Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna wimbo Wa taarabu,jina siujui na wala mwimbaji,ila umeimbwa kwa majibizano kati ya mwanamke na mwanamme ,mwanamme analalamika kuachwa na mwanamke,

Baadhi ya mistari take ni,>>>>jeraha moyoni huu mtihani umenirudia,rudi wangu mpenzi>>>

Kwa mwenye kuujua anitumie
 
Nautafuta wimbo fulani wa kikongo .
Baadhi ya maneno yake ni ..."mama baba jana kalela nkaa....mama jana baba kaleta mkaka kaleta mkaaaa oyoyooo
 
Kuna nyimbo moja ya Ray C kaimba na mkaka simjui jina hata, siyo nyimbo ya siku nyingi sana, idea ipo kama huyo bro anamuelewa Ray C ila Ray C anamchukulia poa, kuna mahala anamuambia 'wewe ni mkangafu', na kitu kama 'pesa anayoiona kwake kubwa, kwa bidada hiyo pesa ina thamani ya cheni ya kiuno' - I don't remember the lyrics well I admit..!

Niliwahi iskia radioni, jamani nimetafuta this song mpaka nimeinua mikono, maana siijui hata jina, any idea please..!
KENZY hebu tazama hapa kama utapata any ideas...!
 
Viongozi! Nisaidie jina la wimbo unaoimbwa hivi.

“Angela Angelina aah! Angela Angelina aah! Ninakuja tafuta so leo eeh! Kisha kwinta kwenta mwambao eeh! Angela Angelina aah! Angela Angelina aah! 🎶 Tu tu tu tu tuuu! Kenda kunda kinka kinkeko eeh!”
Nisaidie jina la huu wimbo! Mahadhi yanaakisi mataifa ya Zimbabwe, Afrika Kusini na Lesotho if not mistaken.
 
Wakuu msaada wimbo flani hivi wa Bongo Flavour, jina la wimbo na msanii nimesahau lakini chorus inaimbwa hivi ''Mpenzi umenikimbia wakati naumwa usiku wa manane, Ulidhani mi ntakufa ili milele tusionane, sasa yamekukuta unaomba turudiane, sina muda mchafu mimi bora niwe mjane''
Alafu pia nautafuta ''My Lady'' umeimbwa na Suma Ryda, video yako jamaa yuko na mwanamke juu ya bus wanacheza. Chorus yake inaimbwa hivi ''Yo ma lady njoo kwangu mi, njoo ucheze na mi ohhh yo ma lady njoo kwangu mi, njoo ucheze na mi
Wanaitwa Wanyamwezi Family... kama ungekuwepo mpaka sasa ningeshaupata maana nahisi nautafuta sana kuliko wewe
 
Natafuta wimbo wa Lumidee ambao upo kwenye miondoko ya reggaeton unaitwa ooh ooh (never leave you) reggaeton remix by dj kazzanova
 
Mwenye ngoma ya wamakua inaitwa 'Achemkwanda', naiomba.

Nyingine ni ya kiarabu, kiitikio kina maneno haya "habibi habibi habibi".
 
Nautafuta wimbo fulani kaimba mwanamke. Mahadhi ya wimbo ni kiumwambao,mara kihindi na kiarabu. baadhi ya maneno yake ni:

"hiiii iii iii anaisumbua akili yangu.... Mikono yake akinigusa sina haaali"

"mikono yake akinigusa,mikono yake akinigusa, mikono yake siiina haliiiii"
 
Nautafuta wimbo fulani kaimba mwanamke. Mahadhi ya wimbo ni kiumwambao,mara kihindi na kiarabu. baadhi ya maneno yake ni:

"hiiii iii iii anaisumbua akili yangu.... Mikono yake akinigusa sina haaali"

"mikono yake akinigusa,mikono yake akinigusa, mikono yake siiina haliiiii"
Wakuu nime ingia youtube nimeipata nimebahatisha baada ya kusearch sina hali
Wanaitwa Mask girls_sina hali.
 
Back
Top Bottom