Ni wakati sahihi kwa Serikali kuanzisha sheria za PreNup Kwa Wanaotaka kuingia kwenye Ndoa kupeusha matapeli

Ni wakati sahihi kwa Serikali kuanzisha sheria za PreNup Kwa Wanaotaka kuingia kwenye Ndoa kupeusha matapeli

Hii kitu inaweza kusaidia kwa kiasi fulani.
Uhalisia ni kwamba kila mtu atakuwa anatazama maisha yake na jinsi gani apambane kuongeza mali zake.

Prenup ni nzuri lakini itaua ndoa mazima.
Kama mwanamke anaingia ndani ya ndoa akifahamu mali fulani za mume wangu ni za kwake mwenyewe, there’s no way akawa submissive kwa % kubwa.

atafanya juhudi ya kutafuta pesa zake kwa nguvu.

Prenup itakuja kusababisha ndoa zisiwepo kabisa kuliko hali ilivyo sasa.

PreNup ndio ndoa yenyewe.
Hiki kilichopo sasa hivi ni utapeli wa wazi kabisa
 
Hujui serikali yenyewe ni upagani kwa sababu haina dini na haiamini katika Dini?
Katiba Inasema serikali haina dini ila watu wake wana dini wakiwemo viongozi wote ndio maana huapishwq kwa vitabu vya dini wote na kuna Wimborne wa taifa unaomtqja Mungu na Bungeni huanza bunge kwa sala na mahakamani watu huapa kwa kitabu cha dini
Upagani hauna nafasi
 
Safi sana, naona somo linazidi kuwaingia..... ndoa ni taasisi ya kitapeli inayojengwa kwa misingi ya udanganyifu.... KATAA NDOA
 
Wakati wa kifunga ndoa zinafungwa kiimani, kidini na kuna dini ni mpaka kifo kiwatenganishe. Wakati wa kuachana ni umafia mtupu.
 
Katiba Inasema serikali haina dini ila watu wake wana dini wakiwemo viongozi wote ndio maana huapishwq kwa vitabu vya dini wote na kuna Wimborne wa taifa unaomtqja Mungu na Bungeni huanza bunge kwa sala na mahakamani watu huapa kwa kitabu cha dini
Upagani hauna nafasi

Unaposema serikali haina dini kwa upeo wako na elimu yako huoni kuwa ni serikali ya kipagani?
Utamtajaje Mungu bila ya Dini?
Hizo elimu mliokotea wapi?
 
Safi sana, naona somo linazidi kuwaingia..... ndoa ni taasisi ya kitapeli inayojengwa kwa misingi ya udanganyifu.... KATAA NDOA
Tatizo la kuzaliwa nje ndoa ndio hili
Wewe umezaliwa na kukua kama mnyama pori asiye na malezi ya wanadoa ndio maana hujui faida ya ndoa
 
PreNup ndio ndoa yenyewe.
Hiki kilichopo sasa hivi ni utapeli wa wazi kabisa
Bro Robert,

Yaani ni hivi, kama mke wako atakuwa anajua mali fulani ni za kwako, na yeye mwisho wa siku hatakuwa na chake.

Usitegemee ukamwambia rudi nyumbani uwahi kunipikia, kuniandalia maji au hata kazi za ndani.

Atakuwa na mentality at the end of this union sina changu hapa, ninahitaji kupambana nipate changu.

Atatafuta kazi, mtalipa mfanyakazi wa ndani pesa wote, mtalipa bill kwa pamoja, sababu kila mtu atakuwa busy kutafuta mali zake.

Prenup inaweza kusaidia ila kwa kiasi kikubwa inaweza kuja kuvunja maana halisi ya ndoa na hali kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo sasa.

Kama kuna reference ya kesi za ndoa ambazo ziliingia prenup tuzilete tuone ni kwa kiasi gani imesaidia hili.

