma yaliyoandikwa ndani ya mada nikaelewa vizuri kinachozungumziwa.

Nadhani ni wakati sasa kuwa wa wazi zaidi kwetu kukubali kwamba tunalo tatizo la udini.

Kila mara jambo hili linapozungumziwa tunakuwa kama tunaogopa kulisemea kwa wazi. Hilo pekee ni tatizo.

Mimi mchango wangu kwenye mada hii ni huu: Kwamba tatizo limekuwepo tokea nyakati za harakati za kutafuta uhuru.
Juhudi kubwa zilifanywa na viongozi wa wakati huo kujaribu kujenga umoja wetu wa kitaifa kwanza, bila ya kutazama imani zetu.
Kwa kiasi kikubwa juhudi hizo zilifanikiwa, lakini hali hiyo ya kujitambua kwa misingi ya kidini pamoja na kufunikwa, halikuondoka moja kwa moja.

Uwepo wa BAKWATA, ni kielelezo tosha cha juhudi zilizofanyika wakati ule; lakini hiyo haikutosha kujenga uTanzania wetu kabla ya dini zetu. Sasa hata BAKWATA yenyewe imejikuta inatumbukizwa kule kule tulikodhani tutaondokana nako.

Sijawahi hata siku moja kusikia CHADEMA wakikataa kuwa na wanachama wa dini yoyote, lakini ninachosikia ni hayo maneno ya CHADEMA ni chama cha kidini, na wanaosema hayo ndio hao hao walioitumbukiza CCM katika majanga haya ya leo..
Na ni hao hao kila mara utasikia wanabaguliwa kwa dini yao.

Hadi hapo tutakapojitambua sote kuwa ni waTanzania kwanza, kabla ya hizo imani zetu, tatizo hili litakuwepo siku zote, na pengine hata kutufikisha mahali pabaya zaidi kama tunavyoona kwenye mataifa kama Nigeria na kwingineko.
 
Waislamu wachache wanaikubali CHADEMA humu ndani, wengi wanaipinga. Hata Zanzibar na Mikoa ya Lindi, Mtawara, Tanga na mengine yenye Waislamu wengi CHADEMA imekuwa inapata shida kufanya vizuri muda wote.
Na inanilazimu niseme; hao CHADEMA wasije wakaingia kwenye upuuzi uliofanywa na CCM.
Yeyote anayetaka kuingia CHADEMA aingie kwa sababu zisizohusiana na dini; na asitegemee kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama au hata serikalini kwa misingi ya dini yake.

Kuna waTanzania wenye dini hiyo ya kiislam wasioendekeza upuuzi huo.
 
Waislamu ni Jamii Duni sana.

1. Wana Torati, Zaburi na Injili ila hawajui hivyo vitabu viko wapi.
(Inassikitisha sana).

2. Wanafuga Majini ambayo ni Malaika walioasi Mbinguni wao waanasema majini ni Mazuri.

3. Majini hayapatani na nguruwe ndio maana Waislamu wakila nguruwe Majini yao yanakimbia kabisa.

4.Jamii nyingi za Waislamu ukanda wa pwani wote hawakuwa na shule hawakuwa na elimu.
Yani wengi ni wajinga sana na wapumbavu.
(Vitabu vya zamani vilijuwa vinaita washenzi).

5. Muislamu yupo tayari aue lakini hayupo tayari kugusa nguruwe.

Lakini yote ya yote CHADEMA kukosa nchi ni ukatili wa CCM na Dola.

SHAME.
 
Chama cha siasa kuwa na viongozi waislamu ngazi ya kitaifa siyo guarantee ya kukubalika na waislamu.

BAKWATA yenyewe inaongozwa na waislamu tupu ila kuna waislamu mamia hawataki hata kuisikia.

Watu hata hawajali kuhusu nani anaongoza chama muhimu ni dhamira yao tu.
 
CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.
Kinachoizuia chadema kuchukua nchi ni dola. Kukiwa na tume huru ya katiba hakuna wa kuizuia chadema wala hizi perceptions haziwezi zuia lolote.
 
CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.
Mkuu,

Nadhani wewe ndio unapenda sana mambo ya udini umekua na tabia za kukosoa waislam pamoja na waislamu wengine wasio na staha kuanza kujibishana kwa kejeli.

Nadhani CHADEMA hata ikishika dola Tutaipokea Pasina udini iwe ni ACT, CHAUMA au CCM hatutaki udini.

VIVA CHADEMA.🔥🔥🔥
 
CHADEMA ni chama chenye sera nzuri sana, maono ya juu na ya mbali ya karne ya 21 na watu wenye akili kubwa sana ila kwa bahati mbaya wamekuwa wa upande mmoja zaidi wa Ukristo. Ni nadra kukuta Waislamu wakijiambatanisha na CHADEMA.

Sijui kwa nini Waislamu wengi hawana mahaba kabisa na CHADEMA pamoja na CHADEMA kutetea mambo ambayo ni ya maslahi kwa raia wote!

Kwa nchi kama hii ya kwetu CHADEMA ina kibarua kigumu sana.

Chama cha Udini na
Ukabila kabisa✍️
 
Mbona humu ndani kuna waislamu wengi wanaikubali Chadema na kuna wakristo wengi wanaipenda CCM?

Waislamu wenye kuipenda CHADEMA
ujue ni kutokea ima Kaskazini au Singida basiiiiiiiii
Lkn Wengi Wakristo
 
Mkuu Bado uko kwenye pingu za dini kwenye hiki kizazi cha kuhoji?! Kama una zaidi ya miaka 35 nitakuelewa ukiwaza kwa mtazamo wa kidini. Ukweli ni kuwa wengi wa walioko chini ya miaka 35 ni nadra kufanya maamuzi kwa hisia za kidini, maana hawaamini kwenye hizo dini, bali AI Technology. Na kwa kukusaidia tu, haitapoteza muda kubalance wafuasi kwa kigezo cha dini, maana dini si kigezo cha kuwa mfuasi wa cdm. Hizo ni siasa za kiccm. Na hakuna muisilamu yoyote kazuiwa kujiunga na cdm.

Wewe kipindi cha CUF Maalim Sefu na CCM kulikuwa na Benjamin William Mkapa wewe ulikuwa upande upi???
 
Wewe kipindi cha CUF Maalim Sefu na CCM kulikuwa na Benjamin William Mpaka wewe ulikuwa upande upi???
Kwamba watanzania wote walitakiwa wawe CUF au ccm enzi hizo? Huu upuuzi wa mitazamo ya kidini ni wa siasa outdated za ccm. Cdm wasije wakalogwa kuiga huu upuuzi. Muisilamu anayetaka kuwa mfuasi wa cdm awe kwa mantiki ya itikadi, cheo ni nafasi ya uongozi ambayo inagombewa. Cha muhimu ni uchaguzi wa haki kama ule wa uenyekiti wa cdm. Sio huo upuuzi wa kubalance hizo dini zenu.
 
Chama cha Udini na
Ukabila kabisa✍️
Hii propaganda ya kipuuzi ya udini na ukabila ilitengenezwa na ccm enzi za Mbowe. Baada ya kuingia Lisu cdm kimekuwa chama halisi cha ukombozi, na sio huo upuuzi wa dini. Waisilamu wenyewe ndio hawa wakina Samia wanaoshinda na hijabu anaiba uchaguzi kitoto hadi kufanya mauaji, na hataki kuwajibika.
 
Chadema wengi kina bwashee na ile Mo29 wengi ndio wameangamia👈
Bisha na ilo???
 
Back
Top Bottom