Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Hizi nyimbo nazitafuta sana.
1. Www.mapenzi abdul misambano akiwa na tam tam ikibidi nipate nyimbo zao zote walizoimba akiwemo sekedia
2. Picco mapenzi hamna tena
 
Kuna album moja ya kwaya ya KKKT nadhani kutoka Arusha inaitwa "Shangilieni"ilikuwa kali sana, itakuwa poa sana kama nitapata nyimbo zake.
 
Kuna album moja ya kwaya ya KKKT nadhani kutoka Arusha inaitwa "Shangilieni"ilikuwa kali sana, itakuwa poa sana kama nitapata nyimbo zake.
Ilikua kali kweli nyimbo kama nakulilia mwokozi,mwana mpotevu na dunia hii ni favourable kwangu,me ninayo full but niko far na home,but nenda kasech yutubu zipo kule japo hazna quality
 
Naomba mwenye wimbo wa Q chillah-nimeridhika naye anisaidie.Nimeutafuta wimbo huu bila mafanikio.
 
Kuna wimbo una maneno.......kitendawili mwanangu mie kanigeuka nataka mwanza aah nikale e sangara........nautafuta.....natanguliza shukrani
 
Habari Wanajukwaa; Kuna Nyimbo sina Hakika na Jina Lake, ila Ina mashairi yanasema;

Rhoda Mpenzi wangu Rhoda,
Umasikini Sikuomba Kwa Mungu,
Umasikini wala Si Kilema,
Wakusema Nitakufa Nacho,
Siku moja Nitakua Tajiri,
Nitanunua Gari la Benzi,
Kama Lile Nililoona,
Mlangoni Kwa Kina Rhoda

Mwenye Kuijua Hiyo nyimbo tafadhali.
 
Natafuta wimbo unaitwa Proposition uliimbwa na group linaitwa Thug City. Shida wimbo haupatikani online.
 
°Hai-make sense hai-make dala hiyo,,,,,,,'yani kama hakupi mchongo siyo mchizi huyo,,,,,'anang'ata na kupuliza ujue ni panya........!





*anaemfaha jina la mwenye wimbo unaitwaje naomba anifahamishe
 
Salamu nishamuachiaga GENTAMYCINE na ndugu zake wa Butiama akiwemo Cognizant


Ndugu zangu wapenda Burudani ya muziki hasa muziki wa Bongofleva wa miaka ya nyuma (Old skool).

Kuna wimbo unaitwa "NIPE NAFASI" umeimbwa na msanii TID akiwa amemshirikisha Fid Q,huu wimbo nimejaribu kuutafuta kwenye kila Platform ya kuuzia miziki lakini sijafanikiwa kuupata,sijaelewa shida ni nini kiukweli hadi huo wimbo kukosekana kwenye Platform hizo!.


Naomba kama kuna member yeyote ambaye anao huo wimbo au anaweza kuupata popote anisaidie kunitumia hapa maana ninaupenda sana na unanikumbusha mambo mengi sana!.

Nawasilisha!
 
Kuna wimbo fulani ulikuwa unatumiwa katika kipindi cha njia panda cha Clouds F.m Radio miaka ya 2002 -4
Unaitwa maisha ni mapambano....naombeni mwenye nao
 
Back
Top Bottom