Ni vitu vipi vinaiangusha Tasnia ya Bongo Movie? Changia Mawazo

Nimecheka kwa sauti
 
Tanzania hakuna Film Schools hivyo kutarajia wafanye ubora zaidi ya hapo ni miujiza tu...hizo nchi zote unazozitaja zina Film Schools za kutosha.

Ipo haja ya kuandaa kizazi kipya kuhusu suala zima la filamu.

Watoto wangali Wachanga Wanapaswa kufahamu umuhimu wa screen play na jinsi ya kuzitumia...kwa leo hii ukitaka uwalazimishe hawa waliopo sio kazi rahisi maana wameshakomaa na waliingia kwenye hii tasnia bila kujali sana mambo mengi yanayoijenga tasnia...shortcut ni nyingi na ukiwauliza watakwambia ni ufinyu wa bajeti.

Suala la kuatengeneza Filamu ni gumu tofauti kabisa na wengi tunavyochukulia.
 
Walisha haribu hao kina wema na Uwoya na wengine kila scene wao ni kuweka mtu mwenye makalio makubwa tu halafu Ray yeye kazi ni kuigiza maisha ya kifahari hawasomi vitabu kupanua akili yani ubunifu hamna kazi kuuza sura tu. Na umalaya.Hopeless
 
Kuchanganya kingereza na kiswahili na kuangalia mpiga picha na hivyo kuonekana na maigizo full suite.
 
Kumbeee haunijuiiii (mkojani)[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my IPhone
 
Reactions: ABJ
Shida kubwa hawana ubunifu, wanakurupuka sana mfano

Jua Kali series ilianza vizuri sana, Lamata kalewa sifa kairefusha sasa hivi hamna kitu🚮🚮
 

Point yako ina make sense [emoji122][emoji122]
 
Kuna wakati nilidhani Watu Weusi hatuwezi haya mambo ya Movie ni ya Wazungu...lakini pia najiuliza mbona wale wa Marekani ni weusi wenzetu lakini wanaweza?.
Angalia taarifa ya habari ya BBC swahili utagunduwa kitu.

Halafu wafuatilie Wazambia wako mbali sana.
 

Budget zao ndogo ndo shida!!
Utalaam wa kushoot katika angle tofauti!!
Uhalisia mdogo sana hasa inapokuja sehemu ya kupiga mtu,kupigana,au kufanya kitu ambacho kinahitaj ufundi wa kimovie zaidi

hawana platform nzuri za kuuza kazi
Movie za kutafsiriwa
 
UMALAYA

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Waongozaji Wana ufahamu ndogo sana kuhusu dhana ya maigizo. Fila zinakosa kabisa muunganiko wa kimatukio kati ya muhusika na mazingira, uchumi wa nchi na upangaji wa matukio, matukio ya vijijini na mijini... Pia watunga story hawana uwezo kutunga visa vya kufikirika vingi vipo open vilevile wahusika wamekosa kabisa uwezo wa kuvaa uhusika.. waigizaji na waongozaji hawajui ung'eng'e, kingereza ni lugha inayokusanya audience kubwa hasa nje ya nchi.
WENGI WANAIGIZA KAMA MWAVULI WA MATUKIO MBALIMBALI
 
Tasnia hailipi najua wengi watabisha lingine tatizo bajeti DSTv, azam na Startime wamalipa china ya Million moja kwa Movie moja.
Lazima walipe pesa kidogo sababu hakuna cha maana kinachopelekwa kwenye screen,

Hebu itengenezwe filamu nzuri, yenye story ya kusisimua uone kama hawatawalipa vizuri.
 
Lazima walipe pesa kidogo sababu hakuna cha maana kinachopelekwa kwenye screen,

Hebu itengenezwe filamu nzuri, yenye story ya kusisimua uone kama hawatawalipa vizuri.
Sure,,, hawana vitu vya kumtoa nyoka pangoni.... Hakuna Cha bajeti wala nini filam bora hutegemea vichwa Bora vya wahusika na directors wa filamu husika
 
film school zipo mkuu.
Tasuba
UDSM
UDOM
Na graduates wapo
 
Sure,,, hawana vitu vya kumtoa nyoka pangoni.... Hakuna Cha bajeti wala nini filam bora hutegemea vichwa Bora vya wahusika na directors wa filamu husika
Screen play bora ndio uti wa mgongo (spine) ya filamu bora...swali ni je tunao au tunazalisha Waandishi wazuri wa Miswada?.

Baada ya screen play bora lazima uwe na Mpiga picha bora (Cinamatographer)...yaani mbali na kuwa na weledi wa kupiga picha pia awe na ufahamu wa tasnia ya filamu...aijue script, ajue kutumia story board, ajue namna ya kuwasilina na timu nzima inayohusika na Filamu, kwamba wanapojadili shotlist basi waongee lugha moja.

Tatu ni Muigizaji bora, bila muunganiko wa hizi kada tatu muhimu usitarajie zao lililo bora.
 
Umeona Sasa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…