Ni wakati wa kutoa ultimatum kwa watawala, bila Katiba Mpya ya wananchi hakuna uchaguzi

Ni kweli Rais Samia ameufufua mchakato wa katiba mpya, lakini msukumo, spidi, na mwelekeo ni wa kutia shaka kwa sababu mchakato mzuma hauna nguvu ya kisheria wala ratiba ya utekelezaji.
Kitu muhimu kuliko katiba mpya ni uwepo wa a political will, ya kupatikana kwa katiba mpya. JK alianzisha mchakato wa katiba mpya lakini hakuwa na a political will, sasa Samia anayo, kitu cha kwanza anachofanya ni kutoa uhuru wa kusemezana, wananchi wanataka nini, ikionekana tuirejelee rasimu ya Warioba na kuanzia ilipoishia, sawa. Ikionekana imepitwa na wakati, wananchi wanataka something new, sawa.

Baada ya kujiridhisha tunataka nini, ndipo sasa tuje kwenye legal framework ya nini kifanyike
Kulistahili kuwepo kwa sheria ndogo ya kuongoza mchakato mzima,. Kulistahili kuwepo hadidu za rejea.
Huu ndio uzuri wa mchakato wa Samia tofauti na mchakato wa JK. Mchakato wa JK aliunda Tume ya Warioba na kuipa hadidu, Samia anataka wananchi ndio watoe hadidu wanataka nini. Mchakato ule haukuwa right na hili nililisema Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio Samia is doing the right thing.
Wananchi walistahili kutambua kwa uwazi juu ya kinachoendelea, hatua itakachopitia na hatima yake. Mathalani, kinachoendelea sasa, ni mwendelezo na maboresho ya maoni ya wananchi waliyoyatoa kwa Tume ya jaji Warioba au ni mchakato mpya kabisa?
Samia katoa uhuru tuamue.
Ni uboreshaji wa katiba pendekezwa ya Bunge la katiba au ni mchakato mpya?
Samia katoa uhuru tuamue
Kama ni maboresho, ni vipengere gani vinavyotazamwa na kufanyiwa marekebisho?
Hili la vipengele linahitaji ujuzi, inahitajika elimu ya katiba watu waijue kwanza katiba iliyopo na madhaifu yake, ndipo tupendekeze katiba mpya. It's very unfortunately hatuna kipindi chochote cha uelimishaji umma kuhusu katiba popote!. Mimi nimejitolea humu JF, Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio ila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani? angalia response utashangaa!.
Mchakato ule was wrong, lets do it right sasa!.
Haya wanayoyaita eti maboresho ya katiba pendekezwa iliyotokana na maoni ya wananchi, tangu mwakajana tunaambiwa kuwa yanafanywa lakini mpaka leo siwezi kusema kuna kubwa la maana ambalo wananchi tumeambiwa kuwa limekamilika.
Give it time. kwa huu muda uliopo mpaka uchaguzi wa 2025, hautoshi kutupatia katiba mpya bora, ila unatosha kubadili sheria na kuisuka upya NEC tukafanya uchaguzi Mkuu huru na wa haki, ndipo tuje kwenda kwenye katiba mpya. Tumemshauri Mama Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
na amepokea ushauri huu, kazi inaendelea.
P
,
 
Ultimatum siyo za kumpinga Rais, lakini ni njia mojawapo ya kuongeza msukumo. Lakini pia itampa picha ya kuelewa namna tunavyoliona suala la katiba mpya kuwa kipaumbele juu ya vipaumbele vyote.
ultimatum sio mjadala ni amri, sio busara kumuamrisha rais ambaye ni Mkuu wa nchi.
Lazima wananchi wamthibitishie Rais na Serikali yake na Bunge lake, kuwa wanataka katiba mpya ya watu wote, siyo kesho au keshokutwa, bali sasa. Ma isipopatikana, mambo mengine yatasimama. Iwe ninkauli thabiti hasa, na ya kumaanisha.
Kiukweli wanaotaka katiba mpya ni the elites ambao ni just 20% ya Watanzania wote!. Wananchi wa kawaida wao wanataka tuu mambo yaende.
P
 
Hii mada iko nje ya uwezo wako. Ni wapi mleta mada amesema hiyo katiba ni kwa ajili ya kuwapunguzia madaraka CCM na kuwapa CDM? Nyie wapotoshaji ndio mmekuwa na kuherehere kisha mnajitokeza mbele ya jamii na kuishia kupotosha. Pitia uzi wa mleta hoja uone kama kuna mahali anataka iwe katiba ya vyama.
 
