Ni wakati sasa benki zitanue 'ukomo' wa kutoa pesa kwenye ATMs, milioni moja haitoshi

Ni wakati sasa benki zitanue 'ukomo' wa kutoa pesa kwenye ATMs, milioni moja haitoshi

Ukitaka kutoa nyingi ingia bank watakupa kiwango unacho kitaka, sasa kama mwizi kaiba kadi yangu ya ATM na kiwango kimewekwa 5 million. Unadhania hali itakuwaje ya alie ibiwa kadi ya atm yake?


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]

Benki zinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni, pesa inahitajika 24/7…. Mkuu umefikiria hili?
 
ATM ipo ili kuwasaidia uharaka wa kupata pesa za matumizi ya chap chap. Ukihitaji zaidi ingia ndani. Mtoa uzi hufikirii jinsi watu watakavyoanza kuuwawa kwenye ATM kisa wametoa mil 3 au 5!!!. Fikiria zaidi!

Kuingia ndani ni kwa muda wa mchana tu, pesa hailali mkuu…. kuna dharula sio za kusubiri.

Fikiria hilo pia.
 
Pia umefika wakati wa kuanzishwa noti inayozidi tshs 10,000.

Mtu ukiruhusiwa kutoa pesa nyingi ATM utahangaika kurudia rudia kwa vile unatoa laki nne tu kwa mara moja - wakati noti mathalan ya tshs 50,000 ingekuwepo, mtu angeweza kutoa hata shs 2m mara moja bila kubadilisha mdomo wa ATM.

Raha nyingine ya noti kubwa ni kupunguza ukubwa wa mabulungutu ya kutembea nayo.

We jamaa, hivi unadhani kuwa na noti yenye sifuri nyingi ndio kuwa na pesa nyingi?
 
na kuna account yao pia ya chapchap mwisho milioni tano ukizidiaha waniifunga mpaka ukajieleze na ubaidili

Uongo!

Sio kwamba wanaifunga, bali inabadilishwa ‘tariffs' na hivyo unaondolewa zile benefits za ChapChap.
 
Ndugu zangu!

Sijui vigezo walivyozingatia kwenye kuweka ukomo huo, lakini itoshe tu kusema zama zimebadilika sana.

Enzi hizo milioni iliitwa 'shitabalwa' [uncountable], na ilitosha kwa mambo mengi kwa walio wengi.

Tofauti kabisa na leo ambapo milioni MOJA unaweza kukaa kaunta tu ikayeyuka, pesa imezoeleka kwa wengi na imekuwa na matumizi mengi kirahisi.

Napendekeza angalau tuweze kutoa milioni TATU kwa siku kupitia ATMs, na 'mshindo' mmoja uweze kuvuta hadi MILIONI MOJA [emoji39]

Nasema uongo ndugu zangu?
Usiweke mayai yote kwenye kapu mmoja. Weka benki tofauti uwe na options pana.
 
We jamaa, hivi unadhani kuwa na noti yenye sifuri nyingi ndio kuwa na pesa nyingi?
Hujanielewa.

Ukiwa na shilingi laki moja, badala ya kuwa na noti 10 za sh 10,000 kila moja - waweza kuwa la noti 2 tu za 50,000 kila moja. Uwingi wa fedha unabaki palepale.
 
Uchumi je?
Uchumi umefanyaje mkuu?

Benki kuu ina utaratibu wa kuprinti fedha mpya kuzingatia kanuni za kiuchumi. Yaweza kuwa kubadili noti chakavu au kwa sababu nyingine. Nafasi ya kuingiza noti mpya kubwa bila kuathiri uchumi ipo.
 
Hujanielewa.

Ukiwa na shilingi laki moja, badala ya kuwa na noti 10 za sh 10,000 kila moja - waweza kuwa la noti 2 tu za 50,000 kila moja. Uwingi wa fedha unabaki palepale.

Haiwezekani, muhimu ni kuimarisha uchumi ili hiyo 10,000/- itoshe mahitaji mengi… kama ilivyo U$D 100 thamani kubwa.
 
Kuingia ndani ni kwa muda wa mchana tu, pesa hailali mkuu…. kuna dharula sio za kusubiri.

Fikiria hilo pia.

Bank sio pochi hadi useme kila utakapohitaji pesa lazima uifungue. Unataka kusema huna kiasi kidogo unachokuwa nacho nyumbani? Any way nafikiri ni bora uwe salama na uchukuwe pesa mchana kuliko kuchukuwa pesa muda wowote ukiwa na muuaji nyuma yako!
Kwani ukitoa ndani ndo huwezi kuuliwa kwa watumishi wa benki kuvujisha data?..

Kwanza kwenye ATM inaweza kuwa ni salama kama ipo eneo lililojificha au lililozibwa kidogo.

Sijasema huwezi kuuwa kama ukichukua fedha ndani. Tuangalie hatari kubwa ya kuvamiwa na kuuwawa iko wapi kati ya nje kwenye ATM muda wowote au Ndani kwa muda wa mchana.

Hakuna usalama kuchukuwa pesa nyingi ATM
 
Back
Top Bottom