Nikija kuwa na familia kuna vitu sintoruhusu

Mtoa mada ni tofauti na wewe, na mazingira ya nchi uliyopo, Labda kama yupo ughaibuni, anataka abakie yeye na mumewe tu hataki ndg wa upande wowote, jirani, wachungaji nk kibongo bongo hiyo ni haiwezekani hata uwe unajiweza vipi kiuchumi

Ndio maana nikamwambia anaota, sababu yeye binafsi anaweza kuishi hivyo ila sio kwa mwenzi au watoto nk

Mi pia si mpenda muingiliano hivyo lakini sio kama mtoa mada
 
Wanakuwinda tu wakishakupatia utakuja toa post unaomba ushauri hujielewi
 
Tangu nakua mpaka sasa nazeeka nimekua nikiamini na nitaendelea kuamini kuwa wakubwa wanakutana baa/BAR sio majumbani.
 
Lakini kasema hatajifungia kabisa watu fulani wanaojielewa atawafungulia.

Kufungulia mnaanza kidogo kidogo, halafu mkishatuamini mnatupa yote 🤣🤣🤣
 
Lakini kasema hatajifungia kabisa watu fulaninwanaojielewa atawafungulia.

Kufungulia mnaanza kidogo kidogo, halafu mkishatuamini mnatupa yote 🤣🤣🤣
Unaona hapo eti ananipa tahadhari😅😅😅hili kweli debe tupu
 
Unaona hapo eti ananipa tahadhari😅😅😅hili kweli debe tupu
Ujue kujinafasi ni haki ya kikatiba.

Mimi huwa najiapiza kuna nchi fulani sitakwenda daima kwa sababu za kifalsafa, kupingana na misimamo yao.

"Huku Russia huku, sitakaa nikanyage daima, Putin mshenzi sana kavamia Ukraine, siendi ng'o".

Wakati nilikuwa siendi Russia, hata kabla Russia haijavamia Ukraine.
 
Ukiwa single mother utafanikiwa hilo. Ila ukienda kuishi kwenye maisha ya mwanaume, nyumbani kwake kakuoa wewe umekuta anatembelewa na ndugu zake wanaishi bila shida, wewe ndo uende ukaweke sheria zako......aisee labda kama jamaa hawezi kuinua mdomo kwako.
Na hilo ukifanikiwa basi hiyo ndoa umejioa
 
Na wala huu sio ubinafsi.

Watu wana mazoea ya ajabu sana na nyumba za watu. Unamkaribisha mtu na yeye anakaribisha watu
 
Kuna kaka yetu katika ukoo. Ameoa na watoto wa2. Kuna kipindi mke wake kalibia anaelekea kujifungua mtoto wa3 alianguka na pikiliki akateguka mguu kiasi akawa imobile kwa miezi3.

Mume wake akiwa anarudi kutoka mkoani alipo lazwa mkewe, akapata ajali na kuvunjika miguu na mkono nae akawekewa hogo na kua immobile.

Wote walipotoka hospitali wakaenda kuishi kwa kaka yake na mumd kwa miezi2.

Tunza akiba ya maneno binti
 
Mimi nakuelewa mleta mada, naomba tuijenge family nzuri nitakupenda,kukuheshimu na kukujali daima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…