Ni wakati wa kutoa ultimatum kwa watawala, bila Katiba Mpya ya wananchi hakuna uchaguzi

Hii itaishia kwenye social media tu na kwenye vijiwe !! Kitu chochote kinachotaka kipate sapoti kubwa ya watu ni lazima wawepo viongozi wa hicho kitu !!
Viongozi wapi unataka mkuu wa Dini au Katiba ya nani kama ni yetu wananchi Viongozi watakuwepo kwasabu ni wanachi katiba inatuhusu watu wote wenye nianjema na Taifa letu.
 
Mama ameruhusu mchakato uendelee lakini naona kama hatutaki.

Lakini mwisho wa yote tukianzia ngazi ya familia ni nani mwenye sauti ya mwisho ndani kwako, je ni mtoto, beki tatu, Mama au Baba?
 
Viongozi wapi unataka mkuu wa Dini au Katiba ya nani kama ni yetu wananchi Viongozi watakuwepo kwasabu ni wanachi katiba inatuhusu watu wote wenye nianjema na Taifa letu.
Hata kwenye ibada huwa zipo kengele zinawakusanya waumini au adhana kwenye maspika na shuleni tulikuwa tunakusanywa kwa kengele mkuu 😅😅🙏🙏
 
Umesema kila kitu ni wakati wa kuchukua hatua,leo hii Ethiopia umeme ni tsh elfu kwa mwezi na maji tsh 10k kwa mwaka hio haijalishi matumizi
 
Umenena kweli !
 
ultimatum sio mjadala ni amri, sio busara kumuamrisha rais ambaye ni Mkuu wa nchi.

Kiukweli wanaotaka katiba mpya ni the elites ambao ni just 20% ya Watanzania wote!. Wananchi wa kawaida wao wanataka tuu mambo yaende.
P
Mamlaka yote ya utawala hutoka kwa umma wa wananchi.

Japo siyo wakati wote, lakini wananchi katika ujumla wao wana mamlaka na haki ya kuiamrisha Serikali na kiongozi mwingine yeyote inapoonekana matakwa yao yanapuuzwa, au kucheleweshwa bila sababu.

Kama tangu tuambiwe kuwa mchakato wa katiba mpya umefufuliwa, halafu mpaka leo hatujui kama tunaanza mchakato mpya au kuboresha ule uliokuwepo, hiyo katiba kuja kupatikana si itachukua miaka hata zaidi ya 50?

Hatujaumbwa na Mungu kuishi miaka 1,000 au zaidi. Muda mfupi wa maisha tuliopewa ni lazima tuutumie vizuri kuyakamilisha yanayotakiwa kuyafanywa.

Yaani miaka miwili, hatujui hata tunataka nini, kuanza upya au kuendeleza tulipoishia na kufanya maboresho. Labda ndiyo maana nchi yetu hatua zake kwenye maendeleo ni mwendo wa kinyonga.

Malaysia tuliokuwa nao sawa kwenye uchumi mwaka 1961, taarifa ya UNDP inasema kuwa tukiendelea na speed yetu iliyopo, Malaysia wakabakia pale pale, wasiendelee zaidi, kufika mahali walipo, kwa Tanzania itachukua miaka 250. Hiyo inasababishwa na haya tunayoyafanya na tunaona kuwa ni sahihi. Hatujui thamani ya wakati.
 
[emoji38][emoji38][emoji38] Kuongea hayo mambo ukiwa umejificha Kwenye keyboard ni very easy

Toka nje, simama pale kariakoo then sema hayo uliyoandika, hapo ndio tutajua kweli Una maanisha
Usitishe watu. Tutayasema haya usiku na mchana, kwenye vyombo vya habari na hata sehemu za wazi kama barabarani au majukwaani.

Kama umezoea kutisha watu, umepitwa na wakati. Ulimwengu wa leo siyo wa kumtisha yeyote.
 
Ukweli hiyo hoja haina msingi. Hao wanaosema kuwa katiba pendekezwa imepitwa na wakati, ina maana wakati ule zoezi lingekuwa limekamilika, sahizi tungeanza kuandika nyingine upya au kuifanyia maboresho?

Katiba inaandikwa kukidhi matakwa ya nchi kwa muda hata zaidi ya maiaka 50.
 
Sioni ni vipi hao wananchi wanaweza kujimobilise bila kuwa mobilised na watu wenye sauti katika jamii !!
Ni kweli. Hakuna mapambano yasiyo na viongozi. CHADEMA wameonesha njia, na wengine waje. Wananchi tuungane na watu wote wanatoa uongozi katika kudai katiba.
 
Kama wananchi wanataka katiba mpya mnazunguka na helikopta kutafuta nini?
 
