Nikiiangalia hii picha ya Nape naona kuna shida kubwa kwa hawa viongozi wetu

Nusu ya watu Tanzania hawana elimu na ndio wapiga kura wengi, sasa kotakana na wengi wao wanachagua mjinga mwenzo kuwaongoza, kwaiyo hata ukiwaona hawa viongozi maamuzi wanayoaamua usiwalaumu sana kwani wapiga kura na akili zao ndio hizo hizo..
 
Sasa kama wenyewe walitaka wapandiliwe....
Juu ya migongo yeye angefanyaje.....
Yaan,
Ni vituko juu ya vituko Jk1, JK 2, mkapa,mwinyi, JPM wasinge kubali huu upuuzi...
Hapo hakuna tofaut na kutafuta kiki.........
 
unakuta huyo ni mke wa mtu au mama ake mtu
 
Wote CCM hao!!
 
Uyu na yule mchungaji alieua watu takriban 90 nchini kenya kwa kwajaza imani ya kutokula mpaka wafe ili onana na Yesu hawana tofauti kabisa

Yani unakanyaga makalio ya wenzio kisa kuonekana unakubalika kisiasa, sasa bora angewakanyaga makalio akiwa peku, ila kala kiatu alafu anawakanyaga,

Na nasema ccm ni wajinga ila wajinga kivile huwezi mkanyaga makalio hujatoa rushwa ya pesa hakuna ,hapo kila alielala chini juwa hamtumikii Nape bali tu ile pesa kalipwa basi,

Naongea hili kwa kujiamin ,kama kweli walilala wakanyagwe makalio yao kwa mapenzi yao Nape ajitokeze kulipinga,

Asije pindisha ukweli , maana kiama , itakua juu yake ,asema Bwana
 
Mkuu hayo ndiyo madhara ya mchanganyiko wa ujinga na upumbavu kwa pamoja! Hawa ndiyo watu wa kariba ya Kibwetere ama Mackenzie. Wao hufanya mambo kwa kadiri ya mahitaji ya jamii duni na maskini zilivyo.

Jamii kama hizi zitawaliwa na mila na desturi ambazo ni mbovu, na wala haziendani na ustaarabu wa kisasa,. Badala ya kiongozi kuwa "agent of changing behavior" yeye ndiyo kwanza anaona sifa ya kuendeleza hali kama hiyo.

Akili kama hizi ndiyo zile zile za kupiga "push-ups" mbele za watu badala ya kuinadi ilani ya chama, kupiga deki barabarani ili mgombea unayempenda apite juu yake, kusukuma gari la kiongozi, viongozi wa kitaifa kwenda kwa Babu wa Loliondo kupata kikombe chake cha dawa,

Kiongozi ni lazima awe kichocheo cha mageuzi ya fikra pevu na chanya kwa wale anaowaongoza. Ni vyema awe mstari wa mbele kuwashauri waachane na mambo ambayo hayana tija yoyote kwao na kwake binafsi.

Ni lazima kiongozi atumie njia fikirishi ili kuibadirisha jamii anayoishi, anayoiongoza, ama kutaka kuiongoza. Azitumie ziwe kama zana (tools) za mabadiliko, njia mbadala (alternative means) ya mabadiliko, na vilevile ziwe ndizo wakala wa mabadiliko (agent of change) kwa wale anaowaongoza.
 
Akiambiwa kuhusu hilo tukio huwa anakuwa mkali sana kutetea ni utamaduni wao![emoji1787]
 
Inavyokumbuka walimlazimisha awakanyage na akaambiwa akikataa kimila ni jambo baya..Sasa hapo mtu ufanyaje?? Hakuna haja kulalamika nimila zao nawao wanafurahia kukanyagwa chamsingi mamila ya kijinga tuyaache tusimtuhumu mtu maana ukikahidi unawea pigwa na mapigo ya kimizimu
 
Lakini huyu baba mweee... but hayo yanayokanywagwa nayo vipi😡
😡😡
 
Hakuna kitu kama hicho. Huyo mhusika hana akili. Wewe mama yako akikwambia umkanyage matakoni utakubali?
 
Bora hao ,wanaovuliwa chupi kanisani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…