Ni wakati wa kutoa ultimatum kwa watawala, bila Katiba Mpya ya wananchi hakuna uchaguzi

Ni wakati wa kutoa ultimatum kwa watawala, bila Katiba Mpya ya wananchi hakuna uchaguzi

Kwanza tujiulize, hiyo ultimatum itatolewa na wananchi gani? kumbuka wakati uchaguzi mkuu ukikaribia kuna vile vyama rafiki vya CCM vitaungana nao kushiriki uchaguzi, hivi kwa namna fulani vitasababisha kuhalalisha madai kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki kwa hii Katiba mbovu iliyopo.

Sasa unapozungumzia pawepo ultimatum, vyema tujiulize, hii ultimatum itaanzia wapi na kuishia wapi? ni wakina nani watakaokuwa wahusika wake? vipi kwa wale wengine ambao hawatataka kuhusishwa, wasipofanya hivyo wataonekana wabaya kwa lipi, kama wameamua kufanya hivyo kwa hiyari yao?

Utekelezaji wa hii ultimatum kwa mtazamo wangu, naona nao utakuwa mgumu kama ambavyo tunahangaika sasa hivi na hii michakato ya kuipata Katiba Mpya isiyokwisha, wala kujua Katiba Mpya yenyewe itakayopatikana itakuwa ya sampuli gani, naona kila tunapogusa bado safari yetu ni ndefu sana inayoendelea kuwanufaisha CCM.
Kunajambo unatakiwa kulielewa tume ya Taifa ya uchaguzi itakuwa na kazi ngumu sana kabla na baada ya uchaguzi,badala ya kushirikia na ccm kupanga matokeo kukata majina ya wagombea hizi mambo zitabiki historia

baada ya katiba mpya tume itakuwa na kibarua kizito mno

Nfano hapo jimboni kwenu Kuna idadi ya watu 100 ili mshindi apatikane inatakiwa mshindi atape asilimia fula ya kura zote kulingana na idadi ya watu wanaishi hapo kinyume na hapo tume itashindwa kutangaza mshindi itabidi watembee nyumba hadi nyumba kushawishi watu waende kupiga kura ili apatikane mshindi tofauti na sasa jimbo lina watu 100 wamejiandikisha watu 50 waliopiga kura watu 30 Batili kura 10 mshindi anapatika kwa jumla ya kura 20 kwa katiba mpya hakuna mshindi.

Kuhusu vyama pandikizi automatically vitakimbia uwanja wa vita.
 
Labda wasisitizie na kukazia zaidi.

Binafsi sijawahi kusikia kauli hiyo ya "Bila Katiba Mpya Hakuna Uchaguzi" wakiikana CHADEMA, hata kwenye hayo mazungumzo ya maridhiano.

Kinachotakiwa sasa ni kukumbushia hilo, kwamba hata kama walinyamaza kidogo, sasa ajenda hiyo imerudi juu kabisa zaidi ya ajenda nyingine yoyote.
Na tokea sasa, hiyo ndiyo iwe sala yao katika kila mkutano watakaoufanya nchini kote.

Walitegeshewa kichaka na mama Tozo, kidogo kichaka hicho kilitaka kuwameza.

Na ifahamike wazi hapa, kazi ngumu siyo hiyo ya "Kutangaza, 'ultimatum' kazi muhimu ni kuhakikisha 'ultimatum' hiyo haidharauliwi na kupuuzwa.

Kwa hiyo CHADEMA ni lazima wajipange tokea sasa kuhakikisha kwamba 'ultimatum' hiyo itakapohitaji kutekelezwa, itafanyika kwa ufanisi mkubwa. Hapa ndipo palipo na kazi inayowasubili.
Umenena vema ila hapo mwishoni, kusema CHADEMA wajipange siyo sahihi. Bali tuseme kuwa wananchi wote tunatakiwa tujipange. Kama katiba tunayoitaka ni kwaajili ya wananchi, na tunaoitaka ni sisi wananchi, kwa nini tuseme CHADEMA pekee ndiyo wajipange? Tunaishukuru CHADEMA kwa kusimama mbele na kuwa kinara katika hili, lakini nguvu na msukumo wa wananchi wote wazalendo, ni muhimu zaidi.

Kwa vile wakati wote ubaya na mapungufu ya katiba yetu unahitimishwa na mifumo ya utawala ambayo inatokana na mamlaka yanayopatikana baada ya uchaguzi, sisi wananchi wote tulio wahanga wa katiba hii mbaya, tutamke kuwa bila katiba mpya, hakuna uchaguzi.

CCM kama taasisi haiwezi kutoa kauli kuwa bila katiba mpya hakuna uchaguzi, lakini wanaCCM mmoja mmoja au katika makundi madogo madogo nao wana uwezo wa kutamka hilo. Makundi ya wakulima, asasi za kiraia, wanaharakati, vyama vya kitaluma, vyama vya wafanyakazi, n.k. wote hao wana uwezo wa kutamka kuwa bila katiba mpya, hakuna uchaguzi.