Lakini uhalisia ni kwamba taasisi ya ndoa itakuwa mbaya zaidi maradufu ya sasa kwa sheria hii. Jaribu tu kufikiria kwamba mke wako akufulie, akupikie, akuandalie maji, akupe tendo ipasavyo halafu anafahamu ukimuacha ataondoka kama alivyo hatagusa mali zako mlizowekeana.

Unafikiri ni kwa kiasi gani UPENDO utakuwepo? Zingatia neno UPENDO.
 
Inajulikana. Mwambie mwislamu/Mkristo aende serikalini badala ya utaratibu anaouelewa utanielewa nilichomaanisha.

Hao wanaenda kwa mawakala(hizo dini) lakini hakuna dini au dhehebu linalofungisha ndoa zaidi ya serikali.
Na serikali ndio inayovunja Ndoa. Hizo nyingine ni danganya Toto
 
Bro Robert,

Yaani ni hivi, kama mke wako atakuwa anajua mali fulani ni za kwako, na yeye mwisho wa siku hatakuwa na chake.

Usitegemee ukamwambia rudi nyumbani uwahi kunipikia, kuniandalia maji au hata kazi za ndani.

Atakuwa na mentality at the end of this union sina changu hapa, ninahitaji kupambana nipate changu.

Atatafuta kazi, mtalipa mfanyakazi wa ndani pesa wote, mtalipa bill kwa pamoja, sababu kila mtu atakuwa busy kutafuta mali zake.

Prenup inaweza kusaidia ila kwa kiasi kikubwa inaweza kuja kuvunja maana halisi ya ndoa na hali kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo sasa.

Kama kuna reference ya kesi za ndoa ambazo ziliingia prenup tuzilete tuone ni kwa kiasi gani imesaidia hili.

Lakini uhalisia ni kwamba taasisi ya ndoa itakuwa mbaya zaidi maradufu ya sasa kwa sheria hii. Jaribu tu kufikiria kwamba mke wako akufulie, akupikie, akuandalie maji, akupe tendo ipasavyo halafu anafahamu ukimuacha ataondoka kama alivyo hatagusa mali zako mlizowekeana.

Unafikiri ni kwa kiasi gani UPENDO utakuwepo? Zingatia neno UPENDO.

Mke hatakiwi kuambiwa arudi nyumbani kupika au kufanya kazi fulani yeye mwenyewe kwa hiyari(mapenzi) yake ndio anatakiwa afanye. Mapenzi sio wajibu mapenzi ni hisia za hiyari.

Mali za mke na mali za mme hazihusiani na mambo ya Upendo. Upendo wowote unaoshirikisha mambo ya mali au kazi huo sio upendo hapo tukazungumza biashara au uwekezaji.

Ndio maana vijana wa sasa wanakuambia ndoa ni utapeli kwa sababu ya fikra kama hiyo uliyoitolea mfano.

Hata unapomhudumia mkeo au watoto ni ishu ya upendo.

Linapokuja suala la mali hapo Unazungumzia HAKI. Na kwenye haki nadhani unaelewa
 
Kuna watu akili zao huwa by default zimeshikwa na Papa, Mwakasege, Sheikh Kipozeo, Sheikh Ponda, Kuhani Mussa, Mwamposa etc.

Wajinga Sana.
Kuna Watu ni Wakristo tena Wasabato ninawajua lakini Masuala ya ndoa wameyapeleka kiserikali.
Kuna wengine hawaamini kabisa mambo ya vyeti.
Kuna wengine wanaamini kotekote, itategemea na muktadha na wakati. Yaani mtu wakati huohuo ni kuabudu mizimu, muda huohuo anatafuta Mashekh muda huohuo anamchungaji wake alafu muda huohuo ni atheist
 
Hao wanaenda kwa mawakala(hizo dini) lakini hakuna dini au dhehebu linalofungisha ndoa zaidi ya serikali.
Na serikali ndio inayovunja Ndoa. Hizo nyingine ni danganya Toto
Inajulikana, ila imani za watu haziamini hili unalosema.
 
Back
Top Bottom