Albert Einstein alipokuwa mvulana mdogo akiwa shuleni, uwezo wake ulikuwa mbovu kiasi kwamba mwalimu alifikia hatua ya kumuabia aache shule kwani hawezi kuja kufanikisha chochote. Lakini ndiye alikuja kuwa winner wa nobel prize 1921, tuzo za heshima kubwa sana duniani.
Thomas Edison mwanasayansi aliyegundua bulb, kipindi ni mvulana mdogo akiwa shuleni uwezo wake darasani ulikuwa mbovu kiasi kwamba mwalimu wake akamuambia ''wewe ni mjinga sana na huwezi ukaelewa chochote'', Siku moja dogo kipindi anatoka shuleni, akamuambia mama yake "mama mwalimu kanipatia karatasi hii, lakini kaniambia usome ni wewe pekee unapaswa kusoma, kwani barua hio inasemaje mama?"
Mama alibubujikwa na machozi na akasoma ile karatasi kwa sauti "mtoto wako ni genius sana, hii shule ni ndogo sana kwake na hakuna walimu wanaoweza kumfundisha, tafadhali mfundishe mwanao mwenyewe."
Miaka mingi baadae baada ya mama yake na Thomas Edison kufariki na Edison amekwisha kuwa mwanasayansi mkubwa wa karne aliweza kukuta ile barua kwenye kabati la nguo la mama yake, kumbe kile kikaratasi kiliandikwa "mtoto wako ana upungufu wa akili, hatuwezi kumuacha aendelee na shule yetu, tumemuachisha shule", kwa lugha ya kiingereza mentally deficiency tukitafsiri ni mtu mwenye upungufu wa akili, wengine huku wanasema dishi limecheza, sasa you can imagine Edison uwezo wake ulivyokuwa mdogo darasani.
Baadae Edison aliandika kwenye diary yake “Thomas A. Edison was a mentally deficient child whose mother turned him into the genius of the century.” --
Akiwa na maana kwamba "Thomas A. Edison alikuwa mtoto mwenye upungufu wa kiakili ambaye mama yake alimgeuza kuwa genius wa karne hii."
Hio tunaita ni nguvu ya maneno, maneno ya mama yalimfanya mtoto awe mgunduzi wa bulb ambayo tunaitumia leo, mkuu jaribu kukaa karibu na watoto wako, wapende, wajali, wape moyo, usiwachape hovyo na kuwaita wajinga ukifikiri unawajenga wakati unawaua ndani kwa ndani, ndio watoto wako Mungu kakupa hakuna wengine, mbeleni wanaweza kuja kufanya maajabu kama Edison 🙂