Uchaguzi ndiyo tukio kubwa linaloshirikisha wananchi wote, na kwenye tukio hilo kubwa, ndipo tunaweza kushikamanishwa sisi sote.
 
Maadam Mama ameamua kutumia njia ya majadiliano, tumpe ushirikiano, tumpe muda na sio amri!

Ni kweli, nchi ni mali ya wananchi na ndio wenye katiba iliyompa kiongozi wao mamlaka yote.

Kwa vile tayari ipo, ili ifike mwisho ni lazima Watanzania tuitane ndipo tuitamatishe na ndicho anachofanya sasa Rais Samia

Kiukweli kabisa wengi hawaijui katiba, yote Samia anayoyafanya ni kwa mujibu wa katiba!. Kwa bahati nzuri sana, humu jf, tupo baadhi yetu tunaijua katiba na tukaamua kujitolea kuwafundisha wengine kuhusu katiba, angalia response ya members humu kwenye somo hili Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio ila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
Kwa mujibu wa katiba yetu, imempa mamlaka rais wa JMT atafikia maamuzi yeye kama yeye bila kufuata ushauri wa yeyote!.

Kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa Tanzania ni executive president, hivyo kila kitu ni rais, na watendaji wote wa serikali Wanafanya kila kitu kwa niaba ya rais.

Naunga mkono hoja.

Mbona Mama ameruhusu mchakato uanze!.

Naunga mkono hoja

Japo sijaifuatilia hii ila atakuwa ni Mama, she has all the powers vested on her kwa mujibu wa katiba.

Hili neno!.

Naunga mkono hoja

Naunga mkono hoja, hata mimi hili niliwahi kushauri humu Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Naunga mkono

Hiki ndicho anachokifanya Mama

Naunga mkono hoja
P
Asante Pascal kwa kupitia aya moja moja kwenye bandiko langu, na kulisisitiza, kuunga mkono au kulitolea ufafanuzi.

Ni kweli Rais Samia ameufufua mchakato wa katiba mpya, lakini msukumo, spidi, na mwelekeo ni wa kutia shaka kwa sababu mchakato mzuma hauna nguvu ya kisheria wala ratiba ya utekelezaji.

Kulistahili kuwepo kwa sheria ndogo ya kuongoza mchakato mzima,. Kulistahili kuwepo hadidu za rejea. Wananchi walistahili kutambua kwa uwazi juu ya kinachoendelea, hatua itakachopitia na hatima yake. Mathalani, kinachoendelea sasa, ni mwendelezo na maboresho ya maoni ya wananchi waliyoyatoa kwa Tume ya jaji Warioba au ni mchakato mpya kabisa? Ni uboreshaji wa katiba pendekezwa ya Bunge la katiba au ni mchakato mpya? Kama ni maboresho, ni vipengere gani vinavyotazamwa na kufanyiwa marekebisho?

Kama utungaji wa sheria ya katiba mpya, uchukuaji maoni kutoka makundi yote ya kijamii, bara na visiwani, vikao vya Bunge la katiba na uandaaji wa katiba pendekezwa vilifanyika ndani ya miaka miwili tu, inawezekana vipi marekebisho yanashindwa kukamilika ndani ya miaka miwili?

Haya wanayoyaita eti maboresho ya katiba pendekezwa iliyotokana na maoni ya wananchi, tangu mwakajana tunaambiwa kuwa yanafanywa lakini mpaka leo siwezi kusema kuna kubwa la maana ambalo wananchi tumeambiwa kuwa limekamilika.
 
Kunajambo unatakiwa kulielewa tume ya Taifa ya uchaguzi itakuwa na kazi ngumu sana kabla na baada ya uchaguzi,badala ya kushirikia na ccm kupanga matokeo kukata majina ya wagombea hizi mambo zitabiki historia

baada ya katiba mpya tume itakuwa na kibarua kizito mno

Nfano hapo jimboni kwenu Kuna idadi ya watu 100 ili mshindi apatikane inatakiwa mshindi atape asilimia fula ya kura zote kulingana na idadi ya watu wanaishi hapo kinyume na hapo tume itashindwa kutangaza mshindi itabidi watembee nyumba hadi nyumba kushawishi watu waende kupiga kura ili apatikane mshindi tofauti na sasa jimbo lina watu 100 wamejiandikisha watu 50 waliopiga kura watu 30 Batili kura 10 mshindi anapatika kwa jumla ya kura 20 kwa katiba mpya hakuna mshindi.

