Dah nimeitafuta hii ngoma sijaipata.... hii ni enzi za Diamond International mwaka 1997 wanapiga Silent Inn Mwenge. Kuna ngoma ingine inaitwa Usiku wa Valentine...... katika wanamuziki ongezea jina la Adolph Mbinga
"Neema" wa Diamond Sound (Dar es Salaam Kibinda Nkoi) waimbaji wakiwa akina Alain Mulumba Kashama,Richard Mangustino,Elly Chinyama,n.k
 
Dah nimeitafuta hii ngoma sijaipata.... hii ni enzi za Diamond International mwaka 1997 wanapiga Silent Inn Mwenge. Kuna ngoma ingine inaitwa Usiku wa Valentine...... katika wanamuziki ongezea jina la Adolph Mbinga
Mkuu vuvunduli umenikumbusha Silent Inn Mwenge jamaa yangu.I remember those good days.Namkumbuka pia mkali Adolph Mbinga ambaye alikuwa mmoja wa wanamuziki wazawa (Watanzania) wachache ndani ya bendi hiyo iliyokuwa imejaa Wazaire - tangu mwaka 2001 tulianza kuwaita Wakongo - kwakweli alituwakilisha vizuri.
 
Mkuu nakumbuka niliinunua hii Album mwaka huo. Naikumbuka sababu Neema na Usiku wa Valentine ndo zilikuwa best ngoma. Na nakumbuka ndiyo ilikuwa bendi ilokuwa na wacongo wengi waipiga kama kina Defao,Koffi Olomide na wengine kipindi mtindo wa Ndombolo ya Solo ukiwa juu kabisa.
 
Haya Haya wakuu leo TBT
Kuna wimbo flani hivi kama skosei Ni wa Kenya au Uganda
Baadhi ya mashairi yake Haya hapa.
**Bum bumbaa bubumbu bumba uwiiii...
Bum bumbaa bumba bumbaa baa aiyaa**
Hilo dude ni hatar tatizo silijui jina wala muimbaji.
Huwa linagongwa sana club
Wakuu emu fanyeni mautundu tuone.
 
Wadau naomba nyimbo hizi tafadhali sana sana.
"SIKUTAKA" OG version - Unique sisters
"LEKAMBUKE" - CAZ T WA KOMBA
"NIKUPE NINI MAMA" OG version - GK
"HAYA TWENDENI WOTE"- RC X- MASS SONG
 
Raja Computer-Bumbumba
 

Huyo jamaa anaitwa E-Sir (R.I.P).

Ni moja kati ya wasanii nnaowakubali sana kutoka Kenya, ukiondoa Kalamashaka. Hiyo ngoma inaitwa Boomba Train alikuwa na Nameless humo ndani. Hiyo hapo chini.

Na ngoma nnayoikubali sana kutoka kwake ni Moss Moss. Hatari sana aisee.

Feel The Vibes.
 

Attachments

Asante ndugu,ila hii ni remix kuna Original version yake ambayo wako hao wadada peke yao,ni nzuri sana
 
Aisee. Mimi natafuta wimbo huu niliokariri mashairi yake tu. Sijui unaitwaje na sijui kaimba nani, maana nilikuwa mdogo.

Aia ia ia i, aiyaooo..aiyaoo... X2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…