Mamlaka yote ya utawala hutoka kwa umma wa wananchi.
Ni kweli na ndivyo katiba yetu inavyosema.
Japo siyo wakati wote, lakini wananchi katika ujumla wao wana mamlaka na haki ya kuiamrisha Serikali na kiongozi mwingine yeyote inapoonekana matakwa yao yanapuuzwa, au kucheleweshwa bila sababu.
Very unfortunately hatuna haki hii ya kuanzisha, ila serikali isipotimiza wajibu wake, ah kunitendea ndivyo hivyo, tuna haki ya kuishitaki mahakamani, na mahalama ndio, ikaiamrisha serikali na sio wananchi kuamrisha serikali.
Kama tangu tuambiwe kuwa mchakato wa katiba mpya umefufuliwa, halafu mpaka leo hatujui kama tunaanza mchakato mpya au kuboresha ule uliokuwepo, hiyo katiba kuja kupatikana si itachujua miaka hata zaidi ya 50?
Lazima tujifunze kusikiliza, hatujaambiwa popote na yeyote kuwa mchakato wa katiba mpya umefufuliwa!, bali Mama aliunda kikosi kazi, ndio wananchi wakataka katiba mpya.

Mama akatoa room tusemezane, tunataka mchakato uweje, tuendelee na ile ya Warioba ila tuiboreshe, tuanze upya, au tumalizie na ile katiba pendekezwa ilipoishia tuipigie jura, it's up to us sisi wananchi. Msajili wa vyama vya Siasa, Jaji Mutungi ameanza kusemezana na vyama vya siasa.
P
 
Wapo watu wanadhani watu wote ni wajinga wajinga tu hawajui kitu ! Na ukizowea tabia za kudanganya danganya watu wakati mwingine unasahau unaanza kujidanganya mwenyewe !! 😂😅
 
Ni kweli. Hakuna mapambano yasiyo na viongozi. CHADEMA wameonesha njia, na wengine waje. Wananchi tuungane na watu wote wanatoa uongozi katika kudai katiba.
Kabisa !
 
...hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024, wala uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Mleta mada kama utajali ninaomba unipatie mnyororo wa thamani wa kupata Katiba mpya. Na kwa Kila fundo la mnyororo huo unitajie wanaufaika.

Yaani kuanzia uratibu wa maoni wa ukusanyaji wa maoni, uchakataji na uandaaji nyaraka za kumsaidia kukusanya maoni..... mlolongo wote ukiwahusisha watu wa ugavi, watoa huduma....mpaka kupata katiba mpya.

Hii itasaidia kujua hawa wanaopiga zumali la katiba mpya wanafanya hivyo kuburudisha wasikiliza zumali na wao pia ama wanapiga zumali kwa sababu Kuna mlundikano wa kandarasi na posho kibao unaviziwa??

Swali chonganishi ama?
 
Kuna mahali hapo juu Pascal Mayalla amauliza mbona mama ameruhusu mchakato wa katiba uanze?
Nio acho mimi kilichofanyika ni kama umemuozesha mwanao mke na kumwambia kazaeni muniletee wajukuu kisha una mpatia mabox ya condom kama zawadi atumie. Nimeeleweka!
 
Ikiwezekana kwa Kila njia itakayotumika kupata Katiba hiyo, tupewe mnyororo wa thamani wa Kila njia na wanaufaika wake na namna watakavyonufaika katika viwango vya malipo ya fedha.

Hili ni muhimu katika kutusaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya hili.
 
Posho zitaendelea kuliwa kila siku hata bila Katiba ! Hujasikia juzi hapa watu wanepitisha kwa nguvu kubwa posho ya bilioni 47 !!

Katiba mpya bora itakuja kuzuwia vitu vya namna hiyo !!
 
Na kwenye hili wananchi tushikamane, tuache mambo ya uCHADEMA, uCCM, uCUF, uACT, au tofauti zile nyingine za kijinga eti huyu ni sukuma gang, yule ni msoga gang, nasema huo ni upuuzi, sote tuunganishwe na utaifa wetu.
uTaifa kwanza,
uchama baadae na pale tu utakapoendana na uTaifa.
Kama unaipenda Tanganyika, utalitetea Taifa hili bila kujali madhara yake kwenye chama chako.
Mgongano wa Nia wa wazi ( clear conflict of interest)

Swali pana ni - Mzanzibari anapata wapi uhalali wa kuifanyia maamuzi Tanganyika katika mambo yasiyo katika Muungano?

Hatutaki katiba maslahi ya watawala au wanasiasa tu, bali katiba itakayompa mamlaka makubwa mwananchi.
Tanganyika ni Republic, nashauri kwenye Katiba mpya tuondoe kabisa dhana ya "utawala/kutawala/Mtawala" na tuwe na "Uongozi/Kuongoza/Kiongozi"
 
Tukianza kuangalia mnyororo wa thamani, tutarudi kule kule kwenye bora katiba, Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio sasa let's do the right thing tupate katiba bora na sio bora katiba.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…