Nikasome degree nyingine au nifungue biashara?

Nikasome degree nyingine au nifungue biashara?

Mwaka wa pili kazini, unaenda kusoma miaka mitatu jumla sita..utarudi kusubiri recate..miaka mitatu..utarudi kazini unakuta hakuna nafasi ya hicho kipya ulichosomea...
Unaingia kwenye kundi la hao wanaolia.
Alafu nilisahau hii kusoma at least apande daraja ndo aende si ndio
 
Kwenye ualimu muda tunao, pia nataka nioe mwanamke ambae anao uwezo wa kusimamia biashara,
😂😂Uoe Kisha umpe biashara asimamie!?wewe mbona naona kama unaelekea kwenye kilio,hiki sio kigezo kizuri Cha kuoa mtagombana Kila siku na mke wako we muoe aje nyumbani Anza kuishi nae kama mke ukiona anaweza biashara mfungulie ya kwake sio aendeshe Yako mtagombana Kila siku hadi mshindwe kulana humo ndani aanze kulana na boda anae mletea mizigo
 
Asante, siendi kuchukua master's nilitaka nisome degree nyingine alafu nisubiri kufanyiwa re-categorization business ndio naiwaza zaidi mkuu.
Hiyo recategorization sio rahisi kama unavyo fikiria,kwanza itategemeana na uwepo wa nafasi katika Halmashauri yako-pia itategemana na huyo Mkurugenzi & Afisa Utumishi wako utake kiwepo kipindi una maliza hiyo shule yako.Hivyo,huo mpango bado ni probability na bado utatumia muda mrefu 3 years ya kusoma hiyo bachelor mpya plus 2 yrs ya kusubiri hiyo re-cate.

Sambamba na hilo bado ukifanikiwa kuifanya utaanzia chini,ambapo mshahara ni sawa na huo unaopata sasa hivi.
Ushauri wangu,tafuta biashara ndogo ambayo unaweza kusimamia mwenyewe katika hilo eneo ulipo-invest hiyo 15M na 5M weka kama akiba.
 
Nakuona kabisa huna skills na biashara hata ya kuchoma mahindi😂,

Wenye vichwa vya biashara hawaitaj elimu yoyote sanasana ndio wanaongoza kuajiri waliosoma,,

Nakuona kabisa fursa yako iko kwa kitabu na kuajiriwa.

Ongezea ujuzi wa Udereva,, kamata leseni yako,, alafu yakitokea machaka ya udere unaenda😂
 
Alafu nilisahau hii kusoma at least apande daraja ndo aende si ndio
Kweli kabisa..hapo kuna kizingiti cha kupata ruhusa na kwa vile anaenda kusoma kozi tofauti...ongeza uhaba wa walimu wa hayo masomo ya sayansi anayofundisha...
Aseme tu kuna gani huko za biashara ili tumsaidie mawazo.
 
umewaza vibaya ndio maana unasema biashara ni giza.

biashara ni rahisi sana iwapo utakubali kufata kanuni za biashara husika..ni kama 1+1=automatic jibu ni mbili. Ndio maana nimemshauri ajitafute katika biashara anayoiweza,atafute maarifa yake then afanye.

Hicho cheti ataishia kuwa mwajiriwa tu na kutumikia wengine.
Biashara ikienda wrong ndo atakumbuka bora angezihongea TU hizo Hela,umri unaruhusu mwajiriwa akiwa na cheti atakopa mara mbili ya hizo.
Biashara sio always ni kupata TU hata kama ulifanya feasibility study,kumbuka hakuna anaependa kutupa pesa kutoboa biashara ni uwe na uwezo wa kuvishinda vikwazo vyote kuanzia wachawi,wezi,serikali,madalali nk kumbuka nchi yetu haina mifumo ya kuvuta watu wafanikiwe kama ilivyo ulaya.
 
