Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Hapa mwisho. Sitasahau huu wimbo nilipousikiliza nikipanda ndege kuelekea nyumbani Tanzania wakati huo
 
Mnisaidie na jinsi ya kudown load nyimbo zenye format ya video zinazopandishwa humu
 
Nimefanya mema mengi kupita uwezo wangu,nimekubeba lakini haubebeki...uzalendo umenishinda...by muumin mwinjuma jina LA wimbo silijui wakuu
 
Kuna nyimbo za dada mmoja wa Kenya sijui alikuwa anaitwa nani nyimbo ya chakacha yanilisha chakacha yanivisha alikua na albam kabisa naitafuta sana
 
"Watu wanasema nisikufuateee,tena ikibidi nisikukumbuuuke,thamani ya kitu ajuaye mwenye chakee,niacheni chozi linidondoke.Nikikumbuka iyo sura yaaake ...."

Wakuu anayeukumbuka huo wimbo naomba anitajie hata jina la wimbo au aliyenao aniwekee hapa please .

Ni wimbo aliouimba Kwa sauti zilizolangiliwa vizuuuuuurii sana.

Msaada Please,
Pasha
 
Minaomba mnisaidie wimbo wa adele helo kila nikipakua hauiingii kabsa
 
peace and love mwimbaji ana sauti kama ya lucky dube
 
Natafuta wimbo wa dini umeimbwa Na Kinondoni revival kwaya, wa kitambo kidogo unaitwa "wrong number shetani kwangu".

Pia kuna wimbo mwingine umeimbwa Na Nioth Prophetical singers unaitwa " Mapambazuko" upo kwenye album yao ya "Unangoja nini".
Jamani... Mnikumbuke..
Kuna wimbo wa kitambo kidogo, unaitwa Birthday, kiitikio kasimama babu Ayubu.

Mahudhui ya wimbo ni kuwa siku hiyo ya Birthday aligonganisha madem zake wawili, ilitokea mara baada ya MC kusema ***** mheshimiwa aje kula keki, mara ghafla madem wawili wakainuka...
Na hapa pia
 
Mi natafuta wimbo wa Bushoke
siujui jina ila maneno yake ndani yanasema"kama ulikua hutaki ishi nami kwani hukuneleeza mapema..........nk....
 
URITHI GANI TUNAWAACHIA WATOTO WETU. KWAYA YA MOYO MT. WA YESU SINGIDA. NIKIPATA VIDEO YAKE YOTE NITAFURAHI SANA
 
Back
Top Bottom