Ni wapi naweza kupata Kiwanja cha chini ya milioni 4 kwa Dar es Salaam?

Ñnjoo nikuuzie kiwanja changu kipo kigamboni magorofani dege hakina udalali wala nn nione 0653054835 30*20 hakina migogiro

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Habari Wana JF,

Natafuta Kiwanja Dar es salaam Cha bei poa Chini ya Mil 4

Vigezo;
  • Eneo liwe lina upatikanaji wa maji na umeme
  • Pasiwe mbali sana na Mji(Ndani ya dar es salaam)
  • Eneo la kutosha vyuma ya vyumba 3 na choo 2.
Zungumza na madali, huwezi kukosa. Wengi wana grupu zao siku hizi, zinawasaidia sana kuhudumia wateja wao.

NB: Taja ukubwa wa kiwanja unachotaka (kwa Sq M) na sio aina au size ya jengo pekee. Ukinipa kiwanja hata cha sq.m 64 (8mx8m) naweza kuweka hapo nyumba yenye vyumba 3 na vyoo 2 kama utakavyo...... najenga kighorofa tu na basement!
 
Magoe na Majohe ni sehemu mbili tofauti? Au ni mimi ndiyo sijui kitu....
ni sehemu mbili tofauti.majohe ni njia ya gongo ka mboto wakati magoe ni njia ya kibamba
 
dah! ndo nauona uzi! kipo million 3 kiwanja njia ya chanika unashuka kwa zoo, boda hadi eneo la kiwanja buku
 
Mji mwema kiwanja 4m? Kwanza Mji mwema kuna kiwanja kitupu?!
 
Mji mwema kiwanja 4m? Kwanza Mji mwema kuna kiwanja kitupu?!
Inawezekana wewe ni mgeni, Kibugumo ipo kata ya mji mwema.

Ukitaka kiwanja kikubwa standard kuanzia million 8.

Mimi nina site hapo Kibugumo na viwanja kibao vipo wazi, kama unahitaji sema na siyo kuhisi na kubisha.

Huyo niliyemwambia anapata kwa bei hiyo ni wale wanaomega mashamba yao na kuuza vipande vidogo vodogo, still bado Kibugumo ni karibu kutoka mjini au ferry.
 
Ahaa kumbe Kibugumo. Hapo Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…