Wazo Zuri Sana mkuu..
Kwani 99% ya vituo vya kulea watoto yatima ni wapigaji..
99% wamefungua vituo kwa ajili ya maslahi yao binafsi...
Wazo Zuri Sana mkuu..
Kwani 99% ya vituo vya kulea watoto yatima ni wapigaji..
99% wamefungua vituo kwa ajili ya maslahi yao binafsi...
99% ni wapigaji? Mkuu una uhakika na usemalo? Unataka uniambie Serikali imelala kiasi hicho?
Kama huo ndiyo mtazamo uliopo kwa Watanzania wengi, basi sitashangaa tena kufahamu kuwa vituo vingi vinawategemea wafadhili wa nje(Wazungu) kwa kila kitu, mpaka chakula cha watoto.
Ni kweli kuna vituo vya "kinchongo", lakini siamini kama ni vingi kwa kiwango hicho.
Ni kweli kuna hayo katika baadhi ya vituo, lakini mimi naona bado ni afadhali kuliko maisha ya mtaani!
Kituoni, mtoto ana uhakika wa kulala ndani ya jengo hata kama ni sakafuni kuliko kulala barazani mjini!
Kituoni, kuna uhakika wa kula kila siku hata kama si mlo mzuri sana kuliko mitaani ambako wasipifanikiwa kupata kwa kuombaomba, huishia kula vya kuokota majalalani!
Mtoto akiwa kituoni, ni rahisi zaidi kuepushwa kujiingiza kwenye tabia hatarishi kama uvutaji fundi na utumiaji wa madawa ya kulevya!
Kituoni kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kusoma kuliko akiwa mtaani!
Ukiona mtoto wa mtaani kakubali kukaa kituoni, ujue na yeye kagundua utofauti. Kunaweza kujazwa hakiwahudumii vizuri sana lakini kina uafafhali kuliko kuhangaika maishani. Mkuu, hao watoto nao wana akili ujue! Wakiona kituo "kinazongua", hawakai.
Nisemalo ni hili, HATA KAMA KUNA VITUO VYA KIMCHONGO, BADO NI AFADHALI KULIKO VISINGEKUWEPO.
Ubinafsi wa waliovianzisha hivyo vituo vina msaada zaidi kuliko upendo wa wengi ambao hawajauweka katika vitendo! Vituo vya watoto vinastahili kusaidiwa.