Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Samahani kwa mwenye Nyimbo za Kamanda Marehemu Mzee Kundambanda nilikuwa nazielewa sana maudhui yake maana ndo aliyokuwa anaaimba ndo yameeanza kutokea.
 
Natafuta wimbo WA parapanda arts uitwao Nyota ulitungwa wakati WA kifo cha mwl nyerere, ulitungwa na msanii Mgunga Mwamnyenyelwa, sijui yuko wapi siku hizi na kundi lake
 
Kuna wimbo cjui msanii gan na jina ila umetoka kama c 2007/2008 una maneno yanasema "acha mimi niende acha mm niende nakutakia maisha mema" n bongo flavour jamaa analalamika amemfumania demu wake
 
Kuna wimbo wa kitambo kidogo, unaitwa Birthday, kiitikio kasimama babu Ayubu.

Mahudhui ya wimbo ni kuwa siku hiyo ya Birthday aligonganisha madem zake wawili, ilitokea mara baada ya MC kusema ***** mheshimiwa aje kula keki, mara ghafla madem wawili wakainuka...
 
Wakuu naomba mwenye wimbo wa bushoke nafikiri unaitwa maria amepiga kama charanga hivi.
 
Utawezaje kutupenda wawili, namimi nami najua unamoyo mmoja, lazima utadanganya mmoja, kama yeye au mimi sijui!
Jina la wimbo hata siufahamu..
 
Mimi natafuta wimbo mmoja ulikuwa unaimbwa sana kwenye kipindi cha "Tuimbe sote" kilichokuwa kinarushwa na RTD wakati ule. Wimbo huo ulikuwa unaitwa "MTAMA WA BABA".
Wimbo huu kama nakumbuka vizuri uliimbwa na vijana wa shule moja hivi ya Tanga. Kama kuna mtu yuko nao naomba auweke hapa tafadhali.
 
Kuna sebene fulani wanapenda kuipiga kwenye maharusi siijui jina
 
Kuna wimbo wa kikongo miaka ya 90s siukumbuki jina ila nakumbuka sehem ya rap yake inayosema "tala mama kiddekude eee kiddekude"
 
Back
Top Bottom