Pre GE2025 Ni wazi CHADEMA sasa imegawanyika, kuirudisha kuwa pamoja ni Mbowe kutogombea uenyekiti tu

Pre GE2025 Ni wazi CHADEMA sasa imegawanyika, kuirudisha kuwa pamoja ni Mbowe kutogombea uenyekiti tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yoda kwanini CCM mnamuogopa Mbowe? Let us talk as friends...
Hapa umetufunga kamba. Wenje ndio alienda na Abdul nyumbani kwa lissu. Wenje ndio ameshawishiwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti. Kama mbowe akiendelea makamu wake anayemtaka Ni wenje, fikiria hiko chama kitakuwaje?
 
Hana hekima na busara amevikosa kabisa. He was one of my favorite politicians until recently after his stupid press!
Hekima na busara ni nyenzo muhimu kwenye uongozi.
Huwa tunamlamu Mbowe kukalia kiti muda mrefu kumbe watu wenyewe ndiyo kama hawa!!!
 
Hekima na busara ni nyenzo muhimu kwenye uongozi.
Huwa tunamlamu Mbowe kukalia kiti muda mrefu kumbe watu wenyewe ndiyo kama hawa!!!
Haahaa mbowe kafanikiwa kuijenga machawa wengi sana, nahisi hata wenyeviti wa mikoa huenda aliwapanga yeye
 
Mambo aliyoyaongea Lissu kuonyesha weaknesses kadhaa za kimfumo ndani ya Chama ni "indirect" attack kwa Mbowe.

Kama Mbowe ataamua kugombea na Lissu akashindwa (kihalali au kwa figisu), most likely Lissu ataondoka CHADEMA na chama kitapoteza mvuto wake kwa kiasi kikubwa sana

Miaka 20 ni mingi na Mh. Mbowe angekaa kando tu na kuwa mshauri wa chama.
 
I think it is too late for that. Chama kimesha pasuka
Kama Mbowe ataamua kuufuata ushauri wa watu wengi wakiwemo ndugu kutoka familia yake na kuachana na shinikizo/ushauri kutoka kwa chawaz wanaoneemeka kwa yeye kuwepo madarakani, wanaweza kusalvage something
 
Sijausoma muelekeo wa Mbowe mpaka sasa.
Mpaka sasa mwelekeo wa Mbowe ndiyo uliopelekea Lissu kuamua kugombea ile nafasi, walichofanya ni kukubaliana pasipo kuhusisha wapambe wakitaraji kutojua kwao kutauchangamsha zaidi uchaguzi sababu vile watakavyokuwa wakipambania pande hizo mbili.
Bahati mbaya upande wa Mbowe uka panic na kukosa busara na kuanza mashambulizi na dhihaka, wakashindwa kabisa kuiishi demokrasia kwa vitendo.
Ukimsikiliza vizuri alivyoongea Mbowe leo, everything tells kwamba alishaamua kugombea, ameenda mbele kwa kuihusisha familia yake kwamba imemtaka apumzike
 
Chadema inapitia kipimo Cha Imani ambacho haijawahi kukipitia, chadema ikivuka salama hili la uchaguzi wa mwaka huu...! basi nitaamini ile kauli ya "chadema ni mpango wa mungu"
 
Maneno aliyozungumza Lissu leo wakati anarudisha fomu ni mazito sana, anasema mtu aliyemleta Abdul kwake ampe pesa na akamwambia hata wengine wameshapewa pesa ndiye anagombea kuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na anamuunga mkono Mbowe kuwa mwenyekiti!

Katika hili jambo kama ni kweli ni baya sana kwa CHADEMA kwa maana chama kinapoteza imani mbele ya umma. Kwa upande mwingine kama Lissu ni muongo basi hawezi kuaminiwa kuwa kiongozi tena na wenzake ndani ya CHADEMA maana ni dhahiri atakuwa ana nia mbaya sana dhidi ya chama na hii inamaanisha safari yake ya kugombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2025 inaweza kuwa imefika mwisho.

Pia amekejeli mtindo wa mwenyekiti Mbowe ambao huwa anaombwa na wapambe kila uchaguzi kugombea.

Lissu asipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA atajaribu kuanzisha chama kingine, ataelekea ACT au ataachana na siasa kabisa.
CDM kimepitia magumu makubwa, hili la sasa wala si chochote, CDM ndio kwanza inaimarika.
 
uumbaji wa Mungu usiudhihaki. Kesho yako na wanaokuhusu huijui.
Sapoti yako kwa Mbowe imekufanya upoteze hata umakini unaposoma maoni ya watu kiasi cha kushindwa kuelewa hata lugha nyepesi katika sentensi fupi kabisa ya huyo jamaa unayemtisha! Kweli watanzania ni walewale, ni suala la maslahi kuguswa tu kila kitu kinabadilika.
 
Banana republic ni shida sana.

Huyo Abdul kaibuka tu majuzi hapa baada ya mama yake kuwa rais sasa ni bilionea anasambaza hongo za kutosha.

Mpaka dili za nchi anaenda kwenye misafara rasmi kujadiliana.

Msipojifunza kwa hii awamu ya 5&6 hamtojifunza tena katiba mpya lazima iwe ni hitaji la lazima.
Hii nchi tunahitaji zaidi katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kuliko kitu kingine chochote.

Ila kwakuwa hatujitambui tutaendelea na utaratibu huo, na utakuwa utamaduni wa kawaida kwa kila awamu inayokuja.
 
Back
Top Bottom