Kuhusu vyama pandikizi automatically vitakimbia uwanja wa vita.
Tume ya Taifa ya uchaguzi itaendelea kuwanufaisha CCM kwasababu ya muundo wake, wala usitazame vitu vidogo kama kukata majina ya wagombea na vingine, mchakato mzima wa zoezi, kuanzia kupiga kura mpaka kutangaza washindi, CCM na Tume wana mianya mingi ya kucheza rafu.

Nimekusoma lakini sioni kama umejibu hoja yangu, nachoona ulichozungumzia wewe ni baada ya Katiba Mpya kupatikana na vipi washindi wapatikane { asilimia za kupata washindi}, jambo ambalo mpaka sasa halipo.

Nilichozungumzia mwanzo, ni kuhusu ultimatum aliyoitoa mleta mada, ili Katiba Mpya ipatikane, hapo ndipo nikaonesha concern yangu hasa pale ambapo wananchi aliowazungumzia wasipoonesha ushirikiano kwenye hilo.

Ndipo nikahoji hao ambao hawataonesha ushirikiano watabanwa na nani? kwa vipi? hasa ukizingatia hii issue ya Katiba Mpya wapo wanaoitaka, na wasioitaka, hasa CCM na washirika wake? nijibu hapo.
 
Point of correction: Kuna Rasimu na Katiba iliyopendekezwa iliyotoka Oktoba, 2014! Usichanganye hapo!

Kwanini tuirudishe uliyoitaja 'Rasimu'? Wakati mazingira ya kisiasa, kiuchumi, kimfumo na hata kijamii yamebadilika? Ningedhani hoja yako ingekua na mashiko kama unge propose mchakato uanze upyaaa!

Unakumbuka makundi ya uwakilishi kwenye Bunge Maalum? Wavuvi, wafugaji nk? 60% ya waliokua wakitajwa kuwa wawakilishi wa makundi hawakua na lolote zaidi ya kupachikwa na vyama fulani fulani!

Ni namna gani mchakato huu hasa kwenye makundi ya uwakilishi utakua wa wazi? Binafsi nawafahamu watu fulani ambao hata kuku hawakua nao ila leo ni watu wazito!

Hebu tushirikiane kwa mijadala kama hii ya kufumbua bongo za Watanzania! Kuna tatizo mahali..unajua ni lipi? FIKRA!
Mkuu rasimu pendekezwa ndo ilileta sitofahamu mpaka sasa hatuna katiba mpya na hii ilichagizwa na wajumbe baadhi kutoelewa na kuzaa UKAWA wakidai kwamba maoni ya wananchi yalichakachuliwa.

Kuanza mchakato upya itakuwa kupoteza resource pesa ya umma wakati tayali mchakato usha fanyika uko nyuma nacho weza sema ni kwamba tunaweza boresha rasimu ya Jaji Warioba kwa kuweka Sawa sehemu tata hasa kuhusu muungano juu ya pendekezo la serikali 3 na mambo mengine ili kuendana na mazingira ya sasa.
 
Mkuu Kinkunti El Perdedo , SSH ana nia ya kweli kabisa na ya dhati kutupatia katiba mpya na hili nimelisema sana humu Ikitokea umeshauri mtu avae Hijab nyekundu, huyo mtu akavaa, utajisikiaje? Kwa hili, Big Up Rais Samia na Serikali yako kwa kuwa wasikivu

Japo watu humu wanawatania Chadema ni manyumbu!, hakuna manyumbu wakubwa kama CCM, kwasababu manyumbu wa Chadema ni wanachama tuu lakini manyumbu wa CCM ni hadi viongozi!. Rais Samia ndie Mwenyekiti wa CCM, akiishaonyesha nia na kusema, hakuna anayekohoa, japo kuna wahafidhina wa chini kwa chini, hawa wanaendeleza kusafishwa!.

Nimewaita CCM ni manyumbu wakubwa kuliko Chadema, kwasababu, ile 2015 hoja ya katiba mpya ilikuwepo kwenye ilani ya CCM, Mwenyekiti aliposema sio kipaumbele changu!, wote walinyamaza!, nikawauliza Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?
P

Pascal umeusema ukweli ulio dhahiri. Yawezekana unyumbu upo kwenye vyama vyote vya siasa, lakini unyumbu ndani ya CCM ni wa kiwango cha juu kuliko chama au taasisi yoyote nchini. Ndiyo maana akitoa tamko mwenyekiti wa CCM, ni sawa na kusema tamko hilo ndiyo tamko la mwisho la CCM.

