Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Mtoto anatengenezwa siku 1000 za mwanzo ukikosea hapo tegemea muujiza mtoto kuwa kipanga, sijasema hawez ila ni nadra sana.

Swali la msingi, unawalisha wanao ugali?
 
Maneno ya busara sana haya. Hasa hili la kuwachapa watoto na kuwatukana ''jinga hili, shuleni halijui kitu''. Halafu unakuta mzazi anajaribu kushindanisha mtoto wake na wengine, eti ni lazima ushike namba moja. Busara ni kumpenda mtoto, kutokum-overwork na kumsaidia kuelewa na siyo kushindana kimasomo.
 
Akili hufuata mkondo,kama wazazi bichwa maji,likewise kwa watoto,hakuna dawa hapo ulikosea kuchagua mke kilaza kwa kuangalia shape badala ya kichwa
Sioo kweliii mkuuu nakupinga hiloo ndoaa pekee ndio inafwata ukoo wenh watototo akili zaoo na jinsi ta kuwatengeneza wawe vichwa ngoja nkakojoe narudi
 
Mama ni wa la saba tu, baba ana diploma ya IT, na anadigrii ya uongozi na maendeleo ya jamii, pia anacheti ya veta ya udereva. Huyo bado sio, hata kwao baba ndugu zake ni wasomi waziristan tu hata mzazi wa baba naye msomi mzuri tu.
Kuishia darasa la saba hakumaanishi mama yao hana akili. Aidha, wewe kuwa na digrii hakumainishi kuwa una akili kuliko mke wako. Kuwachapa wakishindwa kupata maksi unazotaka wewe hakusaidii isipokuwa kunawatia uoga kiasi cha kutofanya vizuri. Waonyeshe upendo na uwatie moyo kila wakifanya vibaya. Angalia wanapenda vitu gani ( hata upishi ni fani nzuri) na uwape moyo wajiendeleze huko. Wewe ni mtu wa IT, washirikishe katika mambo unayofanya. Badala ya kufanya mambo ya darasani kuwa ni kigezo pekee wekeza nguvu zaidi kuwa wanakuwa na tabia njema na upendo kwa binadamu wengine. Mwisho, ujue kuwa kuna wanaoitwa late bloomers. Unaweza kushangaa watakavyokuwa vipanga wakipata fani wanayoipenda na kuimudu.

Amandla...
 
usiachee kuwaombee mkuu peleka kwa maombi m nilikuwa na mmmoja mzuri sana gafla akabadilika matokeo nkasimama na Mungu karudi kwenye mstariioii wafundishe piaa na wao jinsi ya kufanya maombiiii

nilikwenda mwakajana shule moja maeneo ya goba kufanya maombi ya la sabaaa ndugu walikuwa wanafanya mtihan hamster akaomba ntafute past akakubali alipipga maombi kaka walidondoka watotooo cha mtoto wengine wanasema sitokii umekuja kufanya nn kuchukua akili zaooo so wengine sioo wanapenda n mapepoo mkuu watoto wengine aako kama agent wa shetani mashulen so pamabana na maombi na wajue kujimbea

wafunike kwa damu ya Yesu
 
Mtoto anatengenezwa siku 1000 za mwanzo ukikosea hapo tegemea muujiza mtoto kuwa kipanga, sijasema hawez ila ni nadra sana.

Swali la msingi, unawalisha wanao ugali?
Hii kitu bila supplement ya heavy protine ya maziwa na samaki kwisha habari ya watoto kuwa na akili. tegemea kuwa na makuli na wasukuma mikokoteni wenye manguvu.
 
Ni kweli mkuu, mtoto akishakuwa kwenye hofu, hawezi kujiamini tena, hivyo itampelekea kutojiamini kwenye kila jambo.
 
Mkuu watakuwaje na akili nyingi wakati wazazi wenyewe akili zenu za kuungaunga kwa gundi!
 
Ukitaka kuwa na watoto vipanga darasani hakikisha unaoa mke kipanga haswa.Yaani mkeo awe mwerevu Kweli Kweli.

Then hakikisha watoto wako hawali ugali kbsa coz Ni chakula kinachodumaza akili.
Kwenye ugali mkuu umedanganya! Kwenye mahindi kuna co-enzyme ya muhimu sana katika kuimarisha akili kama ulikuwa hujui! Sisi tuliokuwa tunakamata nguna kwa samaki na maziwa pembeni darasani tulikuwa njema sana!
 
Usiwalazimishe watoto kuwa na ufaulu mkubwa wa darasani bali aangalia vipaji vyao vipo wapi. Then wasaidie kufikia kiwango cha juu kuweza kuzzitumia vizuri vipaji vyao. Ufaulu mkubwa tu wa darasani siyo kigezi cha watoto kufanikiwa kupambana na mazingira na kufaulu maisha. Bill gate alikuwa kilaza darasani
 
Siyo Kwa damu ya kibongo....bila fimbo Maji hayapandi ni wachache mno eatapanda
 
Acha kujidanganya wewe. Kupata A ni kipimo kizuri na cha kuaminika kwa mtoto. Sifuri ni dalili ya ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…