Ni wakati sasa benki zitanue 'ukomo' wa kutoa pesa kwenye ATMs, milioni moja haitoshi

Ndugu zangu!

Sijui vigezo walivyozingatia kwenye kuweka ukomo huo, lakini itoshe tu kusema zama zimebadilika sana.

Enzi hizo milioni iliitwa 'shitabalwa' [uncountable], na ilitosha kwa mambo mengi kwa walio wengi.

Tofauti kabisa na leo ambapo milioni MOJA unaweza kukaa kaunta tu ikayeyuka, pesa imezoeleka kwa wengi na imekuwa na matumizi mengi kirahisi.

Napendekeza angalau tuweze kutoa milioni TATU kwa siku kupitia ATMS, na 'mshindo' mmoja uweze kuvuta hadi MILIONI MOJA [emoji39]

Nasema uongo ndugu zangu?
Ukiongea na bank yako unaweza kutoa hata 15m kwa siku. Ila utatoa kwa awamu.
 
Pia umefika wakati wa kuanzishwa noti inayozidi tshs 10,000.

Mtu ukiruhusiwa kutoa pesa nyingi ATM utahangaika kurudia rudia kwa vile unatoa laki nne tu kwa mara moja - wakati noti mathalan ya tshs 50,000 ingekuwepo, mtu angeweza kutoa hata shs 2m mara moja bila kubadilisha mdomo wa ATM.

Raha nyingine ya noti kubwa ni kupunguza ukubwa wa mabulungutu ya kutembea nayo.
 
In jiwez voice
 
5m kidogo ina shepu.
Mpesa unaweka mpaka 10 million na unaweza kufanya malipo mpaka Million 3 au 5 kama sikosei. Issue ya ATM kutoa pesa nadhani 1 m sawa kwa security ila kama unafanya malipo kwa card unaweza kufanya mpaka 5 million kwa hiyo sioni sababu ya kutoa cash tuwekeze sana katika digital kama mobile money na App za banks siku hizi rahisi sana kufanya malipo njia ziko nyingi sana na safe.
 
Asante mkuu. Hata mimi naona.

Story yangu hapo juu ilikuwa kitambo kidogo, kama miaka 10 iliyopita.

Tumejiongeza sana hapa kati.

Shukurani kwa detail.
 
ATM ipo ili kuwasaidia uharaka wa kupata pesa za matumizi ya chap chap. Ukihitaji zaidi ingia ndani. Mtoa uzi hufikirii jinsi watu watakavyoanza kuuwawa kwenye ATM kisa wametoa mil 3 au 5!!!. Fikiria zaidi!
Kwani ukitoa ndani ndo huwezi kuuliwa kwa watumishi wa benki kuvujisha data?..

Kwanza kwenye ATM inaweza kuwa ni salama kama ipo eneo lililojificha au lililozibwa kidogo.
 
Pia umefika wakati wa kuanzishwa noti inayozidi tshs 10,000.

Mtu ukiruhusiwa kutoa pesa nyingi ATM utahangaika kurudia rudia kwa vile unatoa laki nne tu kwa mara moja - wakati noti mathalan ya tshs 50,000 ingekuwepo, mtu angeweza kutoa hata shs 2m mara moja bila kubadilisha mdomo wa ATM.

Raha nyingine ya noti kubwa ni kupunguza ukubwa wa mabulungutu ya kutembea nayo.
Uchumi je?
 
Back
Top Bottom