Mliona wakati wa kura za maoni mwaka 2020, asilimia 75 ya wagombea wote waliochaguliwa na wajumbe kuwa wagombea kwenye nafasi za ubunge, mwenyekiti na wasaidizi wake, walikata majina, tena bila maelezo. Kuna mwanaCCM, kuanzia waliokatwa, viongozi wa mikoa na wilaya, mpaka wanachama wa kawaida, kuna aliyenyanyuka kuhoji chochote? Hakuna. Walikatwa watu waliopata kura 300 za wajumbe, wakachwa waliopata kura 100, au 50, anaenda kuwejwa aliyepata kura 3. Na wote, kimya!! Hiyo inaonesha jinsi Mwenyekiti wa CCM alivyo na nguvu kushinda wanachama wote, hata wakiwekwa pamoja.

Ndiyo maana hata kwenye hili la katiba mpya, haitazamwi sana CCM kama chama, bali maamuzi ya mwenyekiti wa chama. Maamuzi yake ndiyo yatakayotoa mwelekeo juu ya mwelekeo wa CCM kwenye kupatikana katiba mpya ya nchi.
 
Asante Pascal kwa kupitia aya moja moja kwenye bandiko langu, na kulisisitiza, kuunga mkono au kulitolea ufafanuzi.

Ni kweli Rais Samia ameufufua mchakato wa katiba mpya, lakini msukumo, spidi, na mwelekeo ni wa kutia shaka kwa sababu mchakato mzuma hauna nguvu ya kisheria wala ratiba ya utekelezaji.

Kulistahili kuwepo kwa sheria ndogo ya kuongoza mchakato mzima,. Kulistahili kuwepo hadidu za rejea. Wananchi walistahili kutambua kwa uwazi juu ya kinachoendelea, hatua itakachopitia na hatima yake. Mathalani, kinachoendelea sasa, ni mwendelezo na maboresho ya maoni ya wananchi waliyoyatoa kwa Tume ya jaji Warioba au ni mchakato mpya kabisa? Ni uboreshaji wa katiba pendekezwa ya Bunge la katiba au ni mchakato mpya? Kama ni maboresho, ni vipengere gani vinavyotazamwa na kufanyiwa marekebisho?

Kama utungaji wa sheria ya katiba mpya, uchukuaji maoni kutoka makundi yote ya kijamii, bara na visiwani, vikao vya Bunge la katiba na uandaaji wa katiba pendekezwa vilifanyika ndani ya miaka miwili tu, inawezekana vipi marekebisho yanashindwa kukamilika ndani ya miaka miwili?

Haya wanayoyaita eti maboresho ya katiba pendekezwa iliyotokana na maoni ya wananchi, tangu mwakajana tunaambiwa kuwa yanafanywa lakini mpaka leo siwezi kusema kuna kubwa la maana ambalo wananchi tumeambiwa kuwa limekamilika.
Binafsi hushangaa sana Vipi Vyama pinzani wanapoingia kwenye uchaguzi bila tume huru kweli are they serious? Au tunafanyana usenge?
 
Dah!

Mkuu 'Bams', naona leo umekula pilipili kali!

Hiyo mistari miwili niliyoinyanyua, nisingeweza kupata maneno fasaha kabisa ya kuwasilisha maneno hayo kama ulivyofanya hapa.

Lakini ni budi niseme, hata wakati wa Mwalimu Nyerere ilipokuwa Katiba hii inatumika bila kuhojiwa, si angalau huko kwenye chama chao cha CCM kulikuwa na uvuguvugu kidogo, ambako mambo yaliamuriwa kwenye vikao baada ya mijadala ya kutosha, na watu kutoa dukuduku zao kwenye mambo walivyoyaona.

Leo hii Mwenyekiti wa Chama, ambaye ndiye huyo huyo mkuu wa nchi, ndiye anayemaliza kila jambo bila ya mjadala wowote wala kuhojiwa na yeyote.
Hii inatokana na mtu huyo huyo mmoja ndiye anayempa ulaji mtu aliyeko kwenye chama au serikalini.

Kila mtu analinda maslahi ya tumbo lake kwanza na mwisho.
Rais mwenyewe yupo, hana uchungu wowote na nchi anayoiongoza. Hapo utategemea kitu gani?
Ndugu yangu Kalamu, tukitaka kuwa wakweli wa nafsi zetu, na hasa sisi wa umri wa Pascal Mayala na zaidi, ni dhahiri wakati wa mfumo wa chama kimoja, kulikuwa na demokrasia ya kuwango fulani (ukiacha demomrasia ya vyama vingi) kuliko ilivyo sasa.

Hata kwenye uchaguzi (ukiacha zile kura za Rais za ndiyo au hapana), kwenye ubunge na udiwani, kulikuwa na uchaguzi halisia. Wagombea walitakiwa kusafiri kwenye gari moja, kulala chumba kimoja, kula pamoja; yote ilikuwa kuhakikisha hakuna rushwa ya aina yoyote au mbinu chafu. Aliyetangazwa kuwa mbunge, ni kweli alikuwa amechaguliwa na wananchi.

