Mimi nilikuwa msimamizi mkuu ktk Moja ya kituo kata ya Ngokolo -Shinyanga Manispaa
Kituo chetu kilikuwa na registered voters 428
Hadi inafika saa 10:00 jioni siku hiyo, ni wapiga kura 31 tu ndo walifika na kupiga kura siku hiyo!!
Tulipopeleka matokeo yetu kwa Returning Officer (Mtendaji wa Kata), tulikuta fomu zingine kabisa za matokeo za kituo chetu zikionesha kuwa Samia (CCM) amepigiwa kura 412 na wagombea wengine wakagawiwa zilizobaki
Hali ilikuwa hivyo hivyo katika vituo vyote vya kupigia kura
Hivyo, tulilazimishwa kusaini fomu hizo ambazo honestly hakuna aliyejua zimetokea wapi. Na ilikuwa ukileta ubishi, tulikuwa tunaambiwa kabisa baya lolote litakalokukuta, usilaumu na ndugu zako wasije kulaumu.
Ilikuwa ni wakati mgumu sana kukumbana nao sisi wasimamizi wa uchaguzi huo. Ilikuwa ni kuchagua kukubaliana nao au upoteze kazi au ufe kabisa!!
Kwa kifupi uchaguzi ule ulikuwa very disgusting, uchafu mtupu. Na kamwe haumpi heshima yeyote anayejiita kiongozi aliyetokana na uchaguzi huo!!