99% ni wapigaji? Mkuu una uhakika na usemalo? Unataka uniambie Serikali imelala kiasi hicho?
Kama huo ndiyo mtazamo uliopo kwa Watanzania wengi, basi sitashangaa tena kufahamu kuwa vituo vingi vinawategemea wafadhili wa nje(Wazungu) kwa kila kitu, mpaka chakula cha watoto.
Ni kweli kuna vituo vya "kinchongo", lakini siamini kama ni vingi kwa kiwango hicho.
Ni kweli kuna hayo katika baadhi ya vituo, lakini mimi naona bado ni afadhali kuliko maisha ya mtaani!
Kituoni, mtoto ana uhakika wa kulala ndani ya jengo hata kama ni sakafuni kuliko kulala barazani mjini!
Kituoni, kuna uhakika wa kula kila siku hata kama si mlo mzuri sana kuliko mitaani ambako wasipifanikiwa kupata kwa kuombaomba, huishia kula vya kuokota majalalani!
Mtoto akiwa kituoni, ni rahisi zaidi kuepushwa kujiingiza kwenye tabia hatarishi kama uvutaji fundi na utumiaji wa madawa ya kulevya!
Kituoni kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kusoma kuliko akiwa mtaani!
Ukiona mtoto wa mtaani kakubali kukaa kituoni, ujue na yeye kagundua utofauti. Kunaweza kujazwa hakiwahudumii vizuri sana lakini kina uafafhali kuliko kuhangaika maishani. Mkuu, hao watoto nao wana akili ujue! Wakiona kituo "kinazongua", hawakai.
Nisemalo ni hili, HATA KAMA KUNA VITUO VYA KIMCHONGO, BADO NI AFADHALI KULIKO VISINGEKUWEPO.
Ubinafsi wa waliovianzisha hivyo vituo vina msaada zaidi kuliko upendo wa wengi ambao hawajauweka katika vitendo! Vituo vya watoto vinastahili kusaidiwa.
Mkuu elewa maana ya neno
wapigaji
Watu wengi waliofunguo hivyo vituo wana maslahi binafsi..
Yupo jamaa mmoja naficha code zake kwa maslahi mapana ya utu na ubinadamu.
Ila anamiliki kituo cha kulelea watoto yatima,,lakini anayoyafanya sisi ndy tunaoyajuwa..
-- pesa za misaada anayopata anafanya maendeleo yake binafsi .mfano,
*Kujenga nyumba zake binafsi,,kununuwa Magari ,,mashamba nk huku walengwa(watoto yatima) wakiambulia patupu.
-- anapewa misaada ya madawa ya hospital lakini anaishia kuuza kwenye pharmacy binafsi na pesa kufanya mambo yake.
-- Kuna wafadhili wanasomesha watoto hewa kwa mgongo wa majina ya watoto yatima.
Mfano:
Mfadhili anahitaji majina ya watoto awasomeshe shule za english medium lakini majina yanayokwenda ni ya wajukuu zake na watoto wa ndugu zake, huku mfadhili anadhani anasomesha watoto yatima kumbe anasomesha watoto ambao wazazi wao wapo na sio yatima.
Tajiri analetewa majina ya watoto ambao sio yatima anasomesha bila kujuwa watoto walengwa ambao ni yatima wanasoma
KAYUMBA
-- amekuwa akiuza Michele /sukari/nk ambavyo anapewa kama misaada kwa mgongo wa yatima.
Ninaposema wapigaji namaanisha...
Serikali inapaswa iangalie kwa makini eneo hili la watoto yatima.