Vikao ndani ya chama, vilikuwa vya uhuru mkubwa sana. Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa machozi alipopendekeza jina la Kawawa kuwa Katibu mkuu, wajumbe kabla hata ya kupiga kura, wakaanza kutikisa vichwa kumgomea. Mwalimu Nyerere aliinama kwa muda, wajumbe hawakujua ni kwa nini, baadaye alitoa leso mfukoni, akapangusa machozi yake. Ndipo wajumbe walipogundua kuwa Mwalimu alikuwa analia kutokana na wajumbe kuonekana kutomkubali Kawawa kuwa katibu mkuu wa chama.

Mwalimu kwa taabu akasema, "nimfananishe na nani Rashid katika nchi hii? Wakati wote tulipokuwa na jambo ambalo hatuna uhakika kama litafanikiwa au kama wananchi watalikubali au kulikataa, tulimpa Rashid akatangaze. Hata lilipoonekana jambo hilo kukataliwa na wananchi, Kawawa alisemwa vibaya na kulaumiwa, sisi sote tulikaa kimya, Kawawa hakujitetea, aliibeba aibu ya sisi sote". Baada ya maneno hayo ukumbi mzima ulilipuka na kuimba, Kawawa, Kawawa, Kawawa. Lakini CCM hii ya leo, kweli kuna mwanaCCM tena mjumbe wa Halmashauri Kuu wa kumfanya Mwenyekiti atoe machozi kuomba kuungwa mkono kwenye maamuzi?

Wakati ule wa G55, wabunge wa Bunge la chama kimoja, akina Kasaka, waliitikisa hasa Serikali, lakini hakuna aliyefanyiwa fitina. Kama ingekuwa ni hii CCM ya leo, hilo lingewezekana?

Ukweli ni kwamba, tunafikiria tunaenda mbele lakini kwenye mambo mengi tunarudi nyuma.
 
Pascal umeusema ukweli ulio dhahiri. .

Ndiyo maana hata kwenye hili la katiba mpya, haitazamwi sana CCM kama chama, bali maamuzi ya mwenyekiti wa chama. Maamuzi yake ndiyo yatakayotoa mwelekeo juu ya mwelekeo wa CCM kwenye kupatikana katiba mpya ya nchi.
Ni kweli kabisa na Tanzania tumshukuru sana Mungu for Samia, ni mtu mkweli bonafide genuine, atatupatia katiba mpya!,Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... hivyo tusimtibue kwa ma ultimatums, tumpe muda.
P
 
Naomba kuuliza ,Katiba Mpya inayozungumziwa ni ya kuwapa Wananchi mamlaka au ya kuwapunguzia ccm mamlaka na kuwapa wezi wengine in the name of Chadema?

Maana nimesikia somewhere kwamba ati Vyama vya siasa ndio vipendekeze Wataalamu wa kuandika Katiba,kuliko kuandika Katiba ya Wanasiasa Bora tubakie hivi hivi.

Majibu yote yapo kwenye bandiko.

Ndiyo maana tunapinga hata huu utaratibu wa kumpa msajili wa vyama vya siasa kuwa kiongozi mkuu kwenye mchakato wa uandaaji wa Katiba mpya.

Mutungi ni msajili wa vyama vya siasa. Katiba ni ya wananchi wote. Mutungi anasimamia mchakato wa katiba mpya kwa mamlaka gani?

Nawaunga mkono CHADEMA kugomea vikao vya katiba mpya vitakavyoendeshwa na Mutungi. Hatutaki katiba ya vyama vya siasa, tunataka katiba ya wananchi wote, katiba ya Taifa. Na hakuna suala la kusema afadhali tuendelee na katiba hii hii ya sasa. Tumekwishaona, na wananchi, nchi nzima, bara na visiwani, mpaka walioiandaa walikwishatamka kuwa katiba yetu ya sasa ni mbaya, haifai, hatuwezi kuendelea nayo. Lazima ipatikane katiba mpya, tena ya wananchi na siyo ya watu fulani wachache.

Nawapongeza sana CHADEMA kwa kuamsha ari na kutoa elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya. Vyama vingine vya siasa, asasi za kiraia, vyama vya kitaluma, majukwa na mitandao kama yetu hii ya JF, tuungane na CHADEMA kwenye hili ili kuweka mizania sawa kuwa ni sauti za wananchi. Iwe kama ummanulivyokuwa umeshiriki kwenye kutoa maoni yao kwa tume ya Jaji Warioba. Wakati ule, hakuna asasi, chama cha kitaluma au taasisi yoyote iliyosema katiba tuliyo nayo ni nzuri, tuendelee nayo hii hii.
 
Kwanza tujiulize, hiyo ultimatum itatolewa na wananchi gani? kumbuka wakati uchaguzi mkuu ukikaribia kuna vile vyama rafiki vya CCM vitaungana nao kushiriki uchaguzi, hivi kwa namna fulani vitasababisha kuhalalisha madai kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki kwa hii Katiba mbovu iliyopo.

