Nikilala baada ya muda kuna kitu mwilini kinakuja kinanivaa kwa nguvu na kunibana

Nikilala baada ya muda kuna kitu mwilini kinakuja kinanivaa kwa nguvu na kunibana

Chunguza afya yako kikamilifu, ukiona uko poa, muone Jr Mshana kwa ushauri.
 
Habari wana JF,

Moja kwa moja niende kwenye mada jamani kumekua na hili tatizo limekua likinitokea mara kwa mara hasa ninapo lala si mchana si usiku yaani ninapo lala baada ya muda nasikia kuna kitu mwilini kinakuja kinanivaa kwanguvu kinanibana.

Pengine nakua nahisi mpaka kukosa pumzi kabisa basi nakua kama napambana nacho mpaka ninapo stuka toka usingizini nakua nahema sana jasho linanitoka muda mwingine nakua nahisi kichwa kinagonga na koo kukauka hii mara nyingi inakua ni usiku.

Lakini ninapokua nimepumzika mchana na kupitiwa na usingizi hali hii yenyewe inakua tofauti kidogo yaan naanza kuhisi kama kizungu zungu hivi wakati huo nakua nipo usingizini na muda kidogo nasikia tena kitu kinanivaa mwilini na kunikaba kwa nguvu basi nakua napambana nacho kwa nguvu zote hatimae nakishinda na ndipo ninapo stuka haraka na kutoka usingizini.

Hii kitu imekua ikinisumbua sana mwenye ufaham kuhusu hii kitu naomba anisaidie.
Hilo jinamizi mkuu ,yaan wanasema unalala vibaya ? Yan kila siku ndio ulale vibaya? Jamani haya mambo ya majinamizi ,majinamizi ni roho chafu ambazo huzunguka duniani na kuwachezea watu dhaifu .Jaribu kumrudia Mungu yaani halitakaa likutokee ,utaniambia
 
Ungeongea bila kunitukana ungepungukiwa nini? Hayo mapepo yatakutesa sana tuu na yatablock Kila kitu kwenye maisha yako mpaka utubu na kumwamini Yesu

Ukiamini Yesu sio kila mtu anaamini huyo unae muamini wengine tunaamini tofauti na unavyo amini.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Mkuu hujafafanua haswa hicho kitu kinapambana kukuvua nguo au haswa kinataka nn?

Usije ikawa umehamia nyumba watu wanatafunwa.
 
Pole sana
huyo ni pepo mbaya..kama ni mtumiaji wa bible uwe unasoma zaburi23 na 91 kabla ya kulala.
 
Hali kama hizi huwa zinasababishwa na kukosa mahitaji muhimu ya mwili katika shughuli zake zakila siku (body physiological functions), hasa hasa wakati ukiwa haujitambui (unconscious), mfano; usingizini.

Inategemea na sehemu gani yamwili imekosa hayo mahitaji na ndio itakayokujia ndotoni kua imebanwa. Hii ni kazi ya ubongo ukiwa hujitambui 4 4 4=fo fo fo, kwaiyo ubongo unatafuta njia mbadala yakukushitua ili ukae sawa.

MFANO 1:
Kama mfumo ulioathiliwa ni wa upumuaji labda ulilalia pua hivyo mwili ukawa unakosa hewa (oxygen) yakutosha katika maeneo nyeti (sensitive organs) kama vile ubongo, moja kwa moja hapa ndoto itakayo kujia ni inahusu kubanwa pumzi, Lini?, wapi? na nani?, kiasi gani umebanwa? Ubongo utaoketeza data zilizopo kwenye center husika ya huohuo ubongo, apa itategemea na mazingira unayo pigia shughuli zako.

MFANO 2:
Kuna watu wengine wanaota wamebanwa tumbo sasa hapa mfumo uliohalibiwa ni mfumo wa umeng'enyaji chakula aidha umelala na njaa kali au umelalia tumbo vibaya. Kwahiyo harakati za vimeng'enyo kupambana na ukuta wa tumbo badala ya chakula kule tumboni ubongo unapata breaking news kua mkuu eee!!? kimeumana tumboni uku...! apo ubongo unajua nini cha kufanya.

Kwaiyo mambo mengi ni inakuaga utendaji kazi wakawaida tu wa mwili tusiegemee saana kwa Sir🥁.
Thanks
 
Habari wana JF,

Moja kwa moja niende kwenye mada jamani kumekua na hili tatizo limekua likinitokea mara kwa mara hasa ninapo lala si mchana si usiku yaani ninapo lala baada ya muda nasikia kuna kitu mwilini kinakuja kinanivaa kwanguvu kinanibana.

Pengine nakua nahisi mpaka kukosa pumzi kabisa basi nakua kama napambana nacho mpaka ninapo stuka toka usingizini nakua nahema sana jasho linanitoka muda mwingine nakua nahisi kichwa kinagonga na koo kukauka hii mara nyingi inakua ni usiku.

Lakini ninapokua nimepumzika mchana na kupitiwa na usingizi hali hii yenyewe inakua tofauti kidogo yaan naanza kuhisi kama kizungu zungu hivi wakati huo nakua nipo usingizini na muda kidogo nasikia tena kitu kinanivaa mwilini na kunikaba kwa nguvu basi nakua napambana nacho kwa nguvu zote hatimae nakishinda na ndipo ninapo stuka haraka na kutoka usingizini.

Hii kitu imekua ikinisumbua sana mwenye ufaham kuhusu hii kitu naomba anisaidie.
Kama wewe muislamu ingia mitandaoni dowloand surat ul bakarah, ama ayat ul kursy na sura nyengine za kurani kisha usiku ukilala washa hizo rekodi zikeshe zinasoma kurani ama weka redio ya kiislamu unayosoma kurani usiku kucha. Kwenye hadithi za mtume tu naamini malaika wa mwenyezi mungu hutembelea na kulinda watu katika nyumba zenye kusoma kurani pia majini wabaya na wachawi huogopa na kukimbia inaposomwa surat ul kursy kwa sababu inaapia kuwa mungu ni mkuu nao huwa hawapendezwi kuusikia hivyo.

Kama mkristo download au tafuta rekodi ya maombi ya kufukuza vitu vibaya na mungu kukulinda.

Pia sali
Pengine unaishi bila ibada
Ibada hufukuza vitu vya ajabu kwenye nyumba
 
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom