Kaka mkubwa unaweza kuwa na kundi la wadogo zako mmepata dharula, pesa ipo, lakini ATM limit ikasumbua.
Nakumbuka kuna siku miaka kama 10 imepita nilikuwa nakwenda Zenj na kundi la wadogo zangu. Sasa hapo mimi nimerudi likizo nimekuwa kama mgeni tena jijini kwangu Dar. Tukawa na safari ya utalii wa ndani Zanzibar.Nikawa nawahimiza tuwahi kwenda bandarini. Wao wanasema tuna muda, mbona unakuwa kama umesahau Dar ndogo hii.
Nikawaambia sitaki tuchelewe. Nikaambiwa haina noma.
Long story short, tumeondoka nyumbani, tukakutana na foleni barabarani. By the time tunafika bandarini tukawa tumechelewa meli. Na tunatakiwa kwenda Zanzibar usiku huo huo.
Tukaulizia options, tukaambiwa hapo ni kuwahi airport kupanda ndege tu.
Tukafika Dar airport kupiga mahesabu nauli kwa wote ikawa kama laki tano.
You can imagine watu wangekuwa wamezidi mara mbili nauli ingekuwa zaidi ya milioni, hela ipo, halafu unashindwa kuitumia.
Naelewa kuna rationale ya kuweka hii limit, mfano kama mtu anafanya wizi kwenye ATM asiibe zaidi ya milioni. Lakini, kama mtu ana hela nyingi na biashara nyingi, awe na uwezo wa ku evaluate risk, akiikubali risk awe na option yana kuongeza limit.
Nafikiri benki nyingi zina option hiyo.