Nikasome degree nyingine au nifungue biashara?

Nikasome degree nyingine au nifungue biashara?

Kama umepata business inayoeleweka chukya pesa fanya biashara na pia kama unaweza kuifanya bila kuacha kazi itakuwa nzuri zaidi.

Usikope ili ujenge nyumba tafadhali.

Pia kama hiyo masters unaenda kusoma ukiwa na connection kuwa ukimaliza utapata chaka la maana sawa ila sio kuisoma ndio uanze kutafuta mchongo. Siku hizi bila connection kutoboa ni ngumu.

Chukua loan, fanya biashara huku ukiendelea na kazi. Kama utafanikiwa katika biashara na kazi unayo utafurahia maisha.
Asante, siendi kuchukua master's nilitaka nisome degree nyingine alafu nisubiri kufanyiwa re-categorization business ndio naiwaza zaidi mkuu.
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu Kwa kijana wenu hapa, Mimi ni Mwalimu wa physics na chemistry nipo nkasi-rukwa, form six nilipata division two PCB point 11, nipo kwenye kufundisha Mwaka wa pili Sasa, naona ni wakati wa kuwaza nje ya box.

Kwenye Ili Chaka nimekuta watu wapo zaidi ya miaka 10 lakini vilio ni vingi sana, nadhani nisipofanya maamuzi sasahivi nitaenda kua kama wao tu, hakuna kitakachoharibika,

Nina-acces ya kukopa million 15/20 NMB/HAZINA. Japo za hazina kuzipata ni ngumu mno, nawaza vitu viwili nikasome au nitafute biashara nifanye?

Course ambayo nimeplan kwenda kusoma ni bachelor degree in business statistics and economics nadhani kwamba nikimaliza hii naweza fukuzia na kufanyiwa re-categorization.

Vipi wakuu niendelee kushika chaki huku nikifungua biashara? Au niende kusoma TU?.
Kwani ukifanikiwa kusoma mshahara wako utafikia 20million?
Start business.
 
USHAURI WANGU

Kama una access ya kupata milion 15/20 achana na habari za kusoma kwanza, huko Nkasi Rukwa kilimo cha mahindi kinastawi sana, na biashara ya mazao pale Boda ya Tunduma ni biashara nzuri unaweza anza kidogo kidogo, au shuka bondeni kalime mpunga kule kilyamatundu-kituku kuna kilimo cha mpunga watu wanapiga hela, au wekeza kwenye uvuvi- samaki & dagaa wanatoka Rukwa kwenda mpaka kongo. kila kitu ni kujifunza na kujaribu. Ubarikiwe sana
 
Mi nakushauri nenda kasome kama umri unaruhusu kikubwa nilichogundua kazi ya ualimu huipend ss cha msingi n bora usome na ufanye kazi unayoipenda then uje ukope badae ufanye biashara i think utaishi kwa amani coz ww uko kwenye system ukienda kusoma hakuna kitu utapoteza tofaut ungekuwa huna ajira ndo ningesema ukienda kusoma utapoteza fanya ivo mdogo wang ualimu ni jau sn huwez toboa
 
Kwa PCB yako kama utarudi shule nakushauri kasome kozi za afya.

Hasa hasa Udaktari.

Umuhimu wa daktari haujawai na hautawai kuisha duniani
nakazia nakazia nakazia, dogo kama yupo njema kichwani achukue ushauri wako, kuna mwana alisoma bachelor of education(biology and chemistry), akafanya kazi mwaka tu akaona hamna anachokifanya, akarudi akasoma madicine, kwa sasa yupo botswana anakula dolari za maana. mwingine aliamua kwenda jeshini kwa sasa yupo njema tu.
 
Unachohitaji ni ujuzi..na wala siyo degree. Ni Bahati mbaya Sana kwamba degree zetu nyingi na mfumo wa ufundishaji unaishia kutoa maarifa na wala siyo ujuzi.

Mfano unaweza ukasomea Human resources management unaishia kuwa na maarifa, lakini zile ule ujuzi unaohitaji katika hii fani Kwa mfano; jinsi ya kuamsha ari ya ufanyaji kazi, jinsi ya kukuza na kutumia ujuzi wa watu wakiwa makzini ukakosa.


So tafuata fani unayoipenda jifunze maarifa na ujuzi katika hiyo fani na uwe mbobevu, kiasi kwamba watu watakuwa wanakutafuta wewe na siyo wewe kuwatafuta, Kwa Sababubu utakuwa tofauti na wengine, pia utakuwa unatatua changamoto za watu in a best way.

Mfano Kwa fani yako unaweza ukaongeza ujuzi na maarifa kwenye pharmacy Kwa lengo kwamba siku moja uje kuwa na duka lako la madawa. Kama ni hivyo usiishie hapo Tu pia;
-jifunze kuendesha na kusimiamia biashara
-jifunze kuwa mwajiri Bora n.k

I hope hayo yatakusaidie.
 
Maisha hayarudi nyuma. Achana na mawazo ya kusoma. Songa mbele. Kopa ujenge nyumba ya kuishi.
Kujenga hapana ni kujitafutia umasikini zaidi.

Mimi nadhani akope pesa kidogo sana kama milioni 5 then aingize kwenye biashara, mfano afungue duka.la kuuza simu na vifaa vidogo vidogo vya simu hapo anunue hizo simu (nyingi ziwe za kichina button) na vifaa vidogo vidogo vya simu eg. Earphones, charger na screen protector kutoka Kariakoo (Dar)

Hapo ahakikishemtaji anaotumia ni milioni 2 na nusu tu iyo nyingine ataongezea taratibu kwenye hiyo biashara. Ikichanganya aendeleee na biashara huku anafungua nyingine mf. Kuleta mazao Dar wakati akija kuchukua mzigo wa simu.

Ni swala la kujipa muda tu ataona mwanga
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu Kwa kijana wenu hapa, Mimi ni Mwalimu wa physics na chemistry nipo nkasi-rukwa, form six nilipata division two PCB point 11, nipo kwenye kufundisha Mwaka wa pili Sasa, naona ni wakati wa kuwaza nje ya box.

Kwenye Ili Chaka nimekuta watu wapo zaidi ya miaka 10 lakini vilio ni vingi sana, nadhani nisipofanya maamuzi sasahivi nitaenda kua kama wao tu, hakuna kitakachoharibika,

Nina-acces ya kukopa million 15/20 NMB/HAZINA. Japo za hazina kuzipata ni ngumu mno, nawaza vitu viwili nikasome au nitafute biashara nifanye?

Course ambayo nimeplan kwenda kusoma ni bachelor degree in business statistics and economics nadhani kwamba nikimaliza hii naweza fukuzia na kufanyiwa re-categorization.

Vipi wakuu niendelee kushika chaki huku nikifungua biashara? Au niende kusoma TU?.
Nenda kasome
 
Mkuu viazi vitamu au hivi wanaviita viazi ulaya
Viazi mviringo ,Irish potato ,mfano Mimi nitapanda wa 5 ibofwe kilolo ,ili vipishane kutoka na ludewa hivyo nitatoa watisa mwishoni. Na nitapanda mwezi 10 ,vitatoka wapili

Usilime lime tu ,unatakiwa ujue kila baada ya miezi mitatu mkoa Gani utakuwa unatoa viazi kwawingi ili msigongane sokoni
 
Back
Top Bottom