😂😂Uoe Kisha umpe biashara asimamie!?wewe mbona naona kama unaelekea kwenye kilio,hiki sio kigezo kizuri Cha kuoa mtagombana Kila siku na mke wako we muoe aje nyumbani Anza kuishi nae kama mke ukiona anaweza biashara mfungulie ya kwake sio aendeshe Yako mtagombana Kila siku hadi mshindwe kulana humo ndani aanze kulana na boda anae mletea mizigo
Hahaha, mkuu Mimi nimeichukua Kwa Mzee wangu, miaka yote mzee wangu anafanya biashara Mama ndio anakaa dukani mzee yeye ni kusafiri na kusepervise, lakini tokea tunasoma ukimuomba mama Hela alikua hawezi kutoa bila ridhaha ya baba, Sasa najiuliza sijui baba aliweza wapi? Mimi simpi mwanamke Hela afungue biashara then Mimi no relax, Kwa sababu ndoto yangu ni biashara nitafungua biashara ya ndoto yangu then yeye akae ndani kama msimamizi, sitajitenga na biashara natoka saa 7 school naenda kwenye biashara yangu ,mke akiniibia Mimi itakua afadhali kuliko kumuajiri kijana. Mimi maono yangu ndio hayo mkuu.
 
Hiyo recategorization sio rahisi kama unavyo fikiria,kwanza itategemeana na uwepo wa nafasi katika Halmashauri yako-pia itategemana na huyo Mkurugenzi & Afisa Utumishi wako utake kiwepo kipindi una maliza hiyo shule yako.Hivyo,huo mpango bado ni probability na bado utatumia muda mrefu 3 years ya kusoma hiyo bachelor mpya plus 2 yrs ya kusubiri hiyo re-cate.

Sambamba na hilo bado ukifanikiwa kuifanya utaanzia chini,ambapo mshahara ni sawa na huo unaopata sasa hivi.
Ushauri wangu,tafuta biashara ndogo ambayo unaweza kusimamia mwenyewe katika hilo eneo ulipo-invest hiyo 15M na 5M weka kama akiba.
Shukrani Asante, naichukua hii na nitalifanyia kazi, kusoma ni kwenda kupoteza muda na pesa, biashara ikikubali Wala sitawaza kwenda kusoma.
 
Nakuona kabisa huna skills na biashara hata ya kuchoma mahindi😂,

Wenye vichwa vya biashara hawaitaj elimu yoyote sanasana ndio wanaongoza kuajiri waliosoma,,

Nakuona kabisa fursa yako iko kwa kitabu na kuajiriwa.

Ongezea ujuzi wa Udereva,, kamata leseni yako,, alafu yakitokea machaka ya udere unaenda😂
Sawa mkuu. Lakini sikujua kama skills kwenye biashara inafundishwa.
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu Kwa kijana wenu hapa, Mimi ni Mwalimu wa physics na chemistry nipo nkasi-rukwa, form six nilipata division two PCB point 11, nipo kwenye kufundisha Mwaka wa pili Sasa, naona ni wakati wa kuwaza nje ya box.

Kwenye Ili Chaka nimekuta watu wapo zaidi ya miaka 10 lakini vilio ni vingi sana, nadhani nisipofanya maamuzi sasahivi nitaenda kua kama wao tu, hakuna kitakachoharibika,

Nina-acces ya kukopa million 15/20 NMB/HAZINA. Japo za hazina kuzipata ni ngumu mno, nawaza vitu viwili nikasome au nitafute biashara nifanye?

Course ambayo nimeplan kwenda kusoma ni bachelor degree in business statistics and economics nadhani kwamba nikimaliza hii naweza fukuzia na kufanyiwa re-categorization.

Vipi wakuu niendelee kushika chaki huku nikifungua biashara? Au niende kusoma TU?.
Umezunguka tuu mbuyu, ungesema tuu huutaki ualimu.