Wazee wetu huwa na jicho la ndani la kuona mbali naomba kukuuliza swali mkuu PM je,rais SSH ana nia ya dhati kabisa ya kuipatia Tanzania Katiba mpya ? Na vipi kuhusu Chama chake kina nia pia hiyo hiyo ?
Hapa siyo suala la SSH, kuna watu wanajua watakuwa wajumbe na posho ilikuwa 350k per day huenda ikaongezwa.
Kama kweli wanania na katiba mpya tayari Warioba alishakusanya maoni na katiba pendekezwa ipo sasa kuna haja gani ya mchakato mpya?
Waibane serikali wamalizie sehemu iliyobaki àmbayo itatumia muda mfupi na gharama kidogo.
 
Kwa Hesabu za kawaida huwezi kuupata Katiba mpya Kabla ya 2025
Inawezekana, ikiwa mchakato hautaanza UPYA.

Tume ya Warioba ilishamaliza KAZI Kwa kiasi kikubwa.

Rasimu alosimamia Judge WARIOBA kabla haijaitwa KATIBA pendekezwa irudi mezani tufanye marekebisho kidogo, tuchague wajumbe wa Bunge la Katiba, hatimaye by May mwaka huu tunapata Katiba.

Kama haijapatikana Katiba mpya by Sept 2024, wananchi tutahakikisha uchaguzi unafanyika Kwa KURA YA WAZI mabarabarani na viwanjani.
 
ultimatum sio mjadala ni amri, sio busara kumuamrisha rais ambaye ni Mkuu wa nchi.

Kiukweli wanaotaka katiba mpya ni the elites ambao ni just 20% ya Watanzania wote!. Wananchi wa kawaida wao wanataka tuu mambo yaende.
P
Mbona tozo zipo, hizo wananchi walizitaka? Hii katiba ya mwaka 77 watanzania wote walishaelewa ya huko nyuma, kiasi kwamba ikabidi hiyo 77 ipatikane? Kwahiyo kwa mtazamo wako unataka ili kitu kibadilishwe ni lazima kieleweke na kila mwananchi?! Halafu bro una elimu ya chuo kikuu!
 
MNYIKA amekuwa akiirudia sana kauli hiyo.

Bila KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi hautafanyika uchaguzi wowote.

Sanduku la kura limeporwa na halijulikani lilipo,

Wananchi tunasubiri Kwa hamu kupiga KURA YA WAZI viwanjani na mabarabarani.

Tusubiri.
 
Kwenye issue ya KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi tutaidai hadharani.

HAKIKA, kama wanadhani wananchi tumelala, wasubiri movement zianze.
 

😆😆😆 Kuongea hayo mambo ukiwa umejificha Kwenye keyboard ni very easy

Toka nje, simama pale kariakoo then sema hayo uliyoandika, hapo ndio tutajua kweli Una maanisha
 
Naunga mkono HOJA 100%.

Viongozi ni WAAJIRIWA wa Wananchi hivyo kupewa ultimatum ni sawa kabisa.

Ni miaka 60 ya uhuru lakini Kila linapokuja suala la KATIBA mpya wanadai muda haitoshi Ili waendelee kubaka Sanduku la kura.

Mkipuuza HAKI ya wananchi, tutapiga KURA ya WAZI viwanjani na mabarabarani.
 
Pascal, kwa maelezo yako, zoezi la katiba mpya halina kikomo. Ikiwa hivyo, kwa nini tusielekeze juhudi zetu kwenye mambo mengine kwa sababu hili litakuwa limeshindikana katika kizazi hiki - why waste time and our limited resources.
 
Mimi huwa nashindwa kuwaelewa wale wanaodai eti ile Rasimu ya katiba ya Warioba imeshapitwa na wakati kwa sababu imepita miaka kumi na mambo mengi yamebadilika 🙄🙄 !!


Je ina maana yale yanayowekwa katika katiba ni mambo ya miaka kumi tu. ???!

Kisha baada ya miaka kumi katiba inatakiwa iandikwe nyingine maana ile imeshapitwa na wakati ????!

Hii ni Akili ya wapi ???!
 
Simply wanaodai RASIMU ya WARIOBA imepitwa wakati ni majizi na wanufaika wa wizi.

Hawashangai kwann Katiba ya 1977 yenye viraka Kila Kona, kutumika Hadi sasa hawaoni kuwa imepitwa wakati!!!!
 
Pascal, kwa maelezo yako, zoezi la katiba mpya halina kikomo. Ikiwa hivyo, kwa nini tusielekeze juhudi zetu kwenye mambo mengine kwa sababu hili litakuwa limeshindikana katika kizazi hiki - why waste time and our limited resources.
We will be wasting our time and our resources kama tutaendelea kuwa na katiba ambayo watu wakubwa watakuwa wanafanya mambo wanavyotaka wao na sivyo wanavyotaka wenye Nchi ambao ni Wananchi wenyewe wa Nchi hii !!
 
Simply wanaodai RASIMU ya WARIOBA imepitwa wakati ni majizi na wanufaika wa wizi.

Hawashangai kwann Katiba ya 1977 yenye viraka Kila Kona, kutumika Hadi sasa hawaoni kuwa imepitwa wakati!!!!
Na huo ndio ukweli mchungu. !!
 
