Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna huu mziki unaimbwa hivi:

Tuliishi kama ndugu we kushoto mi kulia mtaani walitushidia utakapoonewa lazima nitaingilia ndivyo ilivyokuwa na Kwa upande wako pia,
Ukaniapa moyo na maneno mazur muziki sio bagamoyo ila tu nikaze msuri nisiache kusali ipo siku tuatawapiku wanaoendesha Magali.

Msaada Kwa anaeujua
 
Gloria wa Ottu jazz band
Si wazuri binadamu wengi wa hila wa OSS
Nazihitaji hizo mwenye nazo
 
Wenyewe kabisa aisee 🙏

Kuna wimbo mwingine aliimba msanii wa Mwanza kashirikiana na juma nature wanainba" popote uendako maisha magumu, wengine wanalala mitaloni, wengine wakula majalalani" kama unaufahamu naomba msaada aisee nimeukumbuka pia.

Ile record nkiipata natoa 5000!
Yan naitafuta Sana broo, pia Kuna ule wimbo jamaa animba kwa huruma kaenda kutafuta kazi mjini..baadhi ya mistari yake anamba hivi " maisha ya mjini wanasema ujanja, ukishuka kwenye ndege wanakuita kibopa, ukishuka kwenye treni wanakuita wakuja" ni wimbo wakitambo Sana nadhani miaka ya 2001
 
Kuna wimbo fulani jamaa animba kaenda mjini kutafuta kazi watu wakawa wanamshangaa nakumuona mshamba, baadhi ya mistari yake anamba hivi "maisha ya mjini wanasema ujanja, ukishuka kwenye gari wanakuita mjanja, ukishuka kwenye treni wanakuita wakuja, ukishuka kwenye ndege wanakuita kibopaaa" jamaa anaimba kwa huruma eti naomba kazi brother wimbo huo nadhani ulitoka miaka ya 2000 kwendelea .anae ufahamu anisaidie tafadhalini wadau naomba Sana,
 
Hii nyimbo inaitwa zilitiririka naitafuta sana,, nimeitafuta sana siipata. Hii audio niliipata youtube ilikuwa kama ni tangazo la tamasha
 

Attachments

Kuna wimbo unasema NATAKA NIKUJUE SANA ILI NIWE NAYO AMANI NDIPO HAYO MEMA YATAKAVYO NIJIA MIMI ni Gospel YouTube kuna watumishi waliimba chorus tu nautaka wote tafadhari. Nisaidieni.

Uliypata huu wimbo mkuu?

Nautafita pia
 
"maisha ya mjini wanasema ni ujanja, ukishuka kwenye meli wanakuita mshamba, ukishuka kwenye treni wanakuita wakuja, ukishuka kwenye basi wanakuita mshamba na ukishuka kwenye ndege wanakuita kibopaaa " hicho ni kiitikio Cha wimbo mmoja ulitoka miaka ya 2001, 2002, 2003 jamaa alienda mjini kutafuta kazi akawa anashangazwa na tabia za mjini wakawa wanamuona mshamba..anaimba kwa huruma.. mwenye ku ufahamu huu wimbo anisaidie tafadhalini wadau nimeumiss sana, wadau mwenye kufahamu huu wimbo anisaidie tafadhalini ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom