Mkuu hao hawaehauriki. Kabisa. Unadhani hawaoni hizi nyuzi, wanaona ila wanajiamini wao ndio kila kitu.
- Movie zao ata ule uharisia kidogo tu hazina.
- Kila mlinzi/mfungua geti ni tahira.
- Kila mchekeshaji lazima apige kelele na avae kama kichaa.
- Wanaume kuigiza scene za mwanamke.
- Hao wakina mkojani sijui ata uwa mnawaelewaje.
- Movies hazina ata ile scripts sijui inaitwa. Naona kama msanii anatafuta maneno pale pale kwenye camera.
- Movie moja hafu visa kama mia mbili hivi. Movie inaanza mtu na mke wake wana ugomvi, utakuta katikati jamaa amerogwa kazini, kisha boss wake amefumaniwa na mwanafunzi, then mkuu wa shule wa uyo mwanafunzi ameibiwa baiskeli, then mama wa mwizi wa baiskeli bishara yake ya vitumbua inaenda vizuri, yaani unapotea.
Tukianza warekebisha hao tutaonekana tunawaonea wivu. Waache waendelee kunyonywa na Sinema Zetu, DSTV na Channel zingine.
Me nasahivi saburia Thor: Love & Thunder. We endelea msubiria Mkojani aendelee kusema “Nyamazaaa weweeee”