Sioni ni vipi hao wananchi wanaweza kujimobilise bila kuwa mobilised na watu wenye sauti katika jamii !!
 
Sioni ni vipi hao wananchi wanaweza kujimobilise bila kuwa mobilised na watu wenye sauti katika jamii !!
Mkuu changamoto tunazozipitia kwnye maisha ya kilasiku kila kundi kwenye jamii zinatosha tumobilise zenyewe bilakutegemea watu wenye sauti.
 
SSH aliposhika madaraka ya uongozi wa nchi yetu wengine tuliamini alikuwa na maono ingawa hatukuwa na uhakika aliona mbali kiasi gani na alijiamini kiasi gani katika maono yake hayo. Hata hivyo taratibu alianza kubadilisha mwelekeo kiasi cha kupelekea vurugu nyingi ya kuvunja vikao vya ndani vya vyama shindani. Bila shaka hili lilitokana na ushauri wa kiusalama uliotolewa wenye lengo la kudhibiti vuguvugu la mabadiliko. Hitimisho la ushauri huo wa kusambaratisha vuguvgu la mabadiliko ni ile kesi ya ugaidi.

Tunaweza kusema kuwa mfumo ulifanikiwa kumbadilisha maono ya SSH na pengine hata kumkaripia kuwa maono yake yangepelekea kukabidhi nchi kwa "mabeberu"! Kwa sasa tunaweza kusema kimwelekeo tumepiga "U" turn. Wakati huo tumeaminishwa kuwa yapo mazungumzo ya maridhiano yanaendelea ingawa yanahusisha vyama viwili vikibwa tu. Tulitegemea msingi wa maridhiano endelevu ni katiba mpya. Wengine tumekuwa tukidhani agenda mojawapo ya hayo mazungumzo ya maridhiano ni kutafuta makubaliano kuhusu mchakato adilifu na wa wazi wa kufuata ili kupata katiba mpya bora. Kinyume chake tumetangaziwa kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaratibu hiyo kazi. Wakati huo huo mmoja wa wale tulioambiwa wanaridhiana akatangazi kutokuwa na imani na mpango huo!

Ndiyo kusema yale mazungumzo ya maridhiano yamesambaratika! Tunarudi kwenye zama za giza! Kwa mwendo huu hakika 2024 na 2025 tutashuhudia uchafuzi mbaya zaidi kuliko hata ule wa 2019 na 2020. Uchafuzi ujao utakuwa mbaya zaidi kwa sababu moja kubwa. Tofauti na kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akitoa amri, safari hii amri zitakuwa zinatolewa na watu wengi kama ambavyo tumekuwa tukiona: wapambe, machawa na wale wote waliopewa au kujipa kazi ya kuuhami na kuupigania utawala uliopo madarakani ikiwa ni pamoja na kuuwezesha kupata kipindi kingine. Kufikia hapo tumuombe sana Mungu atuwezeshe kupata busara na kufanya tafakuri ya kina kuhusu mustakabali wa nchi yetu. Tuwaombee viongozi wetu wa kiroho wapate hekima na ujasiri wa kututangulia katika hili. Mwaka 2014 kuna umoja wa madhehemu ya dini ulijitokeza hadharani kutoa kauli kuwa wasingeunga mkono Katiba Pendekezwa na kwamba muda wa kura ya maoni utakapofika wao wangeendesha kampeni ya kupinga hiyo Katiba Pendekezwa. Baadhi yetu tunaamini msimamo ule uliponya taifa. Mtazamo huo unahitajika zaidi sasa wakati ambapo tofauti na huko nyuma mgawanyiko wa kitaifa unaongozeka.
 
Mkuu changamoto tunazozipitia kwnye maisha ya kilasiku kila kundi kwenye jamii zinatosha tumobilise zenyewe bilakutegemea watu wenye sauti.
Hii itaishia kwenye social media tu na kwenye vijiwe !! Kitu chochote kinachotaka kipate sapoti kubwa ya watu ni lazima wawepo viongozi wa hicho kitu !!
 
Bajeti na katiba ni vitu viweli tofauti sana. Bajeti ni mpango wa muda mfupi: siku moja, wiki, mwezi, miezi 3, 6 au mwaka. Katiba na sheria mama inayoandikwa ile kiweze kutumika muda mrefu kama miaka 50 au hata 100. Misingi ya Rasimu ya Warioba kwa sehemu kubwa hayajabadilika. Sana sana leo hii hatuhitaji kubadilisha hiyo misingi yake; pengine kuna mambo machache madogo madogo yanayohitaji kubadilika kutokana zaidi na uzoefu tuliopata miaka ya awamu ya 5. Kuna mambo ya msingi sana tumejifunza kama nchi ambayo ni muhimu sana katiba ikayazingatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…