Sasa unapozungumzia pawepo ultimatum, vyema tujiulize, hii ultimatum itaanzia wapi na kuishia wapi? ni wakina nani watakaokuwa wahusika wake? lakini pia, vipi kwa wale wengine ambao hawatataka kuhusishwa, wasipofanya hivyo wataonekana wabaya kwa lipi, kama wameamua kufanya hivyo kwa hiyari yao?

Utekelezaji wa hii ultimatum kwa mtazamo wangu, naona nao utakuwa mgumu kama ambavyo tunahangaika sasa hivi na hii michakato ya kuipata Katiba Mpya isiyokwisha, wala kujua Katiba Mpya yenyewe itakayopatikana itakuwa ya sampuli gani, naona kila tunapogusa bado safari yetu ni ndefu sana inayoendelea kuwanufaisha CCM.
Hakuna kibaya kisicho na wa kukiunga mkono.

Leo hii hata tukitaka kuweka utaratibu utakaowafanya viongozi wasitumie vibaya oesa ya Serikali, wapo ambao watataka hilo lisitokee, kwa sababu wao ni wanufaika ni mianya hiyo ya sheria.

Hata hii katiba yetu mbaya tuliyo nayo sasa, wapo wanufaika wengi wa moja kwa moja na wengine indirectly. Hao hawawezi kuwa nasi katika kuweka utaratibu ambao wao watakuwa hawana uhakika kama wataendelea kunufaika kama ilivyo sasa.

Wapi pa kuanzia kutoa ultimatum, nionavyo ni kwa kupitia taasisi mbalimbali mbalimbali, vyama vya siasa, vyama vya kitaluma, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima, majukwaa mbalimbali, n.k. Hawa wakishatoa matamko ya kitaka Serikali kuliweka suala la katiba mpya kwenye top priority, inakuwa tayari ni hatua.

Hakuna mapambano yasiyo na kiongozi. Na kwenye hili tayari CHADEMA wameonesha kuchukua nafasi ya uongozi. Kuwa kiongozi kuna gharama kubwa, na siyo kila mtu anaweza kuwa kiongozi, hasa kwenye mapambano. Kwa hiyo ni vema kuwaunga mkono CHADEMA kwenye hoja hii ya katiba maana wanalo jukwaa tayari, tena jukwaa kubwa.
 
Ifike wakati Watanzania tutoe amri kwa watawala kwamba kama hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024, wala uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Nchi hii ni ya Watanzania. Watanzania ndio wanaotakiwa kuwa na maamuzi ya namna gani wanataka nchi yao ifanye kila kitu.

Katiba hii ambayo Baba wa Taifa alisema inamfanya Rais kuwa dikteta sasa ifike mwisho. Rais anatakiwa kupewa mwongozo tuliokubaliana namna anavyotakiwa kutuongoza, na siyo yeye kutupangia namna anavyotaka kututawala kama ilivyo sasa.

Leo hii kila kitu ni Rais, kama vile nchi ni ya Rais. Kodi ni ya mwananchi, lakini Rais ndiye anakuletea mkurugenzi kuja kusimamia matumizi ya pesa yako. Hata ukiona huyo mkurugenzi anaiba, wewe unayetoa pesa huna uamuzi, mpaka aliyemteua apende, asipopenda, mteule wake anaendelea kutafuta pesa ya wananchi na hamna uwezo wa kumfanya chochote.

Fikiria, mpaka pesa ya wananchi, siku hizi inatajwa kuwa ni pesa ya Rais, eti Rais emetoa bilioni kadhaa kwaajiki ya ujenzi wa kisima, zahanati, shule, n.k.

Hata huko kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri na mifumo mizuri ya utawala, siyo kwamba watawala walikuwa malaika, bali pressure ya wananchi iliwalazimisha watawala kukubali matakwa ya wananchi.

Kwa kuwa Serikali inalegalega, na kupiga danadana nyingi kuhusiana na suala la katiba nzuri mpya, katiba ya wananchi, lazima nguvu ya wananchi ishike hatamu, na Serikali ilazimishwe kufuata matakwa ya wananchi.

Na kwenye hili wananchi tushikamane, tuache mambo ya uCHADEMA, uCCM, uCUF, uACT, au tofauti zile nyingine za kijinga eti huyu ni sukuma gang, yule ni msoga gang, nasema huo ni upuuzi, sote tuunganishwe na utaifa wetu.

Leo mmesikia kuwa TANESCO, inayoendeshwa kwa ruzuku ya Serikali ya bara (nishati siyo suala la muungano) imesamehe deni la zaidi ya shilingi bilioni 60 iliyokuwa ikiidai Zanzibar. Hizi ni pesa za wananchi walipa kodi. Msamaha huo umetolewa kwa namna gani? Ni utaratibu upi uliofuatwa? Ni nani aliyetoa uamuzi wa kusamehe hilo deni? Ana mamlaka hayo?

