Nikija kuwa na familia kuna vitu sintoruhusu

Nikija kuwa na familia kuna vitu sintoruhusu

Acha roho mbaya we mwanadamu maisha ni watu ubinafsi kwenye maisha sio kitu kizuri leo hii ukifa utazikwa na wanadamu ivyo naomba utambue maisha ni watu ukiwa mbinafsi kupitiliza itakugharimu sana badilika ndugu
 
Wapi tutimbe?
Mimi nipo New York City. Mji wa watu wanaojua kushika hamsini zao na kutojali ndugu.

Lakini najua kutembelewa na wageni na mimi kutembelea wenzangu.

Nishapitia hizo stages zote za kukataa kutembelewa na kutembelea watu, nikazimaliza zote.
 
Mimi nipo New York City. Mji wa watu wanaojua kushika hamsini zao na kutojali ndugu.

Lakini najua kutembelewa na wageni na mimi kutembelea wenzangu.

Nishapitia hizo stages zote za kukataa kutembelewa na kutembelea watu, nikazimaliza zote.
Nini kilikutoa kwenye stage ya kutotembelea watu?
 
unatukana mamba na hujavuka mto chimamy, kwasababu ya uchumba mtamu sio!?, subir uolewe,sisi unaotufukuza ndo utakuja kutuomba ushaur mbon Mr kabadilika sana,,sasa binti tutakukatia cm.
 
Be warry of friends-they will betray you more quickly,for they are easily aroused by envy.
 
Lord protect me from my friends; i can take care of my enemies..VOLTAIRE
 
Nini kilikutoa kwenye stage ya kutotembelea watu?
Kwa kweli mpaka sasa mimi si mtu wa kutembelea watu sana.

Na ingawa nambana mtoa mada, naelewa sana anavyofikiri, kwa sababu hata mimi nimepitia huko.

Sasa hivi kuna mambo mengi sana, na hata tunapombana mtoa mada ajifikirie zaidi, inatubidi tumuelewe. Maneno mengine hayasemwi bure, inawezekana kapitia, kaona au kasikia kitu cha kumpa sababu nzuri za kupanga anavyopanga.

Kuhusu mimi, kuna wakati nilikuwa na focus sana kwenye mambo yangu, kusoma, kuji establish katika kazi, kula bata mwenyewe, kuanzisha famikia yangu.

Halafu, baada ya kuji establish mwenyewe, kuweka himaya yangu, kuanzisha familia yangu, nikaona umuhimu wa kuwa na mahusiano na jamii, familia. Hata kama si kila mtu, kuwa na watu wangu wachache ambao nakuwa nao karibu. Nikawa hata kama sihitaji ku interact na kila mtu, kuna key focal points za jamii, wale viongizi, nakutana nao, nawatembelea. Na wao wananitembelea.

Najivunia sana uwezo wa kuwa na kwangu na ndugu zangu, jamaa na marafiki wakifika Marekani wawe na sehemu ya kufikia.

Mathalani mwaka juzi kuna vijana wawili wa familia (extended) wamekuja kuanza chuo Marekani, wadogo sana, mara yao ya kwanza kuja Marekani, hawamjui mtu. Nikaenda JFK Airport hapa New York kuwapokea, wakakaa nyumbani kwangu siku chache, nikawapeleka mpaka chuoni kuwaandikisha, sasa wanakaribia kumaliza chuo. Wanajua kuwa Marekani kina nyumba ni kwao, wana sehemu ya kufikia.

Kuna kijana kaja mwaka jana kutoka Tanzania kama scholar hapa Marekani, nimekaa naye sikunkadhaa, kafurahi sana kukutana na Mtanzania Marekani.

Kuna mtoto alikimbia kwao Houston akija New York City, kitu cha hatari sana kwa kuwa kuna watu wanateka watu. Nikapigiwa simu na famikia kutoka Dar kumtafuta na kumchukua, akakaa kwangu mpaka alivyopata kutukia na kurudi kwao.

Sasa kaka mkubwa balozi asiye rasmi wa famikia moja ya function yangu ni kuwa na sehemu ambayo ndugu zangu wanaweza kufikia. Nikisema nifunge vioo hata sababu ya mimi kuwa nililo inaondoka.

Ila pia, naelewa matatizo mengi ya kijamii yanayoweza kusababisha watu wafunge vioo.

Issue si kufunga vioo au kutofunga vioo, issue ni kuwa na chujio la kujua unamruhusu nani awe karibu nawe na nani humruhusu.

Naelewa ukifungua madirisha ili hewa safi iingie, unaweza kuruhusu nzi waingie ndani. Lakininunaweza kuweka wavu hewa safi iingie na nzi wasiingie.

Ukiwafungia sana watu vioo, unaweza hata kujifungia wewe mwenyewe advantages fulani.
 
All working situations require a kind of distance between people... Ukiwa mtu unaeweza kuwa jaji watu ,lazima kuna mipaka utaweka ili kupunguza mazoea yaliyopitiliza. Maana watu wakikujua sana in and out ndio mwanzo wa anguko lako. Mtoa mada yupo sahihi kwa maoni yake.
 
Moja ni kuwaalika ndugu zangu nyumbani kwangu ambapo watoto wangu wanaishi na sio ndugu zangu tu hata ndugu wa mume.

Kingine marafiki , wachungaji ,mazoea sitaki.
Majirani wote siwataki kabisaa .

Na mawatu tu ambao hawajui kwanini wanakuja .

Kwangu pawe kwangu tu hawa watu hawana wema ni wanakuja tu kuharibu maisha ya watoto wako. Kabisa ..... hauoni leo ila baadaye wakitaka kuoa , kupata kazi , kuoelewa, kutafuta riziki hapo sasa mnaanza usumbufu usio hitajika.

Labda huyo mtu awe anajitambua . Aisee maana watu ni wanafiki sana.
Na wewe usikanyage kwao maana ni nuksi kwao pia.

Kingine ukifanya birthday party, komunio, kipaimara, graduation ya mwanao usiwaalike waje nyumbani kwako pika kula mwenyewe hvyo vyakula na vinywaji maana hawawezi kuwa wazuri siku hiyo ikiwa miaka yote ni wabaya.
 
All working situations require a kind of distance between people... Ukiwa mtu unaeweza kuwa jaji watu ,lazima kuna mipaka utaweka ili kupunguza mazoea yaliyopitiliza. Maana watu wakikujua sana in and out ndio mwanzo wa anguko lako. Mtoa mada yupo sahihi kwa maoni yake.
Key words "a kind od distance" "kuwa jaji watu" "mipaka".

Haitakiwi kujifungia kabisa wala kujiachia kabisa, kunatakiwa juwa na mipaka iliyofikiriwa vizuri sana.
 
Back
Top Bottom