Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Akili ya darsani inategemea mazingira ya nje zaidi na sio inborn.
Mkuu yote yanachangia ila kwenye zile peformance za juu ni lazma mtoto awe karithi kwa mzazi.

Brother wangu mmoja alikuwa na msemo wake "kusoma ni kipaji ila kufaulu ni tabia ya mtu. "

Kwa hiyo kuna watu wanafaulu kirahisi na wengine ni kwa msuli mzito sana. DNA inahusika mkuu ndio maana hata Albert Einstein alizaliwa na mwanamke hatari kichwani
 
Watakuwa na akili kubwa, hawataki kukaririshwa mawazo ya watu; wafundishe mambo ya ufundi, kama kutengeneza treni, magari, ndege n.k
Watakuwa wavumbuzi wa baadaye.
 
Ujue tu kuna washenzi wanacheza na nyota za watu. Kwanza waweke watoto wako sawa, tembelea wazee wenye busara wakuelekeze.
 
Wabongo tunadanganyw sana na zile A na Division 1 kwamba ndio akili zenyewe. Akili sio kupata A mtoto anaweza pata zero darasana lakini akawa na akili nyingi sana za kufanya mambo makubwa sana.Akili ni pale mind ya mtoto inapo weza kutafasiri au kuchakata yale masomo na kufanya vitu vikibwa sana.

Bahati mbaya tulienda kusomea A na kushindana kutafuta Division ndio maana tuko hapa tulipo.

Shida ni pale tunapo ingizwa chaka na kulipa mamilion ya pesa ili watoto wapate A na Waongee Kingereza.

Ndio maana tuna import kila kitu make tumewekeza sana tena mno kutafuta A na Division One.

Kama una mtoto ambaye ana think beyond darasani hio ndio akili yenyewe, kama anasoma na unaona anafanyia kazi anayo yasoma hio ndio akili. Ila kama ni bingwa wa kupata A hizo ni kukariri tu, sana wanakaririshwa wajibu papper wapate A
 
Nini maana ya akili? tuna kwama sana, Akili kila mtu anazaliwa nazo, hakuna kituo wala shule ya ku inject akili kwa watoto, pale shuleni ni vituo vya kuwafanya zile mind zao sasa au akili walizo nazo ziweze kufikiria vitu, mfano, kwa nini atupe jiwe juu then irudi chini, kwa nini Maeneo yasio kuwa na miti. mingi au misitu hayapati mvua nyingi,

Nyie mnaingizwa chaka na zile A na mtoto kuongea Kingereza kwamba ndio akili? A haiwezi kuwa akili. Ndio maana Vyuo vikuu wamejaa wasomi ambao hawawezi unda hata mashine ya kutengenezea misumari, sabanu ni mawazo kama haya.
Sizitaki mbichi hizi. Wewe andika magazeti yako lakini ukweli ni kwamba hata wewe mwenyewe hauwezi kumpeleka mwanao shule ya kata wakati unao uwezo wa kumpeleka FEZA.
 
Tulikosea tangu mwanzo kuwa na elimu ya kuoata A na Division na kukaririshwa past paper mwanzo mwisho.

Tukaachana na kuwa tuna tuna shughurisha akili zetu ziwaze beyond vile vitabu. So tuka stick kwenye vile vile vitabu, types or rocks, Nile river, na kadhalika.
 
Tulikosea tangu mwanzo kuwa na elimu ya kuoata A na Division na kukaririshwa past paper mwanzo mwisho.

Tukaachana na kuwa tuna tuna shughurisha akili zetu ziwaze beyond vile vitabu. So tuka stick kwenye vile vile vitabu, types or rocks, Nile river, na kadhalika.
OP
 
Wakuu mna maneno makali 😁

Ila ukweli ni kuwa mzazi mwenyewe anatamani kujiona katika peformance ya watoto wake shuleni. Japo ni muhimu kuwakazia ili wasifeli lakini ni vizuri pia kuwasoma watoto wako wapo vizuri kwenye nini kingine zaidi ya class

Jifunze kuwapenda zaidi na usiwakatie tamaa lakini pia usiache kuwaongoza katika vitu vinavyowafaa zaidi
 
Akili za kuzaliwa nazo huanza kupotea siku ile mtoto anakanyaga shule kwa mara ya kwanza. Pale ndio akili za asili huanza kuondoka, mtoto huanza kuforciwa vitu tofauti kabisa.kukaririshwa na kiingiziwa vitu tofauti na hapo swala Drop out likawa linatokea kwa walio kuwa wanaona hapana
 
Back
Top Bottom