Nini kilikutoa kwenye stage ya kutotembelea watu?
Kwa kweli mpaka sasa mimi si mtu wa kutembelea watu sana.
Na ingawa nambana mtoa mada, naelewa sana anavyofikiri, kwa sababu hata mimi nimepitia huko.
Sasa hivi kuna mambo mengi sana, na hata tunapombana mtoa mada ajifikirie zaidi, inatubidi tumuelewe. Maneno mengine hayasemwi bure, inawezekana kapitia, kaona au kasikia kitu cha kumpa sababu nzuri za kupanga anavyopanga.
Kuhusu mimi, kuna wakati nilikuwa na focus sana kwenye mambo yangu, kusoma, kuji establish katika kazi, kula bata mwenyewe, kuanzisha famikia yangu.
Halafu, baada ya kuji establish mwenyewe, kuweka himaya yangu, kuanzisha familia yangu, nikaona umuhimu wa kuwa na mahusiano na jamii, familia. Hata kama si kila mtu, kuwa na watu wangu wachache ambao nakuwa nao karibu. Nikawa hata kama sihitaji ku interact na kila mtu, kuna key focal points za jamii, wale viongizi, nakutana nao, nawatembelea. Na wao wananitembelea.
Najivunia sana uwezo wa kuwa na kwangu na ndugu zangu, jamaa na marafiki wakifika Marekani wawe na sehemu ya kufikia.
Mathalani mwaka juzi kuna vijana wawili wa familia (extended) wamekuja kuanza chuo Marekani, wadogo sana, mara yao ya kwanza kuja Marekani, hawamjui mtu. Nikaenda JFK Airport hapa New York kuwapokea, wakakaa nyumbani kwangu siku chache, nikawapeleka mpaka chuoni kuwaandikisha, sasa wanakaribia kumaliza chuo. Wanajua kuwa Marekani kina nyumba ni kwao, wana sehemu ya kufikia.
Kuna kijana kaja mwaka jana kutoka Tanzania kama scholar hapa Marekani, nimekaa naye sikunkadhaa, kafurahi sana kukutana na Mtanzania Marekani.
Kuna mtoto alikimbia kwao Houston akija New York City, kitu cha hatari sana kwa kuwa kuna watu wanateka watu. Nikapigiwa simu na famikia kutoka Dar kumtafuta na kumchukua, akakaa kwangu mpaka alivyopata kutukia na kurudi kwao.
Sasa kaka mkubwa balozi asiye rasmi wa famikia moja ya function yangu ni kuwa na sehemu ambayo ndugu zangu wanaweza kufikia. Nikisema nifunge vioo hata sababu ya mimi kuwa nililo inaondoka.
Ila pia, naelewa matatizo mengi ya kijamii yanayoweza kusababisha watu wafunge vioo.
Issue si kufunga vioo au kutofunga vioo, issue ni kuwa na chujio la kujua unamruhusu nani awe karibu nawe na nani humruhusu.
Naelewa ukifungua madirisha ili hewa safi iingie, unaweza kuruhusu nzi waingie ndani. Lakininunaweza kuweka wavu hewa safi iingie na nzi wasiingie.
Ukiwafungia sana watu vioo, unaweza hata kujifungia wewe mwenyewe advantages fulani.