Nifahamishe kituo cha watoto yatima chenye uhitaji mkubwa sana

Nifahamishe kituo cha watoto yatima chenye uhitaji mkubwa sana

Mawazo yangu kutokana na baadhi ya mawazo ya wana jukwaa.

Lengo la kusaidia vituo vya watoto yatima ni zuri kabisa ila shida ni kwamba watu wamegeuza vituo vya kulelea mayatima kama chanzo chao cha maokoto.
Na incase zikatokea fursa za watoto mayatima kufadhiliwa au kusomeshwa basi hupeleka watoto wao instead of walengwa.

Nini cha kushauri
Kuna watu wenye uhitaji ambao hawapo kabisa katika mzunguko wako wa maisha jaribu kuwaangaza hao kwa nia ya dhati kama vile wagonjwa waliotelekezwa mahospitalini na watoto wa mitaani wasio na familia.

Suala la kusaidia watu wa ndani ya familia usilifanye kama hujaombwa msaada zaidi ni utazua chuki na husda ndani ya familia ionekane ni kama umewadharau.

Key point ni HUSDA HUSDA HUSDA......
 
Anza na ndugu zako na wanaokuzunguka wenye mahitaji.

Charity begin at home.
Unajuaje kama hajafanya hayo kwa nduguze?

Na hata kama hajafanya, huwezi jua kilichomsukuma kutaka kufanya hayo anayotaka kuyafanya kwa hao watoto yatima!

Ujue, hata watoto yatima na wa "mitaani" nao ni watoto.

Samahani kama nimekukwaza.
 
Habari ya wakati huu wakuu. Ninaomba msaada wa taarifa ya kituo chochote cha kulelea watoto yatima ama watoto walio katika mazingira magumu ambacho kiuhalisia kina hali ngumu ya kimahitaji ya kawaida.

Kituo kiwepo Dar es salaam na nitaomba kama utaweza unisaidie mahali hasa kinapopatikana na mawasiliano ya namna ya kufika.

Asante.
👏👏👏
 
Kwani unajuaje hali ya mtu na familia yake mpaka umshauri aisaidie kwanza familia yake.

Kuna wengine wameumbwa matajiri wao, Vizazi vyao na kila kitu kiwahusucho.
Si mpaka mtu awe tajiri ndiyo anaweza kutoa msaada/sadaka. Hata akitoa pakiti moja ya chumvi nao ni msaada pia, hasa kama atafanya hivyo kwa kusukumwa na upendo.

Miaka ya nyuma, kuna bibi mmoja mjane alitoa msaada wa sh 200/= kwenye kituo kimoja cha watoto jijini Mwanza.

Uongozi wa hicho kituo haukudharau sadaka ya huyo mjane. Waliitumia hiyo 200/= kununulia kipande cha sabuni watoto wakatumia kunawia mikono wakati wa kula.

Kuna watu wana marundo ya nguo za watoto amabazo hazitatumiwa tena na watoto wao. Wanaweza wakazinkusanya na kiziwasilisha kwenye vituo vyenye watoto wahitaji.
 
Amini nakwambia hii threads si kwa ajili yangu pekee, wengine wengi watasauidiwa na ndio maana tumeomba kufahamu sehemu yenye uhitaji hasa. Kwamba kusaidia ama kuungana mkono katika masuala ya kijamii ni kutafuta sifa?
Mkuu, nia yako ni njema. Ni jambo jema limpendezalo Mungu. Songa mbele.
 
Ukisoma comments ndio utaelewa ile takwimu ya Tanzania kua nchi ambayo wananchi wake hawana furaha... mtu akikosa furaha anakua na negativity muda wote, akili inaganda, kila kitu kwake kinakua kibaya, anakua ana roho mbaya.

Inahuzunisha
 
Mawazo yangu kutokana na baadhi ya mawazo ya wana jukwaa.

Lengo la kusaidia vituo vya watoto yatima ni zuri kabisa ila shida ni kwamba watu wamegeuza vituo vya kulelea mayatima kama chanzo chao cha maokoto.
Na incase zikatokea fursa za watoto mayatima kufadhiliwa au kusomeshwa basi hupeleka watoto wao instead of walengwa.

Nini cha kushauri
Kuna watu wenye uhitaji ambao hawapo kabisa katika mzunguko wako wa maisha jaribu kuwaangaza hao kwa nia ya dhati kama vile wagonjwa waliotelekezwa mahospitalini na watoto wa mitaani wasio na familia.

Suala la kusaidia watu wa ndani ya familia usilifanye kama hujaombwa msaada zaidi ni utazua chuki na husda ndani ya familia ionekane ni kama umewadharau.

Key point ni HUSDA HUSDA HUSDA......
Una hoja ya msingi. Kuna wengine wanakwenda kwenye vituo kutoa misaada huku familia zao au mtaani kwao kukiwa na watu wenye hali mbaya sana. Wakati mwingine baadhi ya watoa misaada huenda vituo vya yatima kutoa misaada lakini lengo kubwa likiwa ni kupiga picha za kuanika kwenye social media. NB: sihusishi haya na mwanzisha thread kwani anaweza kuwa na lengo zuri sana.
 
MIHAYO Morogoro Mazimbu,tena wapo na wenye mtindio wa akili.
 
Back
Top Bottom