Mambo haya inawezekana yanafanywa ama kwa shinikizo ama kwa kujipendekeza kwa Rais kwa sababu ni mzanzibari. Hatupingi kusamehe deni, tena kwa sehemu mojawapo ya muungano au kutoa msaada inapolazimu, lakini ni utaratibu upi umefuatwa kwa shirika linaloendesha kwa pesa za walipa kodi kuweza kufuta deni? Mbona hatujawahi kusikia kuwa TANESCO imewafutia deni wadaiwa sugu wa huku bara?

Katiba mpya itayaweka haya mambo yote wazi, na kuweka taratibu zilizokubalika na ambazo kila mmoja, na hasa viongozi, watatakiwa kufuata.

Hii ya kila kitu Rais, haikubaliki kabisa kwa namna yoyote ile. Kwenye teuzi, Rais aishie kuwateua mawaziri tu ambao wataidhinishwa na wabunge. Wengine wote waajiriwe au wachaguliwe. Wakivurunda, mamlaka za uajiri ziwafukuze kiurahisi.

Katiba siyo ya akina Lisu na Mbowe, siyo ya Rais wala Mutungi, siyo ya Chongolo, bali ni ya Watanzania wote. Yeyote anayetaka kujimilikisha uandaaji wa katiba ni adui yetu sote. Yeyote anayetaka kutushirikisha sote kwenye kupata katiba tunayoitaka, ni mzalendo wa Taifa letu, ni mtu mwenye upendo kwa Watanzania wa leo na vizazi vijavyo, na huyo ndiye tuandamane naye.

Hatutaki katiba maslahi ya watawala au wanasiasa tu, bali katiba itakayompa mamlaka makubwa mwananchi.
Hoja nyepesi kwa masuala mazito. Hoja zako zote hazina uhusiano na Uchaguzi.
 
Ni kweli kabisa na Tanzania tumshukuru sana Mungu for Samia, ni mtu mkweli bonafide genuine, atatupatia katiba mpya!,Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... hivyo tusimtibue kwa ma ultimatums, tumpe muda.
P
Ultimatum siyo za kumpinga Rais, lakini ni njia mojawapo ya kuongeza msukumo. Lakini pia itampa picha ya kuelewa namna tunavyoliona suala la katiba mpya kuwa kipaumbele juu ya vipaumbele vyote.

Wakati wa Mwalimu Nyerere, wanachuo pale UDSM walipogomea masomo na kufanya maandamano, na kisha kuwafukuza, siku ya kutangaza msamaha wao alisema, "unapopigania haki lazima huyo anayedhani ameshikilia haki yako umwoneshe kuwa hiyo kweli ni haki yako, na unaithamini kuliko chochote. Uchukulie ni sawa na bidhaa yenye thamani, halafu mtu mmoja mjinga, akaipora, akakimbia nayo. Ukamkimbiza, baadaye akaingia ndani ya nyumba, akajifungia. Ikifikia hapo una mawili, ama kusema kuwa amekwishajifungia, nitafanyaje, basi unaondoka, na hiyo bidhaa yako inayoitwa haki inakuwa imepotea. Au unaamua kuuvunja mlango. Lakini unapouvunja mlango, hujui huyo bwana humo ndani ana kitu gani. Lazima uwe umejiandaa kwa yote".

Lazima wananchi wamthibitishie Rais na Serikali yake na Bunge lake, kuwa wanataka katiba mpya ya watu wote, siyo kesho au keshokutwa, bali sasa. Ma isipopatikana, mambo mengine yatasimama. Iwe ninkauli thabiti hasa, na ya kumaanisha.
 
Ifike wakati Watanzania tutoe amri kwa watawala kwamba kama hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024, wala uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Nchi hii ni ya Watanzania. Watanzania ndio wanaotakiwa kuwa na maamuzi ya namna gani wanataka nchi yao ifanye kila kitu.

Katiba hii ambayo Baba wa Taifa alisema inamfanya Rais kuwa dikteta sasa ifike mwisho. Rais anatakiwa kupewa mwongozo tuliokubaliana namna anavyotakiwa kutuongoza, na siyo yeye kutupangia namna anavyotaka kututawala kama ilivyo sasa.

Leo hii kila kitu ni Rais, kama vile nchi ni ya Rais. Kodi ni ya mwananchi, lakini Rais ndiye anakuletea mkurugenzi kuja kusimamia matumizi ya pesa yako. Hata ukiona huyo mkurugenzi anaiba, wewe unayetoa pesa huna uamuzi, mpaka aliyemteua apende, asipopenda, mteule wake anaendelea kutafuta pesa ya wananchi na hamna uwezo wa kumfanya chochote.

