Ni zawadi gani ukipewa na mpenzi wako unafurahi sana? Naombeni mnijuze

Dadaetu umependa haswa!!

Anyway kama anafatilia mpira na unajua team yake mnunulie jezi lakini kwasasa misimu imeisha subiri msimu uanze mnunulie jezi ya team yake na ukitaka afurahi zaidi print jina lake mgongoni na umfanyie suprice hakika atajiona dunia yote yake

Kama hapendi boli mnunulie nguo nzuri sana jinz,Shati,T-Shirt kali sana ila ukitaka kuupiga mwingi zaidi mnunulie Boksa kila akivaa atakukumbuka NIAMINI

Ikishindikana mnunulie gadget kama Saa au cheni

Ikishindikana mnunulie viatu,Chagua buti kali kama timber black, au simpo au Air jordan OG kama uchumi unaruhusu
 
walau umenielewa ninachohitaji,, thanks 😊
Swali lako ni gumu kwao najibu kama mwakilishi wa wanaume 😁😁😁 men are from mars women are from venus, zawadi ni sign ya caring.....kwa nature sasa caring ni sifa ya mwanamke sio mwanaume, men needs appreciation, trust, nk (sijui umenielewa, ndio maana ukionesha mwanaume kumjali saanaaa anakaa mbali na wewe sio nature yao)
 
nimekuelewa kipenzi,,,
 
anipikie chakula nikipendacho..... baada ya hapo tulewe afu tudinyane😂

nimefikiria wee nimeishia hapo.... kweli wanaume hatuna mambo mengi😂
Wakati mi ukiniuliza nitataja....saa, hereni, blacelet, cheni ya kiuno, pochi, viatu , perfume, oooh kabla ya saa kuna pesa, chupa ya wine alooo ni vingi😁
 
ushauri mzuri sana huu,, barikiwa sana mkuu🙏🏼😊
 
sawa,, Asante kwa ushauri wako mzurii 😊🤗
 
There you are ✌️ umuongeze na space hapo sio kumbana kama umemzaa wewe😁
 
Inategemea na level of appreciation ulio nayo. Mfano mimi wife anaweza leta boxer na vest nikafurahi sana maana sina muda wakuanza kujitafutia boxer madukani anaweza kuta toleo jipya mm hata sijui kama zimetoka mpya, sasa mwingine akipelekewa boxer anaona sio zawadi kwahyo tunatofautiana hapo. Mm kitu kingine ni kutoka na mwanamke wangu yaani yeye atafute sehemu nzuri iliotulia anipige mtoko mmoja wa maana naenjoy sana asee. Ila mwisho wa yote zawadi kubwa kwangu ni yeye kunipa penzi kwa ratiba yenye mpangilio wa kimahaba sio kunikurupusha kama anataka kuanzisha vita
 
ushauri mzuri sana huu,,,Asante 😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…