Kasome pharmacy uje ufungue duka lako la dawA
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu Kwa kijana wenu hapa, Mimi ni Mwalimu wa physics na chemistry nipo nkasi-rukwa, form six nilipata division two PCB point 11, nipo kwenye kufundisha Mwaka wa pili Sasa, naona ni wakati wa kuwaza nje ya box.

Kwenye Ili Chaka nimekuta watu wapo zaidi ya miaka 10 lakini vilio ni vingi sana, nadhani nisipofanya maamuzi sasahivi nitaenda kua kama wao tu, hakuna kitakachoharibika,

Nina-acces ya kukopa million 15/20 NMB/HAZINA. Japo za hazina kuzipata ni ngumu mno, nawaza vitu viwili nikasome au nitafute biashara nifanye?

Course ambayo nimeplan kwenda kusoma ni bachelor degree in business statistics and economics nadhani kwamba nikimaliza hii naweza fukuzia na kufanyiwa re-categorization.

Vipi wakuu niendelee kushika chaki huku nikifungua biashara? Au niende kusoma TU?.
Kama tayari una academic degree; ninakushauri uangalie upande mwingine. Elewa mimi ni mwalimu wa chuo kikuu wa muda mrefu sana, kwa hiyo nina attitude nzuri sana kuhusu elimu. Tatizo kubwa ni kwamba academic degrees nyingi siku hizi hazina ajira, kwa hiyo kama bado unataka kusoma basi usomee professional degree kama vile Engineering, Law, na Medicine ambazo unaweza kuzibadilisha mara moja kuwa biashara.

Elimu yako ya sasa ya Bachelors degree tayari imeshakupanua upeo kiasi kuwa unaweza kufanya utafiti wa jambo gani la kufanya kwa kutumia hizo pesa na zikazaa sana. Tanzania sasa hivi kuna opportunities nyingi sana ila hazina wakuzichimba. Acha biashara ya kununua bidhaa na kuziuza, bali tafuta biashara ya kuongeza value kwenye mali. Kuna value nyingine ni ndogo sana lakini zina return kubwa sana
 
Kama tayari una academic degree; ninakushauri uangalie upande mwingine. Elewa mimi ni mwalimu wa chuo kikuu wa muda mrefu sana, kwa hiyo nina attitude nzuri sana kuhusu elimu. Tatizo kubwa ni kwamba academioc degrees nyingi siku hizi hazina ajira, kwa hiyo kama bado unataka kusoma basi usomee professional degree kama vile Engineering, Law, na Medicine ambazo unaweza kuzibadirisha mara moja kuwa biashara.

Elimu yako ya sasa ya Bachelors degree tayari imeshakupoanua upeo kiasi kuwa unaweza kufanya utafiti wa jambo gani la kufanya kwa kutumia hizo pesa zikazaa sana. Tanzania sasa hivi kuna opportunities nyingi sana ila hazin wakuzichimba. Acha biashara ya kununua bidhaa na kuziuza, bali tafuta biashara ya kuongeza value kwenye mali. Kuna value nyingine ni ndogo sana lakini zina return kubwa sana
Shukrani sana mkuu, nimekuelewa,
 
Biashara ikienda wrong ndo atakumbuka bora angezihongea TU hizo Hela,umri unaruhusu mwajiriwa akiwa na cheti atakopa mara mbili ya hizo.
Biashara sio always ni kupata TU hata kama ulifanya feasibility study,kumbuka hakuna anaependa kutupa pesa kutoboa biashara ni uwe na uwezo wa kuvishinda vikwazo vyote kuanzia wachawi,wezi,serikali,madalali nk kumbuka nchi yetu haina mifumo ya kuvuta watu wafanikiwe kama ilivyo ulaya.
Atakopa mara mbili aendelee kuwa mtumwa wa madeni?? Kumbuka hyo mikopo Ina riba zake...

Ajitafute katika biashara,atakuja kunishukuru.
 
Back
Top Bottom