Fikiria, mpaka pesa ya wananchi, siku hizi inatajwa kuwa ni pesa ya Rais, eti Rais emetoa bilioni kadhaa kwaajiki ya ujenzi wa kisima, zahanati, shule, n.k.

Hata huko kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri na mifumo mizuri ya utawala, siyo kwamba watawala walikuwa malaika, bali pressure ya wananchi iliwalazimisha watawala kukubali matakwa ya wananchi.

Kwa kuwa Serikali inalegalega, na kupiga danadana nyingi kuhusiana na suala la katiba nzuri mpya, katiba ya wananchi, lazima nguvu ya wananchi ishike hatamu, na Serikali ilazimishwe kufuata matakwa ya wananchi.

Na kwenye hili wananchi tushikamane, tuache mambo ya uCHADEMA, uCCM, uCUF, uACT, au tofauti zile nyingine za kijinga eti huyu ni sukuma gang, yule ni msoga gang, nasema huo ni upuuzi, sote tuunganishwe na utaifa wetu.

Leo mmesikia kuwa TANESCO, inayoendeshwa kwa ruzuku ya Serikali ya bara (nishati siyo suala la muungano) imesamehe deni la zaidi ya shilingi bilioni 60 iliyokuwa ikiidai Zanzibar. Hizi ni pesa za wananchi walipa kodi. Msamaha huo umetolewa kwa namna gani? Ni utaratibu upi uliofuatwa? Ni nani aliyetoa uamuzi wa kusamehe hilo deni? Ana mamlaka hayo?

Mambo haya inawezekana yanafanywa ama kwa shinikizo ama kwa kujipendekeza kwa Rais kwa sababu ni mzanzibari. Hatupingi kusamehe deni, tena kwa sehemu mojawapo ya muungano au kutoa msaada inapolazimu, lakini ni utaratibu upi umefuatwa kwa shirika linaloendesha kwa pesa za walipa kodi kuweza kufuta deni? Mbona hatujawahi kusikia kuwa TANESCO imewafutia deni wadaiwa sugu wa huku bara?

Katiba mpya itayaweka haya mambo yote wazi, na kuweka taratibu zilizokubalika na ambazo kila mmoja, na hasa viongozi, watatakiwa kufuata.

Hii ya kila kitu Rais, haikubaliki kabisa kwa namna yoyote ile. Kwenye teuzi, Rais aishie kuwateua mawaziri tu ambao wataidhinishwa na wabunge. Wengine wote waajiriwe au wachaguliwe. Wakivurunda, mamlaka za uajiri ziwafukuze kiurahisi.

Katiba siyo ya akina Lisu na Mbowe, siyo ya Rais wala Mutungi, siyo ya Chongolo, bali ni ya Watanzania wote. Yeyote anayetaka kujimilikisha uandaaji wa katiba ni adui yetu sote. Yeyote anayetaka kutushirikisha sote kwenye kupata katiba tunayoitaka, ni mzalendo wa Taifa letu, ni mtu mwenye upendo kwa Watanzania wa leo na vizazi vijavyo, na huyo ndiye tuandamane naye.

Hatutaki katiba maslahi ya watawala au wanasiasa tu, bali katiba itakayompa mamlaka makubwa mwananchi.

Hii akili iliyotumika kuandika hili bandiko ni akili kubwa, lakini kwa bahati mbaya wenye uthubutu, na uelewa wa kutekeleza haya maoni sioni wikifika hata 1 million. Kuna namna wananchi wa nchi hii wamepumbazwa, na kuishia kujaa woga, huku wakiamini haki yao ni hisani ya viongozi. Bila machafuko ama jeshi kupindua serikali, sioni tukipata katiba mpya ya wananchi.
 
Ni wapi Katiba imeinyima Tume ya Uchaguzi uhuru?
Ukishaona rais yuko juu ya sheria, hapo hakuna uwezo wa taasisi yoyote kuwa na nguvu. Huu ndio uhalisia, na sio hayo maelezo unayotoa ww.
 
Hii akili iliyotumika kuandika hili bandiko ni akili kubwa, lakini kwa bahati mbaya wenye uthubutu, na uelewa wa kutekeleza haya maoni sioni wikifika hata 1 million. Kuna namna wananchi wa nchi hii wamepumbazwa, na kuishia kujaa woga, huku wakiamini haki yao ni hisani ya viongozi. Bila machafuko ama jeshi kupindua serikali, sioni tukipata katiba mpya ya wananchi.
Hii katiba itapatika kivyovyote, mim ni kada mtiifu wa ccm lakini niko mstari wa mbele kuakikisha tunapata katiba ya wananchi ukiona mtu anapinga katiba Mpya sio Rai wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom